Sehemu nyingine ya Wajumbe kutoka nchi Wanachama wakifuatilia Mkutano. |
Mkutano ukiendelea. |
Picha ya pamoja. |
============================================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MHE. WAZIRI MAHIGA AFUNGUA RASMI MKUTANO
WA KWANZA WA MAWAZIRI WENYE DHAMANA YA MASUALA YA MIUNDOMBINU WA NCHI WANACHAMA
WA JUMUIYA YA UTATU WA COMESA-EAC-SADC (TRIPARTITE) UNAOFANYIKA HAPA DAR ES
SALAAM LEO TAREHE 26 OKTOBA 2017
Mkutano wa
Kwanza wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC
umefanyika hapa Dar es Salaam, Serena Hoteli leo tarehe 26 Oktoba 2017. Mkutano
huo unahusisha jumla ya nchi 26 Wanachama wa Umoja huo. Mkutano huu unafanyika
hapa Tanzania kwa kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ndiyo Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC.
Mkutano huu
umefunguliwa na Mhe. Dkt. Augustine Phillip Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Mhe. Prof. Makame Mbarawa
(Mb), Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Kufanyika kwa Mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya masuala ya
Miundombinu kunatokana na maazimio ya Mkutano wa Pili wa Wakuu wa Nchi
Wanachama wa COMESA, EAC na SADC uliofanyika Johannesburg, Afrika Kusini tarehe
14 Juni, 2011 ambao ulipitisha maeneo matatu ya kutekelezwa kwenye ushirikiano
wa Utatu wa COMESA – EAC – SADC. Maeneo hayo ni: 1) Kuunganisha Soko; 2)
Kuendeleza Miundombinu ili kuunganisha Nchi Wanachama kwa miundombinu iliyo
bora; na 3) Kukuza Viwanda.
Kwa upande wa Sekta za Miundombinu, huu ni Mkutano wa
Kwanza wa Mawaziri wa Nchi Wanachama wa
Utatu wa COMESA, EAC na SADC. Mkutano huu katika Ngazi ya Wataalam ulijadili
hatua zilizofikiwa na Nchi Wanachama katika uendelezaji wa miundombinu na
kupendekeza maamuzi ya kisera kwenye sekta za miundombinu ya uchukuzi
(barabara, reli, bandari, anga); teknolojia ya habari na mawasiliano; na
nishati.
Kwa ujumla Mkutano wa Mawaziri umepita na kujadili programu kuu
zifuatazo:
i.
Programu
ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport and Transit
Facilitation Programme (TTTFP);
ii.
Taarifa
za utekelezaji wa miradi na programu kuhusiana na Sekta ya Miundombinu ya
Uchukuzi (Anga, Barabara, Reli na Bandari); Sekta ya Mawasiliano na Sekta ya
Nishati;
iii.
Maendeleo ya Kanda za Uchukuzi (Corridor Development) za Jumuiya ya Utatu wa COMESA, EAC na SADC,
ambapo hatua mbalimbali za Utekelezaji wa Vituo vya Kutoa Huduma kwa Pamoja
Mipakani (OSBPs) kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya hizo zimejadiliwa;
iv.
Utekelezaji
wa Programu ya Kikanda wa Uendelezaji wa Miundombinu katika Ukanda wa Afrika
Mashariki, Ukanda wa Afrika Kusini na Ukanda wa Bahari ya Hindi (Regional Indicative Programme for Eastern
Africa, Southern Africa and the Indian Ocean (2014 – 2020); na
v.
Utekelezaji wa Miradi ya NEPAD Presidential Infrastructure Championship Initiative (PICI);
vi.
Rasimu ya Mpangokazi wa shughuli za utatu wa COMESA-
EAC- SADC hususan uratibu wa mikutano ya miundombinu;
vii.
Utafutaji raslimali fedha za kuwezesha shughuli za
utatu wa COMESA- EAC- SADC; na
viii.
Uzinduzi rasmi wa Programu ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya
Barabara kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport
and Transit Facilitation Programme (TTTFP).
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhe. Waziri Mahiga, pamoja na
kuwakaribisha Mawaziri nchini Tanzania na jijini Dar es Salaam, amesisitiza
umuhimu wa kuwa na miradi ya pamoja ya kuendeleza sekta ya miundombinu baina ya
Jumuiya za kikanda kama njia madhubuti ya kuwaletea maendeleo ya haraka
wananchi. Mhe. Mahiga pia amesisitiza kwamba Tanzania inathamini ushirikiano wa
kanda na hivyo itaendelea kushiriki kikamilifu katika juhudi za maendeleo za
kikanda ikiwemo zile za Jumuiya ya Utatu (Tripartite) kama njia mojawapo wa
utekelezaji wa Sera ya Tanzania ya Viwanda. Mwisho, Mhe. Mahiga amewatakia
mkutano mzuri Mawaziri wa Miundombinu akiwaomba kuibua mikakati na mapendekezo
madhubuti katika kuendeleza miundombinu katika eneo lote la UTATU.
Aidha, Mawaziri kwa pamoja, wakiongozwa na Mhe. Aggrey Henry Bagiire,
Waziri wa Uchukuzi na Ujenzi wa Jamhuri ya Uganda na ambaye atakuwa ni
Mwenyekiti wa Mkutano huo kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, watazindua rasmi Programu
ya Uendelezaji wa Sekta za Uchukuzi kwa njia ya Barabara kwa Nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Utatu wa COMESA-EAC-SADC (Tripartite Transport and Transit Facilitation Programme (TTTFP).
Uzinduzi huu utafanyika
leo tarehe 26 Oktoba, 2017 saa 9.00 Alasiri na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali
wa Serikali na Sekta Binafsi.
I
Imetolewa na,
KITENGO CHA MAWASILIANO
YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI,
TAREHE 26/10/2017