Friday, September 8, 2017

Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa China nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Wizarani Balozi wa China anayemaliza muda wake wa kazi nchini, Mhe. LU Youqing ambaye alifika Wizarani kwa lengo la kuaga. Hafla fupi ya kumuaga Balozi LU Youqing ilifanyika Wizarani tarehe 07 Septemba, 2017.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiwakaribisha Waziri Mahiga na Balozi LU kuzungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Balozi LU iliyofanyika Wizarani.
Waziri Mahiga akizungumza na Balozi LU wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika Wizarani. Katika mazungumzo yao Mhe. Mahiga alimpongeza Balozi LU kwa utendaji wake wa kazi katika kipindi chote alichokuwa hapa nchini. Mhe. Mahiga alimwelezea Balozi LU kama mtu wa tofauti katika utendaji kazi na utekelezaji wake wa majukumu kwa kuwa alijitolea kikamilifu kuhakikisha ushirikiano kati ya Tanzania na China unaimarika na kukua zaidi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima (kushoto) akifuatilia mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Balozi LU (hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi LU. Katikati ni Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Grace Martin na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Magabilo Murobi.
Sehemu ya ujumbe kutoka Ubalozi wa China ambao ulifuatana na Balozi LU.
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi Balozi LU zawadi Maalum ya Nembo ya Taifa inayowakilisha utendaji uliotukuka wa Balozi LU
Mhe. Waziri Mahiga akimkabidhi Balozi LU zawadi nyingine ya Kinyago cha UMOJA kuonesha umoja na mshikamano uliopo kati ya Tanzania na China
Mhe. Balozi LU akipokea zawadi nyingine ya picha ya kuchora inayoonesha Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro pamoja na Tembo kama kumbukumbu kwa Balozi LU ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini na pia mchango wa China katika mapambano dhidi ya ujangili wa pembe za ndovu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Bw. Rogers Sianga nae akizungumza wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi LU.
Balozi LU akifurahia zawadi ya Ngozi ya Pundamilia kutoka kwa Kamishna Sianga ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa China katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya
Picha ya pamoja kuhitimisha hafla ya kumuaga Balozi LU

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.