Tuesday, October 16, 2018

Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi wa Uganda,Uingereza na Kaimu Balozi wa Marekani

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Damas Ndumbaro(Mb.) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe wamekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Patterson. Katika mazungumzo yao Bi. Patterson alitumia firsa hiyo kujitambulisha na kuwampongeza kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Aidha, Dkt Ndumbaro amemuhakikishia Bi. Patterson kumpa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza majukumu yake. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Mazungumzo yakiendelea,  wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na wakwanza kulia ni Katibu wa Naibu Waziri Bw. Charles Faini na wa kwanza kushoto ni Afisa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.  
Dkt. Ndumbaro akiagana na Bi. Patterson


=====Dkt. Ndumbaro akutana na Balozi Cooke=====





Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke, katika Mazungumzo hayo Mhe. Cooke ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kuwapongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani). Aidha, Balozi Cooke alimweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Uingereza ni wa muda mrefu ambapo nchi hizi mbili zinashirikiana katika sekta mbalimbali za kukuza uchumi zikiwemo Elimu, Afya na Kilimo. Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto), pamoja na Maafisa wa Mambo ya Nje, wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro na Balozi Cooke.
Picha ya pamoja mara ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya Dkt. Ndumbaro (wa pili kulia) na Balozi Cooke (wa pili kutoka kushoto), Dkt. Mnyepe pamoja na Afisa Ubalozi wa Uingereza Bw. Matt Sutherlal 



======Dkt. Ndumbaro akutana na Mhe. Kabonero=======  




Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damasi Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Mhe. Richard T. Kabonero. Katika Mazungumzo hayo Mhe. Kabonero ametumia fursa hiyo kujitambulisha na kumpongeza Mhe. Ndumbaro pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (hayupo pichani). Aidha, Balozi Kabonero alitumiafursa hiyo kumweleza Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Mnyepe kuwa mahusiano kati ya Tanzania na Uganda ni ya muda mrefu, ambapo kutokana na mahusiano mazuri kati ya nchi hizi imepelekea Serikali ya Uganda kuamua kupitisha ujenzi wa bomba la mafuta tanzania, ambapo ujenzi huo utazalisha fursa mbalimbali na kukuza vipato vya wananchi wa pande zote mbili pamoja na kukuza uchumi baina ya mataifa hayo mawili. Pia ameupongeza ufanisi mzuri wa Bandari ya Dar es Salaam katika kuwa hudumia.

Kwa upande wa Dkt. Ndumbaro amemuhakikishia Balozi Kabonero kumpatia ushrikano wa kutosha wakati wa utekelezaji wa majukumu yake ya kuiwaikilisha Taifa lake hapa nchini, Mazungumzo hayo yamefanyika Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam Tarehe 16/10/2018
Katibu Mkuu wa Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto), pamoja na Maafisa Mambo ya Nje wafuatilia kwa makini mazungumzo hayo. 
Mazungumzo yakiendelea
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kabonero.
Picha ya pamoja.





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.