Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), akizungumza na waandishi wa Habari juu ya ujio wa Ujumbe mkubwa wa wawekezaji kutoka Ubelgiji, katika mkutano huo na waandishi wa habari Dkt. Ndumbaro aliwaeleza waandishi kuwa "Ushirikiano wetu na Ubelgiji umekuwa mkubwa sasa na kupitia Ubalozi wetu nchini humo umewezesha ujio huu ambapo leo mchana tunawapokea rasmi wangeni hao na tuna imani utafungua ajira mbalimbali zikiwemo za moja kwa moja". hivyo watanzania wachangamkie fursa zitakazoletwa na wawekezaji hao.
Aidha ujumbe huo wa wawekezaji utakuwepo nchini kuanzia Tarehe 24 mpaka 28 Octoba 2018, ambapo wawekezaji hao wanataraijiwa kufanya Kongamano kubwa la biashara hapo kesho katika Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.