Wednesday, November 30, 2016

Waziri Mahiga akutana na Balozi wa Jamhuri ya Korea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Song Geum-Young wakati wa mazungumzo waliyoyafanya Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika masuala mbalimbali ya kudumisha uhusiano kati ya nchi hizi mbili (Tanzania na Korea) sambamba na kuzungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo nchini inayofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Korea, ikiwemo  mradi wa Hospotali ya Muhimbili, Mloganzila na Mradi wa ujenzi wa Daraja jipya la Sarenda unatarijiwa kuanza hivi karibuni.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimsikiliza Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Song Geum-Young wakati wa mazungumzo 

Katika kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara Bi. Mindi Kasiga,wengine ni maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.