Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya Kamusi ya
Kiswahili na Kingereza pamoja na Vitabu vya Kiswahili Rais wa Afrika Kusini
Mheshimiwa Cyril Ramaphosa kwa ajili ya kujifunza lugha hio ya Kiswahili leo
Mei 26, 2019 ikiwa ni siku moja baada ya
kuapishwa kuwa Rais wa Nchi hiyo na
kabla hajateua Baraza lake la Mawaziri.
|
Tuesday, May 28, 2019
RAIS MHE. DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA AFRIKA KUSINI MHE. CYRIL RAMAPHOSA KATIKA IKULU YA PRETORIA NCHINI AFRIKA KUSINI IKIWA NI SIKU MOJA MARA BAADA YA KUAPISHWA NA KABLA YA KUTEUA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI MEI 26, 2019
Makamu wa Rais ashiriki sherehe za uapisho za Rais wa Comoro
Dodoma, 28 Mei 2019
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu wa Rais ashiriki sherehe za uapisho za Rais wa Comoro
Kufuatia Mwaliko
kutoka Serikali ya Comoro, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Samia Suluhu Hassan aliongoza ujumbe wa Tanzania katika sherehe za
kuapishwa kwa Rais Mteule wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Azali Assouman
zilizofanyika Moroni, terehe 26 Mei 2019.
Sherehe hizo
zinafuatia ushindi alioupata Mhe. Azali katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo
uliofanyika tarehe 24 Machi 2019.
Mara baada ya Sherehe
za Uapisho, Mhe. Makamu wa Rais alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe.
Azali ambapo katika mazungumzo hayo, Mhe. Makamu wa Rais aliishukuru Serikali
na Wananchi wa Comoro kwa mwaliko na mapokezi mazuri.
Aidha, aliwasilisha
salamu za pongezi kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumhakikishia kuendeleza uhusiano na
ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili.
Kwa upande wake, Mhe.
Azali alielezea furaha yake kwa ujio wa Mhe. Makamu wa Rais na kueleza kwamba
hiyo ni ishara ya udugu na uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Comoro.
Aidha, Mhe. Rais alieleza
kwamba kutokana na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania, ipo
haja kwa Tanzania kuendelea kuisadia Comoro katika sekta mbalimbali.
Mwisho, aliishukuru Tanzania
kwa salamu za pole kufuatia nchi hiyo kukumbwa na kimbunga Kenneth tarehe 26
Aprili 2019.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki
Thursday, May 23, 2019
Waziri Prof. Kabudi akutana na Kiongozi wa Kanisa la Othodox
Tuesday, May 21, 2019
Waziri Kabudi akutana na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Bi. Jane Edmondson pamoja na ujumbe alioambatana nao |
Call for Applications for the 2019/2020 Academic Year at the Pan African University
Dodoma. 21st May 2019
PRESS RELEASE
Call for Applications for the 2019/2020 Academic Year at the Pan African University
The Pan African University an initiative of the Heads of State and Government of the African Union is inviting young, qualified, talented
and enterprising Tanzanians to apply for Masters or PhD degree
programmes at any of the four Pan African University Institutes listed below:
Interested candidates should visit the following links for enquiries and
more details: - https://www.au-pau.org/submission and pau.scholarships@africa-union.org.
The call for applications is open from May 14, 2019
to June 27, 2019.
Issued by;
Government
Communication Unit,
Ministry of
Foreign Affairs and East African Cooperation
|
Waziri Kabudi akutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania
Maafisa Ubalozi wa Uingereza hapa nchini wakisikiliza mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Sarah Cooke (hawapo pichani) |
Mazungumzo yakiendelea |
Waziri Kabudi akutana na Balozi wa Iran nchini Tanzania
Maafisa Ubalozi wa Irani hapa nchini wakisikiliza mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mousa Farhang (hawapo pichani) |
Mazungumzo yakiendelea. |
Subscribe to:
Posts (Atom)