Sunday, June 30, 2013

Mhe. Membe ashuhudia uwekwaji saini mkataba wa biashara kati ya Tanzania na Malaysia


Mhe. Membe (wa tano kutoka kushoto waliosimama nyuma) akiwashuhudia Bw. Mufuruki na Bw. Choi Gyu Sung, Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HU-CHEMS wakisaini mkataba huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimsikiliza Bw. Ali Mufuruki, Mwenyekiti na Mkurugenzi wa Makampuni ya Infotech Investment Group ya Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kuweka saini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara katika masuala ya Teknolojia  na Kampuni ya HU-CHEMS kutoka Malaysia.Hafla hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere pembezoni mwa Mkutano unaoendelea wa Smart Partnership.

Mhe. Membe akiendelea kumsikiliza Bw. Mufuruki (hayupo pichani). Wengine katika picha ni Balozi Mbelwa Kairuki (kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia.

Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Ki Tai Kim P.E. mmoja wa viongozi kutoka Kampuni ya HU-CHEMS ya Malaysia wakati wa uwekaji saini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya Teknolojia na Kampuni ya Tanzania.

Bw. Mufuruki na Bw.Choi wakibadilishana mkataba huo mara baada ya kuusaini.

Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Mufuruki na Bw. Choi na Wajumbe wengine kutoka Malayasia na Tanzania mara baada ya kusainiwa Mkataba huo akiwemo Bibi Joyce Mapunjo (kushoto), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Balozi Mbelwa (kushoto), Bi. Zaituni na Bw. Omar Mjenga wakishuhudia uwekwaji saini huo.

Mhe. Membe akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu mkataba uliosainiwa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.