Monday, February 10, 2020

DKT. NDUMBARO AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI WANAOWAKILISHA KUNDI LA UFC

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi tano (5) hapa nchini wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa.

Dkt. Ndumbaro amekutana na mabalozi hao leo katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam ambapo ujumbe huo umewahusisha, Balozi wa Italia nchini Mhe. Balozi Roberto Mengoni, Balozi wa Hispania nchini Mhe. Balozi Fransisca Pedros, Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O’Donnel, Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Balozi Ali Davutoglu, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mhe. Tae-ick Cho.


Pamoja na mambo mengine, majadiliano hayo yalijikita kujadili masuala mbalimbali yanayohusu ulinzi na usalama wa Umoja wa Mataifa.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akisalimiana na Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Balozi Ali Davutoglu wakati mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa wakati walipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akiwaeleza jambo mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa wakati walipomtembelea na kufanya nae mazungumzo leo 
Balozi wa Italia nchini Mhe. Balozi Roberto Mengoni akimueleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), wakati mabalozi hao walipomtembelea Naibu Waziri na kufanya nae mazungumzo

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb), akiwa ktk picha ya pamoja na mabalozi wanaowakilisha kundi la Uniting for Consensus (UfC) la Mageuzi ya Baraza la Usalama ya Umoja wa Mataifa 




No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.