Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali
Wilbert A. Ibuge, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kuwait nchini
Tanzania Mhe. Balozi Mubarak Mohammed Alsehaijan katika Ofisi ndogo za Wizara
Jijini Dar es Salaam
Pamoja
na mambo mengine, mazungumzo hayo yalijadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha
uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Kuwait kupitia Nyanja mbalimbali
ikiwemo uwekezaji wa miradi na biashara pamoja na uundwaji wa tume ya kudumu ya
pamoja ya ushirikiano.
Aidha,
Mhe. Balozi Alsehaijan alitumia fursa hiyo kumkabidhi Katibu Mkuu, Balozi Ibuge
salamu za rambirambi kufuatia ajali zilizotokea hapa nchini hivi karibuni.
Kwa
upande wake Balozi Ibuge, alimweleza Mhe. Balozi Alsehaijan umuhimu wa
kuendeleza jiji la Dodoma na kumkaribisha jijini Dodoma.
Mazungumzo
hayo yamefanyika siku moja baada ya Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania
kusheherejea 59 ya Uhuru wake na miaka 29 ya ukombozi wa taifa hilo
yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.