Tanzania na Japan zimeahidiana
kuendeleza uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kushirikiana katika kuhakikisha maendeleo katika
sekta za biashara, uwekezaji na viwanda baina ya nchi hizo mbili.
Akihutubia sherehe ya
kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la
Japan kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Mkuu wa Itifaki Balozi Kanali Wilbert A.
Ibuge alisema kuwa Tanzania na Japan zimekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia
ambapo kutoka na uhusiano, Japan imekuwa ikisaidia ujenzi wa miradi mbalimbali
kama vile ujenzi wa miradi ya maendeleo kama vile daraja la juu lililopo eneo
la Tazara (Mfugale flyover) na mradi wa umeme wa Kinyerezi II.
"Kutokana na
Uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Japan serikali ya Japan imefadhili miradi mingine
mbalimbali hpa nchini ikiepo ujenzi wa barabara ya Iringa - Dodoma, Dodoma - Babati,
Tunduru - Namtumbo, pamoja na upanuzi wa barabara ya Bagamoyo eneo la kuanzia Morocco
hadi Mwenge," Amesema Balozi Kanali Ibuge.
Balozi Kanali Ibuge
aliongeza kuwa, mbali na sekta ya ujenzi, pia Japan imefadhili miradi
mbalimbali katika sekta muhimu nchini kama vile elimu, afya, maji na michezo.
"Serikali ya
Japan imechangia sana sula la elimu ambapo watanzania (wanafunzi) wengi
wamekuwa wakipata ufadhili wa kusomeshwa Japan mafunzo ya muda mrefu nay ale ya
muda mfupi na yamechangia kwa kiasi kikubwa ufanisi wa rasilimali watu,"
Amesema Balozi Kabudi Ibuge
Kwa upande wake,
Balozi wa Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto amesema kuwa Japan
inatambua Tanzania mara baada ya ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa umoja na
mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Japan na kusema kuwa umoja huo umekuwa
ni chachu ya maendeleo kwa Tanzania na Serikali ya Japan.
Japan imekuwa
ikifurahia uhusiano wa kirafiki na mzuri na Tanzania kwa muda mrefu sasa,
ambapo pamoja na mambo mengine Mhe. Balozi, Goto ameishukuru Serikali ya
Tanzania kwa umoja na mshikamano ambao imekuwa ikionesha kwa Japan tangu wakati
huo na kusema kuwa umoja huo umekuwa ni chachu ya maendeleo baina ya mataifa
hayo mawili.
"Urafiki wa
kiuchumi kati ya Tanzania na Japan kwa sasa ni imara, na ni matumaini yetu kuwa
katika siku za usoni uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Japan utafikia
hatua mpya ya ushirikiano," Amesema Balozi Goto.
Mkuu wa Itifaki Balozi
Kanali Wilbert A. Ibuge akiwasilisha hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mabo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati
wa sherehe ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku
ya Taifa la Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa
Japan chini Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto
Mkuu wa Itifaki Balozi
Kanali Wilbert A. Ibuge akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Japan chini
Tanzania, Mhe. Balozi Shinichi Goto
Wanakwaya wa kwaya ya
Dar es Salaam wakiimba wimbo wa Taifa wa Tanzania pamoja na wa Japan wakati wa sherehe
ya kumbukizi ya miaka 60 kuzaliwa Mfalme Naruhito wa Japan na Siku ya Taifa la
Japan iliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.