Mkutano ukiendelea
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Mkutano wa Nne wa Mawaziri
wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Korea ujulikanao kama Korea-Africa
Ministerial Forum unaotarajiwa kufanyika kwa mara ya kwanza Barani Afrika, Addis
Ababa, Ethiopia tarehe 06 na 07 Desemba, 2016. Mikutano mitatu ya kwanza
ilifanyika Seoul, Korea mwaka 2006, 2009 na 2012.
Mkutano huu ambao
umeandaliwa na Serikali ya Korea kwa kushirikiana na Umoja wa Afrika una lenga
kukuza ushirikiano pamoja na kuandaa maeneo mapya ya ushirikiano baina ya Korea
na mataifa ya Afrika katika miaka mitatu ijayo.
Tanzania ni moja ya
nchi nne (4) za Afrika ambazo Korea imezichagua kuanzisha mahusiano ya
kimkakati “strategic partnership” yatakayozifanya nchi hizo kupewa kipaumbele
katika kupokea misaada na mikopo nafuu kutoka Korea katika kipindi cha miaka
mitano ijayo kati ya 2016 hadi 2020.
Katika kipindi hicho,
Tanzania itapokea kiasi cha Dola za Kimarekani milioni 300 ikiwa ni asilimia
17.1 ya msaada utakaotolewa Barani Afrika, hivyo kuifanya Tanzania kuwa nchi
inayoongoza Barani Afrika kupokea misaada kutoka Jamhuri ya Korea. Nchi
nyingine ni Msumbji, Ethiopia na Angola.
Msaada huo unategemea kufadhili miradi katika sekta za
umeme, viwanda na TEHAMA.
Sanjari na Mkutano
huo, ujumbe wa Tanzania utafanya mkutano wa pande mbili na ujumbe wa Serikali ya
Korea kuzungumzia masuala ya ushirikiano baina ya nchi zetu mbili. Tanzania
itatumia fursa hiyo kuiomba Korea kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mipya
ikiwemo mradi wa Daraja la Selander ambao unatarajiwa kuanza mwaka 2017 na
kukamilika 2020.
Aidha, ushiriki wa
Tanzania kwenye mkutano wa Afrika na Korea ni fursa muhimu ya kukuza mahusiano
baina ya nchi zetu mbili hususan katika Nyanja ya uchumi. Serikali ya Korea
ilitoa ahadi ya kuongeza uwekezaji Barani Afrika hususan katika sekta za
nishati, miundombinu na viwanda.
Miradi ambayo Tanzania imefaidika tokea
kuanzishwa mikutano hii mwaka 2006 ni pamoja na mradi wa kuendeleza kilimo cha
Mwani Zanzibar wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 3.6 na Awamu ya Pili
ya Mradi wa Huduma ya Uchunguzi wa Afya ya Uzazi Jijini Dar es Salaam wenye
thamani ya Dola za Kimarekani milioni nne (4).
Miradi mingine ambayo
Jamhuri ya Korea imeshirikiana na inaazimia kushirikiana na Tanzania ni:-
·
Ujenzi wa Mradi wa Daraja la Kikwete
kwenye Mto Malagarasi Mkoani Kigoma ambao umekamilika; Ujenzi wa Hospitali ya Kimataifa
iliyopo eneo la Mloganzila; Dar es Salaam
na Hospitali ya Mama na Mtoto iliyopo
Chanika, Dar es Salaam.
·
Kadhalika, hivi karibuniTanzania
imesaini
o
Makubaliano ya kupanua miundombinu ya Majitaka
jijini Dar es Salaam; na
o
Makubaliano ya kutekeleza miradi
utakaofadhiliwa kwa pamoja na benki ya Maendeleo ya Afrika na Serikali ya
Jamhuri ya Korea.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki
Dar es Salaam, 01 Desemba,
2016.
|