Na Mwandishi Maalum, New York
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban
Ki Moon, ameitaka Tanzania kuendelea na kazi nzuri ya usuluhishi wa migogoro
katika baadhi ya nchi za Maziwa Makuu.Ban Ki Moon ametoa wito huo jana (
jumatano) wakati alipokutana Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Dk. Augustine Mahiga, ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania katika mkutano wa 71 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
unaoendelea hapa Jijini New York, Marekani.Katika mazungumzo hayo Mkuu huyo wa
Umoja wa Mataifa amesema, Tanzania ni kutovu cha Amani, usalama na demokrasia,
na kutokana na sifa hizo Tanzania, inapashwa kuendelea na juhudi zake za
kuzisaidia nchi zenye migogoro.
Akazitaja nchi hizo kuwa ni Jamhuri
ya Kidemokrasi ya Kongo, Burundi na Sudani ya Kusini ambayo ameitaja kuwa ipo
katika kipindi kigumu sana. “ Ninawashukuru sana viongozi wa Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri ya
utafutaji wa Amani katika nchi zenye matatizo, Sudani ya Kusini ni nchi ambayo
inatupa mashaka makubwa. Rais asaidie katika kurejesha hali ya utulivu.Tanzania
ni nchi kubwa kwa hiyo bado ninaendelea kuitumainia.” akasisitiza Ban Ki
Moon.Vile vile Katibu Mkuu Ban Ki Moon ametoa pia shukrani wa ushiriki wa
Tanzania katika operesheni za ulinzi wa Amani na kazi na weledi mkubwa
unaoonyeshwa na wanajeshi wa Tanzania.
Akatumia fursa hii kuishukuru
Tanzania na viongozi wake kwa mchango wao mkubwa uliofanikisha yeye kuchaguliwa
kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Na akatoa pole zake kwa serikali na kwa
watanzania baada ya kupata taarifa kuhusu tetemeko la ardhi lililosababisha
vifo na uharibifu wa mali.
“Naishukuru sana Tanzania, namshukuru
Rais Mstaafu Jakaya Kiwete na wewe ( Waziri) na viongozi wengine, mlichangia
sana kwangu mimi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Ninawashukuru sana sana.
” .Katibu Mkuu Ban Ki Moon anamaliza kipindi chake cha uongozi cha miaka kumi
mwishoni wa Mwaka huu.Na tayari mchakato wa upigaji kura wakumtafuta mrithi
wake unaendelea katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Kwa upande wake,
akiwasilisha salamau za Rais John Pombe Magufuli, Waziri Mahiga amesema. “
Ninawasilisha salamu za Mhe. Rais, alipenda sana kuhudhuria mkutano huu wa 71
wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwa bahati mbaya ilimbidi kuahirisha safari
yake kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibu nchini kwetu ”.
Aidha Waziri Mahinga ametumia pia
fursa hiyo kumshukuru na kumpongeza Katibu Mkuu kwa utekelezaji wa kutukuka wa
majukumu yake katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake.
“Kwa niaba ya serikali ya Tanzania
nikupongeza kwa utekeleaji wa majukumu yake. Ulionyesha ushirikiano wa karibu
na Tanzania, ushirikiano uliokuwezesha kumteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Naibu
Katibu Mkuu na msaidizi wako wa karibu. Lakini pia uliniteua mimi kuwa Mjumbe
wako Maalum huko Somalia . Tanzania inashukuru kwa haya na mengine” akasema
Mahiga.
Aidha amemwelezea Katibu Mkuu kama
kiongozi ambaye aliifanya Afrika kuwa kipaumbele chake, lakini pia aliibeba
sana ajenda ya wanawake jambo ambalo amesema limemjenga sifa kubwa.Akizungumzia
kuhusu Tanzania kuendelea na juhudi za usuluhishi wa migogoro. Waziri
amemhakikisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba, Tanzania na viongozi wake
wataendelea na kujukumu hilo.
“Ni kuhakikishie kwamba Serikali
yangu itendelea na jukumu hili la usuluhisi. Na kwa upande wa Burundi Tanzania,
inaushukuru Umoja wa Mataifa, kwa kutambua na kuamini kwamba Jumuiya ya Afrika
Mashariki inaweza kuushughulikia mgogoro huu. Tanzania ambayo imekabidhiwa
jukumu la uwezeshaji wa mazungumzo ya Amani inataka kufanya kazi kwa karibu na
Umoja wa Mataifa hivyo misaada ya hali na mali kutoka Idara za Umoja wa Matifa
ni jambo muhimu”.Amesisitiza Waziri Mahiga.