Watanzania waishio Visiwani Komoro wakimsikilisha Mhe. Mabumba hayupo pichani.
Watanzania waishio Visiwani Komoro wakiwa kayika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa Kongamano hilo |
UBALOZI WA TANZANIA, KOMORO WAADHIMISHA
MIAKA19 YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE
TAREHE 26 – 27 Octoba, 2018
Katika harakati za kuendeleza kukuza na
kuhuisha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Ubalozi wa Tanzania Visiwani Komoro kwa
kushirikiana na Diaspora ya Watanzania Visiwani Komoro (TADICO) pamoja na taasisi
ya kijamii ya Komoro ijulikanayo kama Udjamaa wa Komori na Afrika Mashariki
uliandaa Kongomano la siku mbili kuanzia tarehe 26 – 27 Oktoba, 2018 kama
sehemu ya kumenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kongomano hilo lilifanyika katika
ukumbi wa Bunge la Taifa la Komoro ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa
Elimu wa Komoro, Mhe. Salime Mohamed Abderemane. Aidha, kutoka Tanzania, Mhe.
Pro. Mark Mwandosya alialikiwa kama mmoja ya watoa mada juu ya maisha ya
Mwalimu Nyerere.
Wageni wengine mashuhuri walioshiriki
katika Kongomano hilo ni pamoja na Mhe. Mohamed Msaidie, Waziri wa zamani wa
Mambo ya Ndani wa Komoro, Mhe. Balozi Ahmed Thabeet, mmoja ya waazilishi wa
Chama cha Ukombozi cha Komoro kujilikanacho kama MOLINACO. Aidha, Balozi wa
Tanzania Visiwani Komoro, Mhe. Sylvester M. Mabumba naye pia aliweza kushiriki
kikamilifu katika Kongomano hilo.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ubalozi wa
Tanzania Visiwani Komoro kusheherekea kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Visiwani
hapa. Lengo la Kongomano hilo ilikuwa ni kuelezea mchango wa Mwalimu Nyerere na
Tanzania kwa ujumla katika harakati za ukombozi wa Visiwa vya Komoro kuanzia
1962 – 1975. Aidha, Kongomano hilo lililenga pia kuikurubisha Komoro katika
ukanda wa Afrika Mashariki, kwa kuwa mda mrefu Visiwa hiyo vimeelekeza
mahusiano yake katika nchi za Ulaya na Mashariki ya Kati.
Watoa mada mbalimbali waliweza kuelezea
kwa kina mchango wa Mwalimu Nyerere katika harakati za ukombozi wa Visiwa vya Komoro
na Afrika kwa ujumla. Prof. Mwandosya kwa upande wake alielezea mchango wa
Mwalimu katika harakati zake za kudumisha umoja na kuwasihi wa Komoro kudumisha
umoja wao hasa katika kipindi hiki ambapo nchi hiyo inapitia mageuzi makubwa ya
kisiasa.
Kongomano la kumuenzi Mwalimu Nyerere lilifana
sana na imekuwa ni chachu kwa Wakomoro kuona umuhimu wa kudumisha mahusiano ya
(Kusini-Kusini), South-South Cooperation. Ubalozi umedhimiria kuendeleza Kongomano
la Mwalimu kwani imeonekana yanachangia sana kudumisha mahusiano mazuri yaliopo
baina ya Tanzania na Komoro.