Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuchapa kazi kwa bidii na kuendelea
kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Katibu Mkuu mpya, Balozi Kanali Wilbert A.
Ibuge.
Mhe.
Prof. Kabudi ametoa rai hiyo jana jijini Dodoma wakati wa kikao na Watumishi wa
Wizara ambapo pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilitoa fursa ya kutakiana
heri ya mwaka mpya 2020 na kumkaribisha Wizarani Katibu Mkuu Mpya, Balozi
Kanali Ibuge.
Aidha, Mhe. Prof. Kabudi aliwaeleza watumishi hao kuwa, mwanzo wa mwaka ni kipindi
kizuri cha kujipanga na kuweka mikakati ya namna bora ya kutekeleza
majukumu kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
ikiwa ni pamoja na kufahamu vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya
uongozi wa wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Joseph Pombe
Magufuli.
Kadhalika
amewataka kufanya kazi kwa bidii, kujitambua na kujenga umoja na ushirikiano katika kutekeleza majukumu
hayo kikamilifu.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge ameahidi ushirikiano kwa watumishi wa
Wizara na kuwakumbusha kuwa kila mmoja ana wajibu mkubwa wa kuchangia maslahi
mapana ya Taifa ilimradi kila mmoja atekeleze wajibu wake kwa kuendelea
kujituma, kuwa tayari kurekebishwa, kuwa watiifu na kuwa tayari kupokea
maelekezo.
"Watumishi
wenzangu, kila mmoja hapa ana mchango mkubwa kwa maslahi ya Taifa letu.
Ninasisitiza kuwa mwendelee kujituma, kufanya kazi kwa weledi, kuwa watiifu,
kuwa tayari kurekebishwa na kuwa tayari kupokea maelekezo. Binafsi nitaendelea
kutoa usikivu kwenu kama ilivyokuwa kwa watangulizi wangu" alisema Balozi
Ibuge.
Kuhusu
changamoto mbalimbali zinazoikabili Wizara, Balozi Kanali Ibuge amewataka
Watumishi wote kushirikiana kuzitatua kwani hakuna changamoto ya kudumu endapo
Watumishi wote watakuwa kitu kimoja.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) akiongea na Watumishi wa Wizara wakati wa kikao kilichofanyika
jijini Dodoma
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.