Mkutano
wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo
Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kufanyika hapa nchini kuanzia tarehe 11
hadi 17 Machi, 2020 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNICC) jijini Dar es Salaam.
Akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushiriikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema
kuwa mkutano huo utafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 17 Machi 2020 ambapo
utatanguliwa na mkutano wa wataalamu pamoja na Makatibu Wakuu na kufuatiwa na
mkutano wa mawaziri tarehe 16 - 17 Machi, 2020.
"Pamoja
na mambo mengine, mkutano huu utahusisha Mawaziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mawaziri wa Fedha, Uchumi na Mipango pamoja na
Mawaziri wa Viwanda na Biashara," Amesema Prof. Kabudi
Waziri
Kabudi amesema kuwa mkutano huo utahudhuriwa na Mawaziri 16 kutoka Nchi
wanachama wa SADC za Angola, Namibia, Zambia, Zimbabwe, Comoro, Lesotho,
Mauritius, Madagascar, Kongo DRC, Shelisheli, Msumbiji, Afrika Kusini,
Tanzania, Malawi, Botswana pamoja na Eswatini)
Aidha,
Kwa mujibu wa Mhe. Waziri Kabudi, Mkutano huo utakuwa mkutano wa kwanzawa SADC
wa Baraza la Mawaziri kuendeshwa kwa lugha ya Kiswahili baada ya lugha hiyo
kuwa miongoni mwa lugha rasmi za Jumuiya hiyo.
Prof.
Kabudi aliongeza kuwa, mkutano huo utajadili masuala mbalimbali muhimu kwa
mustakabali wa maendeleo na ustawi wa nchi wananchama wa SADC.
"Mktano
huu utapokea taarifa na kutolea maelekezo taarifa za vikao mbalimbali vya
kisekta vya kamati za mawaziri ambavyo vimefanyika nchini tangu Septemba
2019," Ameongeza Prof. Kabudi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushiriikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo ktk picha) kuhusu
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC utakaofanyika tarehe 11 – 17 Machi, 2020
Jijini Dar es Salaam. Kulia mwenye kilemba ni Bibi. Zamaradi Kawawa, akifuatiwa na Naibu Katibu MKuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhani Mwinyi, kulia kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bibi. Agnes Kayola