Monday, December 30, 2013

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 
 
220px-Coat of arms of Tanzania.svg f1f71
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa itashiriki katika hafla ya makabidhiano ya magari ya msaada kutoka Serikali ya China katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam, tarehe 31 Desemba 2013, saa 3:00 asubuhi.
 
Hafla hiyo itahudhuriwa na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Wizara ya Fedha, pamoja na Ubalozi wa China hapa nchini.
 
 
Imetolewa na:
 
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
 
Dar es Salaam
 
30 Desemba, 2013.
 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.