Thursday, October 10, 2019

PROF. KABUDI AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA HISPANIA HAPA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini. Kulia kwa Prof. Palamagamba John Kabudi ni Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero.

Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi huyo hapa Nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akigongeana glasi ishara ya kutakiana kheri na Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero,wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini.

Baadhi ya waalikwa walihohudhuria maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini.

Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu

Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu. Mkutano katika ngazi hiyo ulikuwa wa siku mbili na umemalizika leo.
Pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 11 na 12 Oktoba 2019.
Pichani; wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka Rwanda, Balozi Richard Masozera akiongoza mkutano huo, wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Miundombinu, Mhandisi Steven D. M. Mlote, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia sekta za uzalishaji na jamii, Mhe. Christophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara inayoshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kenya, Bw. Rafael Kanoth.

Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akisaini taarifa ya mapendekezo mbalimbali katika mkutano huo kwaajili ya kuwasilisha taarifa hiyo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri. Pembeni yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akishuhudia zoezi la utiaji saini.

Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban pamoja na Dkt. Ndumbaro na Prof. Mchome wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo.

Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen P. Mbundi pamoja na wajumbe wengine wa mkutano wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo.

Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (kushoto) pamoja na sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wakifuatilia majadiliano.


Sehemu nyingine ya wajumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano katika mkutano.

Viongozi wa ujumbe wa mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wakikamilisha zoezi la utiaji saini wa taarifa ya mapendekezo ya mkutano huo.

Wednesday, October 9, 2019

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WAANZA MAJUKUMU YA UENYEKITI WA KUNDI LA MABALOZI KUTOKA NCHI ZA SADC WALIOPO NCHINI HUMO

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akipokea Makabrasha kutoka kwa Balozi wa Namibia nchini India, Mhe. Gabriel P. Sinimbo ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa Kundi la Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC ) waliopo India. Tanzania ilipokea uenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Namibia mwezi Agosti 2019 wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi Luvanda (katikati) akizungumza mara baada ya kupokea uenyekiti wa kundi la Mabalozi kutoka Nchi za SADC waliopo India. Katika picha ni Balozi Sinimbo (kulia) kutoka Namibia na Balozi E.A Ferreira (kushoto) kutoka Msumbiji.
Mkutano ukiendelea
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na na Mabalozi kutoka nchi za SADC waliopo India pamoja na Maafisa wa Ubalozi mara baada ya kikao cha Mabalozi hao kilichofanyika kwenye Jengo la Ubalozi jijini New Delhi.
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Zambia nchini India, Mhe. Judith K. Kapijimpanga ambaye kabla ya kuiwakilisha Zambia nchini India alihudumu katika nafasi hiyo nchini Tanzania.
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, Dkt. Kheri Goloka (kushoto) na Bi. Natihaika Msuya (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kundi la Mabalozi wa nchi za SADC nchini India aliyemaliza muda wake Balozi wa Namibia  Mhe. Gabriel P. Sinimbo.




Monday, October 7, 2019

Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango.

Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango umefunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Jengo la Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha na utafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 12 Oktoba 2019.
 Mkutano huo unaanza na vikao vya awali ambavyo ni kikao cha Maafisa Wa
andamizi kinachofanyika tarehe 7 na  8 Oktoba 2019  na utafuatiwa na kikao ngazi ya Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 9 na 10, na kumalizia na  ngazi ya Mawaziri tarehe 11 na 12 Oktoba 2019.
Pichani; Wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kikao cha ngazi ya Wataalamu na Afisa Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Jamhuri ya Rwanda, Bw. Emmanuel Kamugisha akiongoza kikao hicho. Pembeni ya Mwenyekiti wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Christophe Bazivamo, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Forodha na Biashara, Bw. Keneth Bagamuhunda, na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Raphael Kanoth.
Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu. Wapili kushoto ni Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen Mbundi, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Benard Haule, wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bi. Caroline Chipeta na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Gerald Mweli.

Ujumbe wa Tanzania ukifatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu.

Mkutano ukiendelea.

Simbu afuzu moja kwa moja kushiriki mashindano ya mwakani

Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab akiwa na wakimbiaji wa Tanzania walioshiriki mbio za marathon jijini Doha, Qatar. wakimbiaji hao walienda Ubalozini kuaga kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.

Wakimbiaji wa Tanzania walimaliza rasmi mashindano ya mbio za Marathon na kwa bahati mbaya wanariadha wawili hawakuweza kumaliza mbio hizo kutokana na maumivu ya goti na misuli. Mwanariadha Alphonce Simbu ambaye alikuwa anatetea medali yake ya shaba alishika nafasi ya 16 na alikuwa miongoni mwa wakimbiaji 20 bora ambao wamefuzu moja kwa moja kushiriki mashindano ya mwakani.

Wakimbiaji wa Ethiopia walishinda medali za dhahabu na fedha na Mkenya alishinda medali ya shaba.

Kwa mujibu wa Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab, Mwanariadha Simbu anaonekana ana uwezo mkubwa wa kuweza kushinda na amewasihi wakimbiaji hao waendelee kuwasiliana na ofisi ya Ubalozi ili kuwasaidia kupata ufadhili wa kuwajengea uwezo ikiwemo kupatiwa msaada wa mafunzo na vifaa.

Saturday, October 5, 2019

RAIS MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA HUDUMA PAMOJA (OSBP) MPAKANI TUNDUMA/NAKONDE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli, akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), alipowasili katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja (OSBP) Mpakani Tunduma/Nakonde.

Kituo hicho kimefunguliwa leo tarehe 5 Oktoba 2019, na 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Changwa Lungu.

Wakizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika zoezi la uzinduzi wa kituo hicho, kwa nyakati tofauti Mhe. Dkt. Magufuli na Mhe. Lungu walieleza kuwa wataendelea kudumisha uhusiano mzuri wa kidiplomasia uliodumu kwa muda mrefu baina ya nchi hizo mbili (Tanzania na Zambia) kwa maendeleo ya wananchi.

Aidha, Rais Magufuli alizungumzia umuhimu wa kuiongezea ufanisi Reli ya TAZARA ili kuchagiza kasi ya biashara baina ya Tanzania na Zambia.

Kadhalika, Mhe. Rais Magufuli amewahimiza Wananchi wa mji wa Tunduma kuulinda mpaka kwa kuepuka kujenga katika eneo la mpaka huo.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki amewapongeza Wananchi wa Mji wa Tunduma kwa kuendelea kulinda na kudumisha amani mpakani hapo. Vilevile ametumia fursa hiyo kuwasihi kuendelea na juhudi za kukuza biashara baina yao na Zambia ili kuboresha maisha yao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, alipowasili katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja (OSBP) Mpakani Tunduma/Nakonde kwa ajili ya ufunguzi.
Taswira ya Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja (OSBP) Mpakani Tunduma/Nakonde.
Taswira ya Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja (OSBP) Mpakani Tunduma/Nakonde.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli, akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) alipowasili katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Tunduma/Nakonde
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli  akifuatilia maelezo kutoka  kwa Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) kabla ya kuanza kwa zoezi la ufunguzi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Tunduma/Nakonde. 
Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb)  akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP) Tunduma/Nakonde.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli, na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Changwa Lungu ,wakiangalia jiwe la msingi wakati wa zoezi la ufunguzi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja (OSBP) mpakani Tunduma/Nakonde tarehe 5 Oktoba, 2019 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli, na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Changwa Lungu, pamoja na Wafadhili wa Ujenzi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja (OSBP) mpakani Tunduma/Nakonde wakipanda mti katika zoezi la uzinduzi wa Kituo hicho 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John  Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Changwa Lungu wakikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja (OSBP) mpakani Tunduma/Nakonde tarehe 05 Oktoba, 2019.

Thursday, October 3, 2019

MAANDALIZI KUELEKEA UFUNGUZI WA KITUO CHA PAMOJA (OSBP) MPAKANI TUNDUMA/NAKONDE


UBALOZI WA TANZANIA, UHOLANZI WASHIRIKI KWA MAFANIKIO TAMASHA LA EMBASSY FESTIVAL

Balozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akitoa maelezo kwa mgeni aliyetembelea Banda la Tanzania wakati wa Tamasha maarufu kama Embassy Festival lililofanyika hivi karibuni. Tamasha hilo huandaliwa na Manispaa ya The Hague kwa kushirikiana na Balozi za nchi mbalimbali zenye Ofisi zake The Hague kwa lengo la kutangaza tamaduni za nchi hizo.
Balozi Irene Kasyanju (mwenye fulana kulia) pamoja na Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Bibi Naomi Zegezege Mpemba (wa pili kushoto) wakitoa maelezo kuhusu Tanzania kwa wageni
waliotembelea Banda la Tanzania, huku Bw. Denis Baraka (wa kwanza kushoto)  ambaye ni Mtanzania na mdau wa shughuli za utalii ambaye kwa sasa anasoma nchini Ujerumani na ambaye kutokana na kupenda kutangaza utalii wa Nchi yake alisafiri kutoka Kiel, Ujerumani kuja Uholanzi kuungana na Ubalozi pamoja na Watanzania wengine kwenye Embassy Festival.
Mwonekano wa Banda la Tanzania na wageni waliotembelea.
Balozi Irene Kasyanju (wa tatu kushoto) akiwa na walishiriki wa maonesho ya mavazi pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wakiwa wamevaa fulana za kuitangaza Tanzania ambao ni Bw. Issa Lupatu, Mwambata Fedha wa Ubalozi (wa pili kulia aliyevaa miwani) na Bw. John Appolo Kilasara,Katibu wa Chama cha Watanzania wanaoishi Uholanzi (Tanzanians in the Netherlands – TANE) ambaye pia ni mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha ISS nchini Uholanzi
Balozi Irene Kasyanju akiwa na Bi. Bahia Kihondo, Mtanzania aliyeandaa maonesho ya mavazi
pamoja na watoto ambao walifungua maonyesho hayo kwa kusoma shairi fupi kwa lugha ya Kidachi na Kiswahili. 
Watazamaji wa maonesho ya mavazi yaliyotangaza utamaduni wa Mtanzania walikusanyika kwa
wingi kutazama maonesho hayo

Mwonekano wa Banda la Tanzania kwa sehemu ya ndani, likiwa limefurika Diaspora waliofika
kulitembelea na kupata fursa ya kuzungumza na mmoja wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Uholanzi, Bi Linda Mkony (aliyevaa koti katikati) na Bw. Denis Baraka, wakiwa pia wamevaa
na fulana maalum za kuitangaza Tanzania
Washiriki wakionesha vazi lenye michoro ya wanyama “animal prints” wanaopatikana kwenye mbuga za Tanzania
kwa mtindo wa kisasa
Maonesho ya mavazi yakiendelea– vazi la khanga.

 Washiriki wa maonyesho ya mavazi wakiwa katika vazi la Kimasaai.
====================================================================================================

UBALOZI WA TANZANIA, UHOLANZI WASHIRIKI KWA MAFANIKIO
TAMASHA LIJULIKANALO KAMA “EMBASSY FESTIVALTHE HAGUE”

Ubalozi wa Tanzania The Hague, Uholanzi umeshiriki katika Tamasha maarufu la Embassy Festival lililofanyika mwezi Septemba, 2019. Tamasha hili huandaliwa na Manispaa ya The Hague kwa kushirikiana na Balozi za nchi mbalimbali zenye Ofisi zake nchini humo kwa lengo la kutangaza utamaduni wa nchi hizo.

Kama ilivyokuwa kwa balozi nyingine, Ubalozi wa Tanzania ulikuwa na banda lake kwa ajili ya kuonesha utamaduni wa Tanzania. Kwa kushirikiana na Watanzania wanaoishi Uholanzi (Diaspora), Ubalozi ulitumia fursa hiyo kutangaza utamaduni pamoja na vivutio vya utalii zikiwemo mbuga za wanyama.

Ubalozi uliandaa maonesho ya mavazi (fashion show) kwa kuonesha vazi la Kimasai (shuka na shanga, n.k.), pamoja na khanga. Aidha, Ubalozi uliandaa maonesho ya mavazi na vitambaa vyenye animal prints za Simba, Chui (The big five), Twiga na Pundamilia na kuvionesha kwa mtindo wa kisasa na hivyo kuvutia watu wengi.

Diaspora wajasiriamali walipata fursa ya kuuza bidhaa zao mbali mbali za asili kama vile khanga, chai, kahawa ya Tanzania, shanga, hereni, viatu na bangili. Watu wengi waliotembelea Banda la Tanzania walifurahia korosho, chai na kahawa vyote kutoka Tanzania vilivyokuwa vimeandaliwa mahsusi kwa ajili yao.

Ubalozi umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuitangazaTanzania kupitia tamasha hilo ambapo idadi kubwa ya watu walishiriki na kuchukua vipeperushi vya kutangaza utalii wa nchi.

PROF. KABUDI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU KATIBU KATIBU MKUU UMOJA WA MATAIFA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamgamba John Kabudi (Mb) akislimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed katika ofisi za Umoja huo zilizopo New York Marekani.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) hayupo pichani,wakati akimkaribisha kwa mazungumzo katika ofisi za Umoja huo zilizopo New York Marekani.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed (Hayupo pichani) wakati alipokwenda katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York Marekani.

Naibu katibu mkuu wa Umija wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na ujumbe wake (hawapo pichani) katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York Marekani.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt. Amina Mohammed na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na ujumbe wake. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Umoja wa Mataifa zilizopo New York,Marekani.