Tuesday, March 22, 2016

JK aendelea kusuluhisha Mgogoro wa Libya.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika wa Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya amewasili jijini Tunis nchini Tunisia  kushiriki Mkutano wa nane wa nchi Jirani ya Libya. Mkutano huo ulioitishwa na Serikali ya Tunisia ni muendelezo wa jitihada za nchi jirani kusaidia kuleta hali ya amani na usalama nchini Libya. Rais Mstaafu amewasili Tunis akitokea Salalah nchini Oman aliposhiriki Mkutano wa Kamati ya Bunge la Kuandika Katiba ya Libya.
Akiwa jijini Tunis, Rais Mstaafu Kikwete amefanya mazungumzo na Waziri wa Masuala ya Maghreb, Arab na Afrika wa Algeria Mheshimiwa Abdelkader Messaleh aliyemtembelea hotelini kwake. Katika mazungumzo yao, Waziri Messaleh alimpongeza  Rais Mstaafu Kikwete kwa kuteuliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kusuluhisha mgogoro wa Libya ambapo alimuelezea hali ya usalama na kisisa ya  Libya na mtizamo wa nchi yake juu ya namna bora ya utatuzi wa mgogoro huo.Mheshimiwa Abdelkader Messaleh Alimhakikishia Rais Mstaafu ushirikiano wa Serikali ya Algeria katika jukumu lake alilokabidhiwa na Umoja wa Afrika.
Kwa upande wake, Rais Mstaafu Kikwete alimshukuru Waziri Abdelkader Messaleh kwa maelezo aliyompatia na ushirikiano aliomuahidi na kumuelezea matumaini yake ya kupatikana kwa suluhu ya mgogoro huo madhali nchi jirani na Libya na Umoja wa Afrika zitashirikiana na wadau wote kuhakikisha mgogoro huo unatatulika ambapo Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alisisitiza kuwa hatimaye suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya uko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe.


 Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje ya Oman Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah mjini Salalah, Oman kuzungumzia mgogoro wa Libya. Katika mkutano wao wamebadilishana mawazo juu ya suluhisho la kudumu la hali ya siasa, usalama na amani nchini Libya.


 Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu. Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao. Amewakumbusha dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kupawapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote. 


 Picha ya pamoja.

===================== 
Katika ziara yake nchini Tunisia, mbali na kuhudhuria Mkutano wa 8 wa nchi Jirani na Libya, Rais Mstaafu Kikwete anatarajiwa pia kukutana na Waziri Mkuu Mteule na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Libya (Presidency Council) Mheshimiwa Fayez Al-Sarraj,  wadau wengine wa Libya  pamoja na kutembelea Ofisi ya Ujumbe wa Umoja wa Afrika kwa Libya iliyoko jijini Tunis. Rais Mstaafu Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea nchini tarehe 25 Machi, 2016. 

Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye ndiye Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika utatuzi wa mgogoro wa Libya ameshiriki Mkutano wa Kamati ya Uandishi ya Baraza Maalum la Uandishi wa Katiba ya Libya (Constitution Drafting Assembly) unaoendelea mjini Salalah, Oman. Mkutano huo uliohudhuriwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Mheshimiwa Yusuf bin Alawi bin Abdallah na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler.

Katika Mkutano huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuona kuwa mgogoro wa Libya unapatiwa suluhisho la kudumu na Amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa jawabu la matatizo ya Libya ya hali ya usalama na changamoto zake liko mikononi mwao ikiwa ni pamoja na dhamana kubwa iliyo juu yao na matarajio ya wananchi wa Libya kwa wajumbe hao kuwapatia Katiba ambayo itatoa majawabu kwa changamoto za Libya na kulinda haki na usawa kwa makundi yote. 

Rais Mstaafu Kikwete pia amepongeza jitihada za Umoja wa Mataifa chini ya Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa Bw. Martin Kobler za kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro wa Libya kupitia Mkataba wa Amani wa Libya (Libya Political Agreement) uliotiwa saini tarehe 17 Desemba, 2015 huko Shkirat, Morocco na kuwahimiza wadau wa pande zote za siasa nchini Libya kutekeleza makubaliano hayo ikiwemo kuundwa kwa serikali na kusimikwa kwa serikali hiyo yalipo makao makuu ya nchi hiyo mjini Tripoli mapema iwezekanavyo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa Afrika amewahakikishia wajumbe hao utayari wa Umoja wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Falme za Kiarabu (Arab League)  na wadau wengine wote kusaidia jitihada za wananchi wa Libya kurejesha hali ya usalama, amani na utulivu nchini Libya.
                                     MWISHO.

Friday, March 18, 2016

Mkurugenzi wa Idara ya Asia azungumza na Balozi wa India nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akizungumza na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya alipofika Wizarani kwa ajili ya kueleza dhamira ya India ya kuendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu na ile ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam na Zanzibar.
Balozi Arya akichangia jambo wakati wa mazubngumzo yake na Balozi Kairuki
Balozi Kairuki akiagana na Balozi Arya mara baada ya mazungumzo yao.

Thursday, March 17, 2016

Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wafanya Ziara Kilosa

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. John Henjewele akitoa taarifa ya Wilaya na historia ya migogoro kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini ambao walitembelea jamii ya wafugaji na wakulima Wilayani humo kwa lengo la kuwashawishi kuwa wavumilivu kwa kila mmoja katika kutatua migogoro ya Ardhi na kuimaliza kabisa, sambamba na kutoa vifaa kwa watoto wa shule katika shule ya Sekondari Parakuyo na shule za msingi Mabwerebwere, Tindiga na Ulaya. Kauli mbiu ya Ziara hiyo ilikuwa "Tusipigane Tuzungumze Wakulima na Wafugaji Tushirikiane kudumisha Amani

Sehemu ya Maafisa walioshiriki Ziara wakifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Mhe. Henjewele. 

Maafisa Habari kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa wakikabidhi fulana kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Parakuyo Wilayani Kilosa, kutoka kushoto Bi. Rose Mbilinyi, kutoka kulia Bw. Ally Kondo na Bw. Teodos Komba. Vilevile maafisa hao walikabidhi msaada wa Vitabu, Zana za Kufundishia na Madawati.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Tindiga Wilayani Kilosa wakiwa wamekaa katika Madawati waliyokabidhiwa na Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini, ambapo shule hiyo ilipokea msaada wa Madawati 50.


========================================================================


Ziara hiyo ni miongoni mwa shughuli zilizofanyika wakati Kikao Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kikiendelea, Kikao hicho kilifunguliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye tarehe 14 Machi na kinatarajiwa kumalizika tarehe 18 Machi,2016.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akifungua Kikao kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini nchini hawapo pichani kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel ambapo alieleza lengo la kikao hicho ni kupeana na kushirikishana uzoefu ili kuboresha utendaji na kuleta ufanisi kwa maafisa hao, Pia aliwasisitiza ni vema kila Afisa akaonesha uwezo binafsi ili kuweza kukubalika na kuthaminiwa kwa nafasi yake katika Tasisi anayoiwakilisha.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bi. Mindi Kasiga kati akiwa na baadhi ya Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini wakifuatilia kikao.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini Dar es salaam Bw. Luke Chilambo ambaye alikuwa miongoni mwa wawezeshaji katika kikao kazi hicho akitoa mada kuhusiana na Diplomasia na Itifaki.
Bi Joy Nyabongo ambaye ni muwezeshaji na mtoa mada ya Huduma kwa Mteja akitoa Zawadi kwa mshindi wa pili Bi. Mindi Kasiga baada ya kushinda jaribio la uelewa wa mada hiyo.
Mhe. Waziri Nape na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa Habari na Mawasiliano kutoka Serikali kuu.


Wednesday, March 16, 2016

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje amuaga Mwendesha Mashitaka wa ICTR-MICT

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Mhe. Dkt.Suzan Kolimba (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mwendesha Mashtaka wa iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya  Rwanda (ICTR) na ile iliyoririthi shughuli za Mahakama hiyo MICT, Bw. Hassan Bubacar Jallow alipofika Wizarani kwa ajili ya kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Mhe. Dkt. Kolimba akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Jallow. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Baraka Luvanda (wa pili kulia), Dkt. Cheichk Bangoura (kushoto) ambaye ni Mwanasheria wa MICT na Bw. Elisha Suku (kulia), Afisa Mambo ya Nje.

INTERNATIONAL ESSAY CONTEST ANNOUNCEMENT


2016 INTERNATIONAL ESSAY CONTEST FOR YOUNG PEOPLE

The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation has received an announcement from The Goi Peace Foundation regarding the 2016 International Essay Contest for Young People

The 17th edition of Annual International Essay contest for young people is an activity of the UNESCO Global Action Programme on Education for Sustainable Development. This year’s theme is entitled, Education to Builda Better Future for All”.

The 2016 Essay Contest guidelines can be found at the following website address:http://www.goipeace.or.jp/english/activities/programs/1601.html.

Young people are cordially invited to participate in this renown annual Essay Contest and to submit their entries no later than 15th June, 2016.


Issued by: The Ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation, Dar es Salaam.
16th March, 2016

Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje yakutana na Uongozi wa Wizara

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Balozi Adad Rajab akimkaribisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (hayupo pichani) kuwasilisha taarifa ya Wizara kuhusu Sera, Muundo na Majukumu kwa Wajumbe wa Kamati hiyo. Kikao hicho ambacho kiliwahusisha pia Wakurugenzi kutoka Wizarani kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Machi, 2016.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akiwasilisha mada kuhusu Sera, Muundo na Majukumu ya Wizara kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (hawapo pichani)
Sehemu ya Wabunge wakimsikiliza Naibu Waziri alipowasilisha taarifa ya Wizara.
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam, Balozi Mohammed Maundi akiwasilisha taarifa ya utendaji ya Chuo hicho ambacho ni moja ya Taasisi za  Wizara
Wabunge wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa za Wizara
Katibu Mtendaji wa Mpango wa Nchi za Afrika kujitathmini kiutawala Bora (APRM) kwa upande wa Tanzania, Bibi Rehema Twalib akiwasilisha taarifa kuhusu taasisi hiyo ambayo ipo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakiwa kikaoni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Bw. Elishilia Kaaya naye akiwasilisha taarifa ya kituo hicho kwa Kamati ya Bunge.
Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa
Wakurugenzi
Baadhi ya Wakurugenzi kutoka Wizarani wakati wa kikao
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja wakati wa kikao na Kamati ya Bunge
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati wakifuatilia.
Sehemu nyingine ya Wakurugenzi wa Wizara
Mkutano ukiendelea
Mhe. Dkt. Kolimba akizungumza na Waandishi wa Habari


Tuesday, March 15, 2016

Mabalozi wa Afrika wampa pole Mhe. Dkt. Kikwete kwa kifo cha kaka yake

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimweleza jambo Kaimu Kiongozi wa Mabalozi kutoka nchi za Afrika wanaowakilisha nchi zao hapa nchini ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe, Mhe. Edzai Chimonyo walipofika nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumpa pole kufuatia kifo cha Kaka yake Marehemu Suleiman Kikwete kilichotokea hivi karibuni.
Sehemu ya Mablozi wakifuatilia mazungumzo na Mhe. Dkt. Kikwete (hayupo pichani). Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Samwel Shelukindo ambaye alifuatana na Mabalozi hao.
Sehemu nyingine ya Mabalozi wakifuatilia mazungumzo na Mhe. Dkt. Kikwete hayupo pichani.
Mhe. Dkt. Kikwete akiendelea na mazungumzo
Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Dkt. Kikwete
Mabalozi wakifurahia jambo
Mhe. Dkt. Kikwete akiwaeleza jambo Mabalozi mara baada ya Mabalozi hao kutoa salamu zao za pole
Mhe. Dkt. Kikwete akiagana na Balozi Shelukindo
Mhe. Dkt. Kikwete katika picha ya pamoja na Mabalozi.

Ujumbe wa JWTZ watembelea Ubalozi wa Tanzania Washington, DC

Pichani kutoka kushoto: Col. Adolph Mutta (DA), Brig. Gen. (Dkt) Denis R. Janga, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Brig. Gen. (Dkt) Robinson M. Mwanjela, Lt. Col. (Dkt) Charles E. Mwanziva na Lt. Col. Lawerence T. Banda


Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Washington, DC alikutana na Ujumbe wa JWTZ ulioongozwa na Mkuu wa Tiba Jeshini, Brigedia Jenerali (Dkt.) Denis Raphael Janga, aliyekuwa amefuatana na Mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Tiba - Lugalo, Brigedia Jenerali (Dkt) Robinson Mboni Mwanjela. 

Wengine ni Mkurugenzi wa Kinga Jeshini, Luteni Kanali Charles Emilio Mwanziva pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wauguzi, Luteni Kanali Lawrence Tia Banda. Ujumbe huo ulikwa na ziara ya Kikazi ya wiki moja hapa Marekani, katika kuendeleza mahusiano baina na JWTZ na majeshi ya Marekani. 

Friday, March 11, 2016

Waziri Mahiga afanya mazungumzo na Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Norway

 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Augustine Mahiga akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Bi. Tone Skogen kushoto aliyemtembelea leo katika ofisi za Wizara, ambapo katika mazungumzo yao walijadili mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na Norway ambapo Norway imekuwa ikisaidia katika sekta ya Nishati na  Elimu hasa katika taaluma ya Uhandisi, pia ni mdau katika kupigania haki za binadamu pamoja na masuala ya jinsia.
 Maafisa waliofuatana na Mhe. Tone Skogen wakifuatilia mazungumzo.
 Sehemu nyingine ya maafisa hao wakifuatilia mazungumzo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Balozi Joseph Sokoine kushoto pamoja na afisa mambo ya nje wakifuatilia Mazungumzo.