Thursday, October 18, 2018

Waziri Mahiga ziarani nchini India.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.),  akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mhe. Sushma Swaraj walipokutana katika Mkutano wa 9 wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na India Ngazi ya Mawaziri Uliofanyika mjini New Delhi, katika Mkutano huo uliotanguliwa na Mkutano wa Ngazi ya wataalamu wakiongozwa na Makatibu Wakuu Tarehe 15 na Tarehe 16 Octoba Ngazi ya Mawaziri. 

Pia katika Mkutano huo Serikali ya Tanzania na India ziliwekeana saini kwenye mikataba miwili, ukiwepo Mkataba wa Makubaliano kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na India kwaajili ya kubadilishana uzoefu na kuwaandaa wanadiplomasia bora watakao weza kutekeleza diplomasia ya Uchumi na Mkataba wa makubaliano kati ya Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda (TIRDO) na Taasisi ya Utafiti na Maendeleo ya India (NRDC).

Aidha, Ujumbe wa Tanzania Uliongozwa na Mhe. Dkt. Mahiga, akiambatana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi Muombwa, Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Baraka Luvanda pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bi. Justa Nyange, na viongozi kutoka kwenye Taasisi.

Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa India Mhe. Sushma Swaraj mara baada ya kumalizika kwa Mkutano 
Mkutano wa Ngazi ya Mawaziri Ukiendelea mjini New Delhi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) pamoja na Mhe. Swaraj wakiwekeana saini makubaliano ya mkutano wa 9 wa tume ya pamoja ya kudumu kati ya India na Tanzania mara baada ya kumalizika kwa majidiliano ya mkutano huo kwa Ngazi ya Mawaziri
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan Mwinyi Muombwa kwa niaba ya Chuo cha Diplomasia Tanzania wakiwekeana Saini na Mkuu wa Chuo cha Diplomasia India Bw. Shri J.S. Mukul, kwenye Mkataba wa Makubaliano ya pamoja Kati ya Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Chuo cha Diplomasia India. Lengo la Mkatabao huo ni kubadilishana uzoefu na kuwaandaa wanadiplomasia bora watakao weza kutekeleza diplomasia ya Uchumi kati ya taasisi hizi mbili. 




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.