Wednesday, November 7, 2018
Tangazo kwa Umma
Tanzania na New Zealand kuimarisha sekta ya ufugaji
Mhe. Mike Burrell akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo. Mwingine katika picha ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Bertha Makilagi |
Mhe.Abdallah Hamisi Ulega akiagana na Mgeni wake, Mhe. Mike Burrell |
Naibu Balozi wa Israel nchini Mhe. David Eyal atembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Tuesday, November 6, 2018
TAARIFA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MISRI,
TAARIFA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MISRI,
Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri limefunguliwa leo katika hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam. Kongamano hilo limeandaliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Misri hapa nchini chini ya uratibu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wafanyabiashara na wawekezaji wapatao 35 kutoka Misri wameshiriki kwenye Kongamano hilo kwa lengo la kutafuta fursa katika sekta za kilimo, mifugo, viwanda, madini na ujenzi.
Mgeni rasmi katika Kongamano hilo alikuwa ni Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Waziri Mahiga aliwakaribisha wafanyabiashara hao kuja kuwekeza nchini Tanzania katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, madini na utalii. Aidha, Waziri Mahiga alisifia mahusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Misri na juhudi za Serikali ya Tanzania kuendelea kuboresha mazingira ya biashara hapa nchini ili kuvutia wafanyabiashara na wawekezaji.
Kongamano hilo linafanyika leo na kesho na linaenda sambamba na mikutano ya ana kwa ana (B2B) kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Misri kwa lengo la kuangalia fursa mbalimbali zitakazowezesha kuanzishwa kwa ushirikiano katika Nyanja za biashara na uwekezaji. Aidha kesho kuna mikutano kati ya taasisi za serikali na wafanyabiashara hao (B2G). Taasisi zinazotarajiwa kutoa mada ni TIC, Tanzania Food and Drug Authority (TFDA) na Tanzania Bureau of Standard (TBS).
Ujumbe huo wa wafanyabiashara utaelekea Zanzibar tarehe 08 Novemba 2018 kwa ajili ya kushiriki kwenye Kongamano katika hoteli ya Hyatt Park, Zanzibar tarehe 09 Novemba, 2018
Sunday, November 4, 2018
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapenda
kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya
ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na Mhe. Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.
Katika mkutano wake na vyombo vya habari, Mhe.
Mkuu wa Mkoa alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika
jiji la Dar es Salaam.
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa
kufafanua kwamba, hayo ni mawazo yake na sio msimamo wa Serikali.
Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ingependa kutumia nafasi hii kukumbusha na kusisitiza kwamba, itaendelea kuheshimu
mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na
kuridhia.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na
itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
04 Novemba, 2018
Friday, November 2, 2018
Dkt. Ndumbaro ashiriki Mkutano wa nchi za mwambao wa Bahari ya Hindi
Mkutano ukiendelea |
Picha ya pamoja ya Mawaziri |
Thursday, November 1, 2018
Dkt. Ndumbaro aapa kuwa Mbunge wa EALA
Dkt. Ndumbaro akiwa tayari kwa vikao vya Bunge la Afrika Mashariki mara baada ya kuapishwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)