Thursday, April 25, 2019

Tanzania na China zaadhimisha miaka 55 ya ushirikiano

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako (Mb.) akitoa hotuba kama mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya miaka 55 ya Ushirikiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Watu wa China yaliyofanyika kwenye ukumbi uliopo kwenye Maktaba  ya Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam tarehe 24 Aprili, 2019.

 Katika hotuba yake, Prof. Ndalichako ameipongeza China kwa kuimarisha ushirikiano  na  Tanzania hususan katika sekta za Elimu, Biashara na Ujenzi wa miundombinu. Aidha,   amesema kuwa mahusiano kati ya Tanzania na China ni ya muda mrefu na mchango wa nchi hiyo kwenye maendeleo ya Tanzania ni dhahiri akitolea mfano  ujenzi wa Reli ya TAZARA pamoja na ujenzi wa viwanda mbalimbali vya nguo nchini. Vilevile China imeendelea kushirikiana na Tanzania kwenye Sekta ya Afya kwa kubadilishana uzoefu.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda, Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara, na viongozi mbalimbali kutoka Taasisi  za umma na binafsi nchini. 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda akiwa na mke wake Mhe. Tunu Pinda (kushoto)  pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na Prof. Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.
Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia hotuba hiyo.

Prof. Ndalichako akiendelea kuhutubia kwenye maadhimisho hayo.
Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China nchini, Mhe. Wang Ke naye akihutubia kwenye maadhimisho hayo. 
Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho hayo.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo  Pinda pamoja na mke wake Mhe. Tunu Pinda (kushoto) pamoja na viongozi wengine kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakipitia kitabu chenye kuonyesha ushirikiano wa Tanzania na China kwenye sekta mbalimbali.
Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza (kushoto) kwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia Bw. Caesar Waitara (kulia) wakipitia kitabu kinachoonesha namna Tanzania na China zinavyoshirikiana kwenye sekta mbalimbali.
Maafisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijadiliana jambo wakati wa maadhimisho hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akitambulishwa kwa wageni walioshiriki maadhimisho hayo.
Mshehereshaji, Bi. Bertha Makilagi akitoa mwongozo wa ratiba ya maadhimisho hayo kwa wageni waalikwa.
 Juu na chini ni maonyesho mbalimbali yakiendelea kuonyeshwa na vikundi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo


Mgeni Rasmi pamoja na wageni waalikwa wakiwa wamesimama wakati nyimbo za  mataifa ya Tanzania na China zikiimbwa.
Kikundi chenye mchanganyiko wa wanafunzi kutoka Tanzania na China wakiongoza kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania na China kabla maadhimisho hayo kuanza.
Naibu Waziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wasanii aliyekuwepo kwenye maadhimisho hayo
Mhe. Prof. Ndalichako na wageni waalikwa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi pamoja na Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja.

















 















No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.