UBALOZI WA TANZANIA VISIWANI COMORO
WAADHIMISHA SIKU YA MWALIMU NYERERE
TAREHE
13 Oktoba, 2018
Ubalozi wa Tanzania Visiwani Comoro kwa
kushirikiana na Umoja na Vijana Visiwani hapa ujilikanao kama Udjamaa wa Komori
na Afrika Mashariki tarehe 13 Oktoba, 2018 uliadhimisha siku ya Mwalimu Nyerere
(Nyerere Day). Maadhimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa mkutano wa Ubalozi
uliopo katika mtaa wa Oasis, Moroni, Visiwani Comoro.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika
maadhimisho hayo Visiwani hapa ambapo lengo lake ilikuwa ni:-
i.
Kuonyesha
mchango wa Mwalimu Nyerere na Tanzania kwa ujumla katika ukombozi wa Visiwa vya
Comoro.
ii.
Kuelezea
historia ya baba wa Taifa hasa kwa Vijana wa Comoro amabapo historia hiyo
ilipotea kutokana na juhudi za Mfaransa.
iii.
Kudumisha
ushirikiano wa kihistoria na kindugu uliopo baina ya Tanzania na Comoro hasa
kwa kuzingatia kwamba Comoro ipo katika harakati za kujianga kwenye Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
Katika maadhimisho hayo, Balozi wa
Tanzania, Visiwani Comoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba alifanya mahojiano na
vyombo mbalimbali vya habari viliopo Visiwani hapa na kuelezea kuhusu maisha na
Mwalimu Nyerere na mchango wake katika harakati za ukombozi kwa Bara la Afrika.
Aidha, katika hilo Mhe. Balozi alisistiza kudumisha amani Visiwani Comoro wakati
nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais mapema mwaka 2019.
Balozi wa Tanzania Visiwani Komoro Mhe. Sylvester M. Mabumba akifanya mahojiano na Vyombo mbalimbali vya Habari Visiwani Komoro |
Balozi Mabumba (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Umoja wa Vijana wa Komoro maarufu kama Udjamaa wa Komoro na Afrika Mashariki |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.