Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali
Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamaji (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw.
Charles Kwenin katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Pamoja
na mambo mengine, mazungumzo hayo yalijadili mambo mbalimbali ikiwemo maandalizi
ya Majadiliano kuhusu Uhamaji katika kanda ya Kusini mwa Afrika yanayotarajia
kufanyika chini ya uenyekiti wa Tanzania kama Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).
Majadiliano
hayo yanatarajiwa kufanyika kabla ya mwezi Agosti, mwaka 2020 hapa nchini yakiwa
na dhamira ya kujadili usimamizi wa masuala ya uhamiaji ili kuwezesha uundwaji
wa sera zenye uwiano miongoni mwa nchi wanachama wa SADC.
Aidha,
Balozi Ibuge amewahakikishia wajumbe wa IOM, utayari wa Tanzania kuwa nchi
mwenyeji wa Majadiliano hayo.
Mkurugenzi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Uhamaji (IOM), kanda ya Kusini
mwa Afrika Bw. Charles Kwenin akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge leo katika
Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali
Wilbert A. Ibuge akiwaelezea jambo Mkurugenzi wa Shirika la (IOM), kanda ya Kusini mwa Afrika Bw. Charles Kwenin akiongea
pamoja na Mwakilishi wa IOM hapa nchini Dkt. Qasim Sufi leo katika Ofisi ndogo
za Wizara Jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.