Tuesday, November 29, 2016

Rais Lungu atembelea Bandari ya Dar es Salaam na Kampuni ya Zamcargo

Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwe Lungu akiangalia mfumo wa kielektroniki  (haupo pichani) wa kuharakisha ukaguzi wa mizigo katika bandari ya Dare es Salaam alipotembelea bandari hiyo. Rais Lungu aliwasili bandirini hapo mapema leo asubuhi akisindikizwa na Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga

Meza kuu ikifuatilia shughuli zilizokuwa zikiendelea wakati wa mapokezi mara baada ya kuwasili eneo la bandari ya Dar es Salaam


Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwe Lungu akizungumza na wafanyakazi na wwadau mbalimbali waliojitokeza kumpokea alipowasili eneo la bandari ya Dar es Salaam

Rais wa Zambia Mhe. Edgar Chagwe Lungu akionesha kwa hadhira zawadi ya mchoro wa eneo la bandari aliyokabidhiwa na Mkurugendi Mtendaji wa Bandari ya Dar es Salaam 

Picha ya pamoja

Rais wa Zambia Mhe. Edgar Chagwe Lungu akiongea na wafanyakazi wa kampuni ya Zamcargo alipoitembelea kampuni hiyo mapema leo asubuhi

Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa na Rais wa Zambia Mhe. Edgar Chagwe Lungu  wakiangalia namna ya utendaji wa mashine za kushusha na kupakia mizigo zinazo milikiwa na Kampuni hiyo (Zamcargo). Zambia Cargo and Logistics (Zamcargo) nikampuni ya serikali ya Zambia iliyopo nchini inayojihusisha na  usafirishaji, upakiaji na ushushaji mizigo katika bandari ya Dar es Salaam.
Moja ya mashine za kunyanyu mzigo ikiwa imebeba madini ya shaba


Waziri wa  Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza walipotembelea kampuni ya Zamcargo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.