Wednesday, March 9, 2016

Rais wa Vietnam afungua Kongamano la Pili la Biashara kati ya Tanzania na Vietnam.


 Rais wa Vietnam, Mhe. Truong Tan San kwa pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim wakiwa meza kuu kabla ya kufungua rasmi  Kongamano la Pili la Biashara kati ya Tanzania na Vietnam lililofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

 Rais wa Vietnam,  Mhe. Truong Tan Sang akifungua rasmi Kongamano la Pili la Biashara kati ya Tanzania na Vietnam  ambapo alieleza  nia ya wazi ya Serikali yake ya kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Teknolojia, Kilimo na biashara ili  kuzidi kuimarisha uhusiano.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa akiwasilisha mada katika Kongamano hilo ambapo alieleza kuwa uhusiano wa Tanzania na Vietnam ni mzuri hivyo ni vema sasa wananchi wa nchi zote mbili wakatumia fursa hiyo katika kuwekeza katika biashara na viwanda ili kukuza uchumi.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage akitoa mada ambapo alieleza fursa za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania  na akawakaribisha wafanyabiashara wa Vietnam kuja kuwekeza nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara nchini, Mhe. Regnald Mengi akiwasilisha mada katika Kongamano hilo ambapo alieleza kuwa wafanyabiashara nchini Tanzania wapo tayari kushirikiana na wafanyabiashara wa nchini Vietnam.
Washiriki wa kongamano wakifuatilia ufunguzi wa kongamano hilo.


Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akifuatilia ufunguzi Kongamano hilo.


Mkataba wa Makubaliano ya  Ushirikianmo katika masuala ya Uwekezaji kati ya Tanzania na Vietnam ukisainiwa
Mhe. Rais Truong na Mhe. Majaliwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Viongozi kutoka sekta mbalimbali
Picha ya pamoja

Tanzania isiogope kujifunza kutoka katika nchi zilizoendelea, Dkt. Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli amesema kuwa nchi yake ina mambo mengi ya kujifunza kutoka Vietnam, nchi ambayo kwa kipindi kifupi imeweza kujikwamua kutoka katika dimbwi la umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati. Rais Magufuli alisema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam leo akiwa na Mgeni wake, Mhe. Troung Tan Sang, Rais wa Vietnam mbele ya waandishi wa habari. 

“Vietnam ilipata uhuru mwaka 1945 na baadaye ikakumbwa na vita vya muda mrefu ambapo utulivu kamili katika nchi hiyo ulipatikana kuanzia mwaka 1976. Kuanzia kipindi hicho, Vietnam imeweza kupiga hatua kutoka nchi masikini yenye kipato cha Dola za Marekani 100 kwa mtu mmoja na kufikia nchi yenye uchumi wa kati wa pato la Dola 2000 kwa mtu mmoja kwa mwaka”. Rais Magufuli alisema.

Mhe. Dkt. Magufuli alieleza kuwa uhusiano kati ya Tanzania na Vietnam ni mzuri na unazidi kuimarishwa na ziara za viongozi wa ngazi ya juu baina ya nchi hizi mbili. Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamin Mkapa alifanya ziara nchini Vietnam mwaka 2004 na baadaye Rais wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Kikwete mwaka 2014.  Aidha, Rais Magufuli amealikwa kufanya ziara nchini Vietnam mwaka 2017.

Rais Magufuli aliendelea kueleza kuwa Vietnam ni maarufu kwa kuuza korosho duniani wakati mbegu za zao hilo ilizichukua Tanzania. Vietnam pia inavuna mpunga misimu mitatu kwa mwaka wakati Tanzania inavuna kwa msimu mmoja tu. Mbali na hayo, Vietnam ni maarufu kwa uuzaji wa samaki duniani lakini Tanzania yenye maziwa 21, bahari na mito haina hata kiwanda cha kusindika samaki. “Hivi ni vitu ambayo Tanzania inatakiwa kujifunza kutoka Vietnam” Rais Magufuli alisisitiza.

Alieleza kuwa katika mazungumzo na Mgeni wake walisisitiza umuhimu wa kukuza biashara kati ya Tanzania na Vietnam kutoka kiwango cha sasa cha Dola za Marekani milioni 300 na kufikia Dola bilioni moja kwa mwaka.

Kwa upande wake, Rais wa Vietnam alielezea furaha yake ya kuwa Rais wa kwanza wa Vietnam kufanya ziara katika nchi nzuri ya Tanzania. Alisema licha ya umbali uliopo kati ya Tanzania na Vietnam lakini Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kabisa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Vietnam. Rais Tang aliipongeza Tanzania kwa ukuaji imara wa uchumi na kwamba wamekubaliana na mwenyeji wake kuanzisha Tume ya Pamoja ya Ushirikiano ili kuimarisha ushirikiano katika sekta za kilimo, uvuvi, biashara, mawasiliano kwa faida ya wananchi wa pande zote.

Kwa upande wa masuala ya kimataifa wamekubaliana suala la amani lipewe kipaumbele na umuhimu wa kuzingatia sheria za kimataifa katika kushughulikia migogoro duniani.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (Kushoto) akimkaribisha Mgeni wake, Rais Truong Tan Sang wa Vietnam ambaye yupo nchini kwa Ziara ya Kitaifa ya siku tatu.
Rais Truong pamoja na Mkewe, Bi. Mai Thi wakipokea maua wakati walipowasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli (kulia) pamoja na Mgeni wake, Rais wa Vietnam wakitembea pamoja.
Viongozi Wakuu wa Serikali wakishuhudia mapokezi ya Rais wa Vietnam yakiendelea katika viwanja vya Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli pamoja na Mgeni wake, Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tan Sang wakiwa kwenye jukwaa tayari kwa ajili ya kupigiwa Wimbo wa Taifa uliyoambatana na Mizinga 21, kisha kukagua Gwaride la Heshima
Kikosi cha bendi cha Polisi kikipiga nyimbo za Mataifa yote mawili wakati wa mapokezi ya Rais wa Vietnam (hayupo pichani)
Rais Truong Tan Sang akikagua gwaride la heshima

Rais Magufuli pamoja na Mgeni wake, Mhe. Truong Tan Sang wakisalimiana na wananchi waliojitokeza katika mapokezi hayo 
Waandishi wa Habari nao wakiwa kazini kwa kuchukua matukio muhimu wakati wa mapokezi ya Rais Truong Tan Sang (hayupo pichani). Kiongozi huyo ameambatana na waandishi 22 wa habari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tan Sang
Rais wa Tanzania (kulia) na Rais wa Vietnam na wake zao wakiwa katika moja ya vyumba vya kupokelea wageni mashuhuri, Ikulu Dar es salaam.
Rais Magufuli (kulia) akifanya mazungumzo na mgeni wake, Mhe. Tan Sang. Katikati yao ni Mkalimani wa Rais Tan Sang 
Rais Dkt. Magufuli akiongea na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara hiyo.
Rais Tan Sang naye akiongea na waandishi wa habari kuhusu ziara hiyo ambapo ni mara yake ya kwanza kufika Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ambaye pia alikuwa muendeshaji mkutano wa waandishi wa habari Bw. Gerson Msigwa akipitia ratiba. Wanaomwangalia kutoka kushoto ni Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Vietnam Bw. Le Hai Binh na mwenyeji wake Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania Bi. Mindi Kasiga 
Kaimu Mkuu wa Itifaki Bw. James Bwana akipokea maagizo kutoka kwa Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli
Rais Magufuli (kulia) akimsikiliza Rais Truong Tan Sang alipokuwa akimweleza jambo kabla ya mazungumzo yao na vyombo vya habari
Viongozi mbalimbali wa Tanzania na Vietnam pamoja na waandishi wa habari wakiwasikiliza kwa makini Marais wa Tanzania na Vietnam (hawapo pichani)

Picha na Reginald Philip.



Mke wa Rais wa Vietnam atembelea Ofisini kwa Mama Magufuli na Makumbusho ya Taifa

Mke wa Rais wa Vietnam, Mama Mai Thi Hahn akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli zilizopo Ikulu, Dar es Salaam. Mama Mai Thi Hahn ameambata na Mhe. Rais wa Vietnam Toung Tang San ambaye yupo nchini kwa ziara ya siku 4 kuanzia tarehe 8 Machi 2016.
Mama Mai Thi Hahn akiwasalimia wanawake waliokuja kumlaki katika ofisi za Mhe. Mama Magufuli.
Mama Mai Thi Hahn akisalimiana na mmoja wa wasanii wa vikundi vya ngoma vilivyofika kumlaki katika eneo la Ofisi za Mama Magufuli
Mama Mai Thi Hahn akieleza umuhimu wa ziara yake na Mhe. Rais Toung Tang San ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano  wa kihistoria uliopo kati ya nchi yake na Tanzania.
Mama Magufuli akimkabidhi Mama Mai Thi Hahn zawadi ya Kinyago mashuhuri cha "Umoja" kilichochongwa nchini Tanzania.
Pia Mama Mai Thi Hahn naye alikabidhi zawadi kwa Mama Magufuli.
Wake za Marais wakicheza ngoma na kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitumbuiza ofisini hapo.
Mama Hahn na Mama Magufuli wakiagana na kina mama (hawapo pichani) mara baada ya kutembelea ofisini

 ..........Alipotembelea Makumbusho ya Taifa

Mama Hahn na Mama Magufuli wakisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Makumbusho ya Taifa mara baada ya kuwasili.
Mama Mai Thi Hahn akisaini kitabu cha Wageni katika Ofisi za Makumbusho za Taifa
Mwenyeji wake Mama Janeth Magufuli naye akisaini kitabu cha wageni katika ofisi hizo.
Wakipokea maelezo ya Michoro kutoka kwa afisa wa makumbusha ya Taifa hayupo pichani inayoeleza historia ya nchi ya Tanzania na namna Wasanii walivyoweza kuwa wabunifu kwa kuchora picha nzuri zinazoeleza historia ya Taifa.
Afisa wa Makumbusho akiendelea kuelezea michoro mingine na maana zake ambapo makumbusho hiyo imekuwa ikihifadhi kumbukumbu hizo kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo katika kurithisha historia na wageni kuweza kuijua historia ya Tanzania
Wakiendelea kupokea maelezo.
Wakielezewa na Afisa wa Makumbusho ya Taifa  kuhusu picha zinazoonyesha historia ya utumwa ambapo wakati wa Ukoloni Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi ambazo watumwa walichukuliwa.
Maelezo juu ya  biashara ya pembe za ndovu enzi za ukoloni  yakiendelea kutolewa.
Mara baada ya kumaliza ziara hiyo Wake za Marais kwa pamoja walikabidhiwa zawadi ya vikapu vya asili na ofisi ya Makumbusho ya Taifa.

Rais wa Vietnam awasili nchini kuanza ziara ya kwanza ya kitaifa

Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Mhe. Truong Tang San (kushoto) pamoja na mkewe Mama Mai Thi Hann wakipunga mkono mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere kwa ajili ya kuanza ziara ya kwanza ya kitaifa nchini.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimpokea Rais wa Vietnam Mhe. Troung Tang San kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya kuwasili nchini
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa (kulia) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga ( wa pili kushoto) kwa Rais wa Vietnam Mhe. Truong Tang San (mwenye tai ya Blue).
Rais Truong Tang San akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Autralasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki
Rais Troung Tang San pamoja na Mkewe Bi. Mai Thi Hahn (mwenye nguo ya bluu) wakitizama kikundi cha ngoma kilichokuwapo Uwanja wa Ndege.
Waziri wa Mambo ya Nje akizungumza na waandishi wa habari waliojitokeza kumlaki Rais Truong Tang San
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa akiagana na Rais Truong Tang San mara baada ya kuwasili hotelini kwake.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda akimweleza jambo Balozi Mbelwa wakati wa mapokezi ya Rais Truong wa Vietnam.