Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge amekutana na
kufanya mazungumzo na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini
mwa Afrika (SADC).
Pamoja na mambo mengine, Katibu
Mkuu alipokea taarifa ya ziara ya Sekretarieti ya SADC na kuwahakikishia
ushirikiano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kufanikisha mikutano
yote ya SADC kipindi cha Uenyekiti wa Tanzania.
Ujumbe huo wa Sekretarieti ya SADC una wajumbe
watano ukiongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala wa SADC, Bibi. Bodo Tanrely Radaody
Ravarosy ambao wapo nchini kwa ajili ya maandalizi ya mkutano wa Mawaziri wa
Mambo ya Nje wa SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 10 - 11 Machi, 2020, Jijini
Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine, ujumbe huo ulipata fursa ya
kukutana na Katibu Mkuu Balozi Ibuge na kumpa taarifa ya maandalizi ya mkutano
huo.
Mwezi Augosti, 2019 Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli alipokea
rasmi Uenyekiti wa SADC katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wanachama.
Aidha, hatua hiyo ilifuatiwa na
mikutano mbalimbali ya kisekta iliyofanyika na inayoendelea kufanyika hapa
nchini kwa kipindi cha kuanzia mwezi Septemba 2019 hadi Agosti, 2020 ambapo
hadi sasa imeshafanyika mikutano mitatu ya kisekta.
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika picha ya
pamoja na Sekretarieti ya SADC pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.