Friday, October 19, 2018

Dkt. Ndumbaro akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Kamati ya CPPCC ya China

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya  Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC), Bw. Lou Jiwei alipofika ofisini kwake Dodoma leo tarehe 19 Oktoba, 2018 kwa lengo la kumsalimia na kumpongeza kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo. Mkurugenzi huyo anaongoza ujumbe wa watu wanne wa Kamati hiyo ambao wapo nchini kwa mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai.

Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC) Bw. Lou Jiwei akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) walipokutana katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Jengo la LAPF jijini Dodoma kwa mazungumzo. Mkurugenzi huyo ni mgeni wa kwanza kutoka nchi za nje kumtembelea katika ofisi yake ya  Dodoma.

Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC) Bw. Lou Jiwei akimkabidhi zawadi ya kitabu  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) ikiwa  ni kumbukumbu ya kukutana naye  jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akibadilishana mawazo na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe.  Wang Ke baada ya kumaliza mazungumzo na Mkurugenzi wa Kamati ya Mambo ya Nje ya Mashauriano ya Kisiasa ya China (CPPCC).

Thursday, October 18, 2018

Makabidhiano rasmi ya Ofisi ya Naibu Waziri yafanyika

Mhe. Dkt. Damas Ndubaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki leo amekabidhiwa rasmi Wizara hiyo na aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan A. Kolimba (Mb), hafla ya makabidhiano ilifanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtaa wa Makole jingo la LAPF  jijini Dodoma. Katika hafla  ya makabidhiano walihudhuria Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara hiyo waliosimama nyuma ya viongozi hao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Ndumbaro (Mb) akimshukuru aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan A. Kolimba (Mb) katika hafla ya makabidhiano rasmi ya ofisi jijini Dodoma.

Picha ya pamoja ya Mhe. Dkt. Ndubaro Naibu Waziri Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeingia katika ofisi na Mhe. Dkt. Suzan A Kolimba aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo anayeondoka katika ofisi hiyo wakiwa wamekaa wakibadilishana mawazo.




Waziri Mahiga ziarani nchini India.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.),  akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mhe. Sushma Swaraj walipokutana katika Mkutano wa 9 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India Ngazi ya Mawaziri Uliofanyika mjini New Delhi, katika Mkutano huo uliotanguliwa na Mkutano wa Ngazi ya wataalamu wakiongozwa na Makatibu Wakuu Tarehe 15 na Tarehe 16 Octoba Ngazi ya Mawaziri. 

Pia katika Mkutano huo Serikali ya Tanzania na India ziliwekeana saini kwenye mikataba miwili, ukiwepo Mkataba wa Makubaliano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na India kwaajili ya kubadilishana uzoefu na kuwaandaa wanadiplomasia bora watakao weza kutekeleza diplomasia ya Uchumi na Mkataba wa makubaliano kati ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya India (NRDC).

Aidha, Ujumbe wa Tanzania Uliongozwa na Mhe. Dkt. Mahiga, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Justa Nyange, na viongozi kutoka kwenye Taasisi.

Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mhe. Sushma Swaraj mara baada ya kumalizika kwa Mkutano 
Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri Ukiendelea mjini New Delhi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) pamoja na Mhe. Swaraj wakiwekeana saini makubaliano ya mkutano wa 9 wa tume ya pamoja ya kudumu kati ya India na Tanzania mara baada ya kumalizika kwa majidiliano ya mkutano huo kwa Ngazi ya Mawaziri
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi Muombwa kwa niaba ya Chuo cha Diplomasia Tanzania wakiwekeana Saini na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia India Bw. Shri J.S. Mukul, kwenye Mkataba wa Makubaliano ya pamoja Kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Chuo cha Diplomasia India. Lengo la Mkatabao huo ni kubadilishana uzoefu na kuwaandaa wanadiplomasia bora watakao weza kutekeleza diplomasia ya Uchumi kati ya taasisi hizi mbili. 




Dkt. Mahiga akutana na Mkurugenzi wa Chuo cha Ulinzi na Usalama New Delhi, India.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisalimia na Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Ulinzi na Usalama nchini India Kapt. Guroreet S. Khurana (wa kwanza kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye chuo cha Ulinzi na Usalama,  jijini New Delhi, India. Dkt. Mahiga alifanya mazungumzo na Kapt Khurana, katika mazungumzo yao yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India, mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda (Hayupo pichani).
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Ulinzi na Usalama India, Kapt. Sarabjeet S Parmar
Mazungumzo yakiendelea.