Mabalozi Wastaafu wa Tanzania 34 walifanya ziara ya siku 2 jijini Dodoma tarehe 3 na 4 Februari 2020 kwa mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi.
Lengo la ziara hiyo lilikuwa ni kuendelea kutambua mchango mkubwa wa Mabalozi hao kwa nchi katika medani za kimataifa na masuala ya ukuzaji Diplomasia ya Uchumi kwa ujumla. Pia kuendelea kutoa uzoefu wao kwenye masuala ya Diplomasia kwa makundi mbalimbali ikiwemo Wabunge, Wanafunzi na Watumishi wa Wizara.
Wakiwa jijini Dodoma Mabalozi hao Wastaafu walipata fursa ya kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chuo Kikuu cha Dodoma na Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahriki zilizopo Mtumba.
|
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro wakati alipowakaribisha Bungeni Mabalozi Wastaafu wa Tanzania (hawapo pichani) walipotembelea Bungeni tarehe 3 Februari 2020 kwa ajili ya kujionea shughuli za Bunge. |
|
Waheshimiwa Mabalozi Wastaafu wakifuatilia vikao vya Bunge wakiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe (wa kwanza kulia) |
|
Mhe. Spika Ndugai, Mhe. Ndumbaro na Dkt. Mnyepe wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wastaafu mara baada ya kukamilisha ziara yao Bungeni hapo |
|
Balozi Mstaafu, Mhe. Getrude Mongella akizungumza na Wanafunzi wa Kozi ya Mahusiano ya Kimataifa na Diplomasia (hawapo pichani) katika Chuo Kikuu cha Dodoma wakati wa ziara ya Mabalozi Wastaafu Chuoni hapo tarehe 3 Februari 2020. Pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi Mongella aliwaasa kuzingatia uzalendo, kusoma kwa bidii na kujiongezea maarifa kwa kujifunza mambo mbalimbali yanayoendelea duniani. Pia aliwashirikisha falsafa yake ya kutokata tamaa na kujiamini kwani hakuna lisilowezekana. |
|
Sehemu ya Mabozi Wastaafu na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakimsikiliza Balozi Mongella (hayupo pichani) |
|
Picha ya pamoja kati ya Mabalozi Wastaafu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma |
|
Waheshimiwa Mabalozi Wastaafu wakipata maelezo kuhusu Mji wa Serikali kutoka kwa Bw. Meshack Bandawe, Mratibu wa Ujenzi wa Mji huo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu. Mabalozi hao walipata maelezo hayo walipotembelea Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Mtumba jijini Dodoma. |
|
Waheshimiwa Mabalozi Wastaafu wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki zilizopo Mtumba jijini Dodoma |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.