Wednesday, October 24, 2018

Umoja wa Mataifa wadhimisha miaka 73 tangu kuanzishwa.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim akihutubia katika maadhimisho ya miaka 73 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, katika hotuba yake Mhe. Majaliwa amesema kwamba nchini Tanzania hakuna ubanaji wa uhuru wa vyombo vya habari wala taasisi zisizo za kiserikali.
Aidha, amesema jambo hilo linadhihirishwa na uwepo wa jumla ya vituo vya redio 152, ambavyo kati yake ni vituo vitatu tu ndivyo vinavyomilikiwa na Serikali. Maadhimisho hayo yamefanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam 24 Octoba 2018 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro naye akihutubia kwnye maadhimisho hayo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Juu na Chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria maadhimisho hayo wakifuatilia kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa na Mhe. Kassim Majaliwa (hayupo pichani).


Waziri Mkuu akiwa kwenye Jukwaa maalumu la kupokea heshima wakati wa maadhimisho hayo
Viongozi kwenye jukwaa kuu nao wakiwa wamesimama wakati wimbo ya Taifa ikipigwa

Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nao wakiwa wamesimama wakati wimbo ya Taifa ikipigwa, wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje Bw.  Deusdedit Kaganda
Mhe. Kassim Majaliwa kaiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ndumbaro, Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodrigues pamoja na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini.

Mhe. Kassim Majaliwa akiagana na Dkt. Ndumbaro mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Mratibu wa Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bw. Alvaro Rodrigues naye akiagana kwa furaha na Mhe. Kassim Majaliwa









No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.