Friday, September 8, 2017

Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa China nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Wizarani Balozi wa China anayemaliza muda wake wa kazi nchini, Mhe. LU Youqing ambaye alifika Wizarani kwa lengo la kuaga. Hafla fupi ya kumuaga Balozi LU Youqing ilifanyika Wizarani tarehe 07 Septemba, 2017.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha Waziri Mahiga na Balozi LU kuzungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Balozi LU iliyofanyika Wizarani.
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi LU wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani. Katika mazungumzo yao Mhe. Mahiga alimpongeza Balozi LU kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini. Mhe. Mahiga alimwelezea Balozi LU kama mtu wa tofauti katika utendaji kazi na utekelezaji wake wa majukumu kwa kuwa alijitolea kikamilifu kuhakikisha ushirikiano kati ya Tanzania na China unaimarika na kukua zaidi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Balozi LU (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi LU. Katikati ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Magabilo Murobi.
Sehemu ya ujumbe kutoka Ubalozi wa China ambao ulifuatana na Balozi LU.
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi Balozi LU zawadi Maalum ya Nembo ya Taifa inayowakilisha utendaji uliotukuka wa Balozi LU
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi Balozi LU zawadi nyingine ya Kinyago cha UMOJA kuonesha umoja na mshikamano uliopo kati ya Tanzania na China
Mhe. Balozi LU akipokea zawadi nyingine ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro pamoja na Tembo kama kumbukumbu kwa Balozi LU ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini na pia mchango wa China katika mapambano dhidi ya ujangili wa pembe za ndovu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Rogers Sianga nae akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi LU.
Balozi LU akifurahia zawadi ya Ngozi ya Pundamilia kutoka kwa Kamishna Sianga ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa China katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya
Picha ya pamoja kuhitimisha hafla ya kumuaga Balozi LU

Wednesday, September 6, 2017

Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda akutana na Balozi wa India nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Innocent Shiyo akizungumza na Balozi wa India hapa nchini, Mhe.Sandeep Arya alipotembelea Wizarani hivi karibuni. Katika mazungumzo yao Balozi Shiyo alimweleza Balozi Arya masuala mbalimbali kuhusu Tanzania na ushiriki wake katika masuala ya kikanda ikiwemo amani, siasa na usalama hususan katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
Mazungumzo yakiendelea kati ya Balozi Shiyo na Balozi Arya. Wengine katika picha ni Afisa kutoka Ubalozi wa India (Kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Isaac Isanzu (kulia)
Balozi Shiyo na Balozi Arya katika picha ya pamoja
Balozi Shiyo akiagana na Balozi Arya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Tuesday, September 5, 2017

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wahitimu mafunzo ya JKT

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa wamejipanga kusubiri sherehe za mahafali ya kumaliza mafunzo ya JKT kuanza. Mafunzo hayo yalifanyika Kambi ya JKT ya Oljoro mkoani Arusha kwa kipindi cha wiki sita kuanzia tarehe 24 Julai hadi 04 Septemba 2017.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wa mahafali hayo akiwa katika jukwaa kwa ajili ya kupokea heshima kutoka kikosi cha Vijana cha Operesheni Viwanda (hakipo pichani) ambacho kimejumuisha watumishi 30 wa Wizara ya Mambo ya Nje.

Mgeni Rasmi, Balozi Mlima akikagua gwaride maalum lililoandaliwa kwa heshima yake na kikosi kilichohitimu mafunzo ya JKT ambacho kilijumuisha watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje
 Mgeni Rasmi, Balozi Aziz Mlima wakiwa wamesimama pamoja na Mwakilishi wa Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (kulia) na Kamanda wa Kambi ya Oljoro kwa ajili kuangalia vikosi vikipita mbele yao katika mwendo wa pole na kasi
Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa pole

Kikosi kikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa kasi

Mgeni Rasmi akikabidhi zawadi kwa waliofanya vizuri zaidi. 



Bi. Khadija Othman akipokea zawadi yake

Bw. Graison Ishengoma akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni Rasmi

Bw. Edward Komba akipokea zawadi yake.

Wahitimu wa mafunzo ya JKT kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakila kiapo cha utii

Risala kwa Mgeni Rasmi. katika risala hiyo waliahidi kuyafanyia kazi mafunzo yote waliyoyapata watakaporejea katika kituo chao cha kazi. Walijifunza uzalendo, utii, ustahamilivu, ukakamavu na mengine mengi.

Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao nao washapitia mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wakiwashuhudia wenzao wakihitimu mafunzo ya JKT katika awamu ya pili.

Burdani ilikuwepo siku ya mahafali. Hapo bendi ya Jeshi ikitumbwiza.

Onesho la Makamandoo hapo mmoja wao amebeba ndoo za maji kwa kutumia meno yake.

Mkuu wa Kambi ya Oljoro akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mwakilishi wa Mkuu wa JKT ili amkaribishe Mgeni Rasmi

Mwakilishi wa Mkuu wa JKT akimkaribisha Mgeni Rasmi atoe hotuba ya kufunga mafunzo hayo. Kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi alisisitiza umuhimu wa taasisi nyingine za umma kuiga Wizara ya Mambo ya Nje kwa kupeleka watumishi wao ili kupata mafunzo ya JKT ambayo ni muhimu kwa kujenga uzalendo, nidhamu na umoja.

Mgeni Rasmi akisoma hotuba yake. Alitoa ushuhuda kuwa watumishi walioshiriki mafunzo hayo katika awamu ya kwanza wameonesha umahiri mkubwa katika kutekeleza majukumu yao na ndio sababu amepeleka kundi lingine katika awamu ya pili. Aliahidi atawapeleka watumishi wa Wizara yake wenye sifa ikiwemo ya umri (chini ya miaka 40) hatua kwa hatua hadi watakapomalizika.

Wahitimu wa mafunzo ya JKT wakisikiliza hotuba ya Mgeni Rasmi
 Baadhi ya wageni waliohudhuria mahafali hayo. Hapo afande anateta na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Bw. Othman Rashid.
Mkurugenzi wa Utawala katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nigel Msangi akimpongeza Bw. Wambura kwa kuhitimu mafunzo ya JKT.
Tumemaliza salama, shukran kwa Wizara kwa kutuandalia mafunzo haya yenye tija kubwa kwetu.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala; Bi. Ngusekela Nyerere na Mwalimu wa somo la Uzalendo ambaye alikuwa Msadizi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Nyerere.

Furaha tumemaliza mafunzo, Kutoka kushoto ni Felista Rugambwa, Teodos Komba na Rose Mbilinyi.


Wanaimba nyimbo za jeshi.

Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi na wahitimu wa JKT.

Thursday, August 31, 2017

Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yapungua nchini, Dr. Zekeng

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt Suzan Kolimba (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI (UNAIDS), Bw. Dr. Leo Zekeng ofisini kwake jijini Dar Es Salaam leo. Katika mazungumzo hayo, Dkt. Zekeng alisifu jitihada zinazofanywa na Tanzania katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa ukimwi ambazo zimesaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo kwa asilimia 25 na pia idadi ya watoto wanaozaliwa na virusi vya ukimwi imepungua kwa kiasi kikubwa. Dkt. Zekeng alisema kuwa kutokana na mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Bi Michel Sidibe anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini mwezi Oktoba 2017

Dkt. Zekeng akionesha takwimu zilizopo katika ripoti ya UNAIDS zinazoonesha namna maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI yalivyopungua nchini Tanzania.

Mazungumzo yanaendelea

Mhe. Naibu Waziri akiagana na Dkt. Zekeng baada ya kukamilisha mazungumzo yao

Picha ya pamoja

Wednesday, August 30, 2017

Libya yaipatia Zanzibar Msaada wa Matrekta

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania, Bw. Saleh Kusa  Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam leo. Wawili hao walijadili namna ya kukamilisha taratibu za kukabidhi msaada wa matrekta 10 yenye thamani ya zaidi ya milioni 250 za Tanzania kutoka Libya kwa ajili ya Serikali ya Zanzibar. Matrekta hayo yashawasili jijini Dar es Salaam na wiki ijayo yanatarajiwa kukabidhiwa Serikali ya Zanzibar. Aidha, Kaimu Balozi alisema kuwa Libya imetenga Dola Bilioni 20 kupitia Mfuko wa "Libyan-Africa Investment Portfolio" kwa ajili ya nchi za Afrika. Aliahidi kuwa atahakikisha kuwa sehemu kubwa ya fedha hizo zinaletwa Tanzania.

Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Bw. Suleiman Saleh  na Afisa Dawati wa Libya, Bw. Nicolas wakifuatilia mazungumzo

Kulia ni Mkalimani wa Kaimu Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Serikali ya Zanzibar wakifuatilia mazungumzo hayo

Nazungumzo yanaendelea

Kaimu Balozi wa Libya nchini Tanzania, Bw. Saleh Kusa  akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje
Mhe. Waziri na Kaimu Balozi wakiagana huku Katibu Mkuu, Dkt. Aziz Mlima akishuhudia
Picha ya pamoja