Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC Troika), Balozi Dkt. Aziz Mlima akifungua rasmi Kikao cha Makatibu Wakuu na Maafisa Waandamizi kutoka Asasi hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupitia agenda mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kwenye Kikao cha Mawaziri kitakachofanyika tarehe 03 Novemba, 2016 katika Ukumbi huo. Asasi ya SADC inaundwa na nchi tatu ambazo ni Tanzania (Mwenyekiti), Angola (Makamu Mwenyekiti) na Msumbiji (Mwenyekiti aliyemaliza). Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, Mhe. Dkt. Stergomena Tax. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.