TANZANIA YASHIRIKI KWA MARA KWANZA KATIKA
MAONESHO YA KIMATAIFA YA BIDHAA ZA KILIMO YA PARIS 2020, UFARANSA
Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza katika Maonesho ya Kimataifa ya Bidhaa
za Kilimo ya Paris 2020 yanayofanyika jijini Paris, Ufaransa kuanzia tarehe
22 Februari 2020 hadi tarehe 1 Machi 2020.
Maonesho hayo
ambayo yalifunguliwa na Mhe. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, yanatarajiwa
kutembelewa na zaidi ya watu 600,000.
Wakati wa maonesho
hayo, Tanzania itapata fursa ya kuonyesha bidhaa zake yakiwemo mazao ya
kimkakati. Ujumbe wa Tanzania katika maonyesho hayo unaongozwa na Bw. Victor
Rugemalila kutoka TANTRADE.
Ubalozi wa Tanzania
ambao unaratibu maonesho hayo kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, unaishukuru Kampuni ya Tanzania Re-assurance
(TAN-RE) ya Dar es Salaam, Tanzania, kwa kufadhili kwa kiasi kikubwa ushiriki
wa Tanzania katika maonyesho. Aidha, Ubalozi unatambua mchango wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Kampuni ya Kahawa ya Inter State.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.