Wednesday, June 14, 2017
Friday, June 9, 2017
Wizara ya Mambo ya Nje yafanya uzinduzi wa shindano la kubuni nembo mpya ya EAC
Sehemu nyingine ya Wanafunzi wakifuatilia maelekezo. |
Picha ya pamoja uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje, Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
Picha ya pamoja Viongozi na wanafunzi. |
Siku ya Kongamano la Biashara ya Kilimo na Uwekezaji kati ya Tanzania na Uholanzi yafana
Mhe. Mathew Mtigumwe, Katibu Mkuu wa Wizara Kilimo, Mifugo na Uvuvi akisoma hotuba. |
Mhe. Irene Kasyanju, Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi akisoma hotuba ya ufunguzi. |
Mhe. Marjolijn Sonnema, Katibu Mkuu na Kaimu Naibu Waziri wa Kilimo wa Uholanzi akisoma hotuba |
Picha ya Pamoja ya Waheshimiwa Mabalozi wa Tanzania na Uhoalnzi na Makatibu Wakuu wa Kilimo na Uvuvi na Mkurugenzi wa TAHA. |
Uwekaji saini wa makubaliano (letter of intent) ya kuanzishwa kwa kituo cha kuendeleza zao la viazi Tanzania |
Thursday, June 8, 2017
Vijana wahamisishwa kushiriki mashindano ya kubuni nembo ya EAC
Mazungumzo yakiendelea. |
Balozi Mwinyi akipokea kitabu chenye mwongozo wa namna ya kushiriki mashindano hayo. |
Picha ya pamoja. |
Wednesday, June 7, 2017
Tanzania yashiriki Mkutano wa kujadili matumizi ya Bahari na rasilimali zake
Monday, June 5, 2017
Wizara ya Mambo ya Nje yafanya usafi kwenye ufukwe wa Feri
Mkurugenzi msaidizi Idara ya Utawala na Rasilimali watu Bw. Hamid Mbegu (kushoto) naye akifanya usafi |
Sehemu nyingine ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijumuika kwa pamoja katika kufanya usafi kwenye ufukwe wa bahari eneo la Feri. |
wakisomba taka |
Sehemu nyingine ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiendelea kufanya usafi |
Usafi ukiendelea |
Kaimu Mkurugenzi wa idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Jestas Nyamanga akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza zoezi la kufanya usafi kwenye ufukwe eneo la ferri |
HOTUBA
YA BALOZI DKT. AZIZ P. MLIMA, KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA
USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI KATIKA SHUGHULI YA KUFANYA USAFI KWENYE UFUKWE
WA BAHARI YA HINDI, ENEO LA KIVUKONI (FERRY), DAR ES SALAAM
TAREHE
05 JUNI 2017
Waheshimiwa Mabalozi, Wakurugenzi na Makaimu
Wakurugenzi kutoka Wizarani,
Wawakilishi wa Mashirika
na Taasisi za Umoja wa Mataifa kwenye tukio hili;
Uongozi wa Kata ya
Kivukoni ukiongozwa na Mhe. Henry Massaba, Diwani wa Kata ya Kivukoni;
Uongozi wa Mtaa wa Kivukoni ukiongozwa na Ndugu Gasper Makame, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivukoni;
Wafanyakazi wa Wizara na Taasisi zilizo chini
ya Wizara;
Wananchi wote mlioshiriki;
Waandishi wa Habari;
Mabibi na Mabwana.
Awali
ya yote, napenda kuwasilisha salamu kutoka kwa Mhe. Waziri, Dkt. Augustine P.
Mahiga (Mb.), pamoja na Mhe. Naibu Waziri, Dkt. Susan A. Kolimba (Mb.). Wanawasalimu
sana na walitamani wajumuike nasi kwenye zoezi hili, ila kutokana na kubanwa na
majukumu mengine ya kitaifa wameshindwa. Lakini wamefurahishwa na hiki
tulichokifanya na wanatupongeza sana.
Wizara inawashukuru sana wote mliojumuika nasi kwenye tukio hili muhimu la kusafisha mazingira ya ufukwe huu tunapoadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Maadhimisho
haya kidunia yanafanyika nchini Canada, na kwa hapa Tanzania, yanafanyika
kitaifa huko Butiama, Mkoani Mara, chini ya
kaulimbiu: “Hifadhi ya Mazingira:
Muhimili kwa Tanzania ya Viwanda”.
Kaulimbiu
hii inatukumbusha kuwa tunapoelekea kwenye Tanzania ya Viwanda na Uchumi wa Kati,
hatuna budi kutunza mazingira, kwani rasilimali tunazozihitaji kutimiza azma yetu
hii adhimu zinapatikana kwenye mazingira na mazingira ndiyo maisha yetu. Hivyo
utajiri wetu wa kwanza ni mazingira.
Mabibi na Mabwana,
Tumechagua
kufanya zoezi hili la usafi kwenye ufukwe wa bahari kwa sababu tunapozungumzia
utunzaji wa mazingira, suala la utunzaji wa bahari linasahaulika. Hivyo, sisi
tunaikumbusha jamii kuwa bahari nayo ni sehemu ya mazingira, ni urithi wetu, ni
lazima tuitunze.
Kwa bahati, wakati sisi tunafanya zoezi hili, leo hii pia kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, huko New York, dunia inakutana kujadili namna ya kuhakikisha uhifadhi wa bahari na matumizi endelevu ya rasilimali zake, ukiwa ni Mkutano wa kwanza wa Umoja wa Mataifa kuhusu suala hili.
Hivyo,
ndugu wananchi wenzangu, naomba tuone umuhimu wa kutunza bahari, tunaitegemea sana
kwenye uchumi wetu na maisha yetu ya kila siku, tuache kuichafua kwani
ikipoteza uhai ni hasara kwetu sote.
Mabibi na Mabwana,
Mtakubaliana
nami kuwa, bila kufanya zoezi hili kwa ushirikiano, tusingefanya chochote cha
msingi hapa. Basi, na hili liwe funzo wakati huu tunapotekeleza Malengo ya
Maendeleo Endelevu (SDGs) na Makubaliano ya Paris ambayo yote yanasisisiza
uhifadhi wa mazingira. Bila ushirikiano, itakuwa vigumu kutimiza azma hiyo ya Makuibaliano
ya Paris na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Dunia ni yetu sote,
inatutunza sote, inatukirimia sote sawa sawa, basi sote tuna jukumu la kuitunza,
tena kwa ushirikiano.
Mabibi na Mabwana, Wananchi Wote Mliopo Hapa,
Kabla
sijamaliza kuzungumza, napenda kutumia nafasi hii kuishukuru Ofisi ya Umoja wa
Mataifa hapa nchini; Uongozi wa Manispaa ya Ilala na Kata ya Kivukoni kwa
misaada yao ya hali na mali katika kufanikisha zoezi hili. Tunawashukuru sana.
Asanteni sana kwa kunisikiliza!
Serikali Mpya ya Lesotho yashauriwa kutekeleza Mageuzi - SADC
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Mkuu wa Timu ya waangalizi ya SADC ya uchaguzi wa Lesotho akiwasilisha taarifa ya awali kuhusu uchaguzi huo |
Waziri Mahiga akiendelea kuwasilisha taarifa ya awali ya uchaguzi wa Lesotho jijini Maseru |
Waziri Mahiga bado anasoma taarifa ya awali ya uchaguzi wa Lesotho kwa wajumbe. |
Subscribe to:
Posts (Atom)