Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), akiweka shada la Ua kwenye mnara uliopo kwenye makaburi ya wataalam 70 kutoka China waliokufa wakati wa ujenzi wa Reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya utamaduni wa Wachina na kuwakumbuka wataalam hao yaliyofanyika kwenye eneo la makaburi walikozikwa wataalam hao lililopo Gongo la mboto, Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Hassan Abbas na Kurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Caesar C. Waitara na viongozi mbalimbali wa serikali
Prof. Palamagamba Kabudi pamoja na Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakitoa heshima zao kwa kuinamisha vichwa kama ishara ya kuwakumbuka wataalam hao kutoka China.
Prof. Palamagamba pamoja na Mhe. Wang Ke wakiweka maua katika moja ya kaburi la wataalam hao.
Bw. Caesar Waitara akiweka Ua katika moja ya kaburi la wataalam hao.
Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.), akihutubia katika hafla hiyo mara baada ya kumaliza zoezi la kuweka maua kwenye makaburi ya wataalam wa kichina waliokufa wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara. Katika Hotuba hiyo waziri Kabudi aliendelea kuusifu ushirikiano wa Tanzania na China katika sekta mbalimbali ambapo Ujenzi wa reli ya Tazara ulipelekea kuanzishwa kwa viwanda mbalimbali.
Aidha, alieleza kuwa kutoka na Ushirikiano ulipo Tanzania inatarajia kufungua ubalozi mdogo katika mji wa Guangzhou pamoja na kuanzisha Safari ya Ndege za Shirika la Tanzania (ATCL) kuelekea moja kwa moja Guanghzou ambapo utapelekea kuongeza watalii kutoka China kuja kutembelea vivutio vilivyopo nchini Tanzania.
Balozi Wang Ke naye akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini hotuba zilizo kuwa zikiendelea kutolewa na Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Wang Ke (hawapo pichani)
Prof. Palamagamba John Kabudi akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya vifo vya wataalam hao.
Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza hafla hiyo.
Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi Wang Ke wakiwa katika picha ya pamoja na wageni engine waliohudhuria tulip hilo.