TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
Vivutio vya Utalii
kutangazwa Malaysia, Ufilipino, Thailand na Indonesia
Dodoma, 11 Aprili 2019
Makampuni 20 ya Mawakala wa Utalii na Tiketi za ndege
(Tour Operators & Travel Agents) pamoja na Waandishi wa Habari kutoka
katika nchi za Malaysia, Indonesia, Ufilipino na Thailand walifanya ziara ya
mafunzo ya kutembelea vivutio vya utalii nchini kuanzia tarehe 1 – 7 Aprili 2019.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini
Malaysia kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) yalijumuisha
washiriki 20 ambapo Malaysia ilitoa washiriki 5, Thailand washiriki 6, Philippines
Washiriki 4 na Indonesia washiriki 5.
Washiriki hao walitembelea maeneo mbalimbali
yakiwemo Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro, Mbuga ya Serengeti, duka Maarufu la kuuza
madini ya Tanzanite, duka maarufu la zawadi la Arusha Cultural Heritage, sehemu ya historia ya masalia ya Binadamu
wa Kale la Olduvai (Oldupai) Gorge na Kijiji cha Wamasai ili kujifunza uhalisia
wa maisha yao. Wakiwa kwenye maeneo
hayo, wageni walifanikiwa kuona wanyama maarufu watano- big five (Simba, Nyati, Faru, Chui na Tembo) na kushuhudia makundi
ya Wanyama aina ya Nyumbu, Pundamilia, na Swala ambao hufanya ziara ya mzunguko
maarufu kama Great Migration.
Wageni kabla ya kuagwa na Mwenyekiti wa Bodi ya
Utalii, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo pamoja na Bibi. Devotha Mdachi, Mkurugenzi
Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii waliahidi kuitangaza Tanzania kama eneo jipya la
utalii kwa nchi zao.
Wakati huo
huo, Balozi
wa Tanzania nchini Malaysia, Mhe. Dkt. Ramadhani Dau amepokea nafasi 160 za
ufadhili wa masomo ya elimu ya juu (scholarships) kwenye taaluma mbalimbali
zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 1.9 sawa na Shilingi bilioni 4 za Tanzania.
Ufadhili huo umetolewa na Chuo Kikuu cha Selangor (University of Selangor)
ambacho pia kinajulikana kama UNISEL kilichopo katika Mkoa wa Selangor,
Malaysia, unahusisha masomo ya Bachelors
of Civil Engineering, Bachelors of Electrical Engineering, Bachelors of Mechanical
Engineering, Bachelors of Occupational Health and Safety, Bachelors of Medical Laboratory,
Bachelors of Industrial Biotechnology, Bachelors of Computer Science na Bachelors
of Information Technology. Hivi karibuni Watanzania watafahamishwa utaratibu
wa kuomba masomo hayo.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.