Tuesday, November 29, 2016

Rais Magufuli amuaga Rais Lungu wa Zambia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amembatana na mgeni wake Rais wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu wakiangalia ngoma ya asili wakati akimuaga baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini, katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.  Rais Lungu ameondoka nchini leo mchana kurejea nchini kwake.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Rais wa Zambia Mhe. Edward Lungu wakipeana mikono kwenye hafla ya kumuaga Rais huyo
Waheshimiwa Marais (waliosimama jukwaani) wakitoa heshima wakati wimbo wa Taifa ukipigwa katika hafla ya kumuaga Rais wa Zambia Mhe. Lungu iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima na Rais wa Zambia Mhe. Edward Lungu wakipeana mikono kwenye hafla ya kumuaga Rais huyo

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo kwa Rais wa Zambia Mhe. Edgar Lungu wakati akielekea kupanda ndege muda mfupi kabla ya kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,Jijini  Dar es Salaam.

Mhe. Rais Edgar Lungu akipungia mkono wananchi waliojitokeza uwanja wa Ndege kwenye hafla ya kumuaga

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Mhe. Harry Kalaba wakiwa tayari kusoma tamko la pamoja la Waheshimiwa Marais kwa wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya ziara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisoma tamko la pamoja

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia Mhe. Harry Kalaba wakipeana mikono baada ya kuosoma tamko la pamoja (joint communique)


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.