Friday, October 2, 2020

Mradi wa Umeme wa Pamoja wa Tanzania, Burundi, Rwanda Wafikia Pazuri


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge akipokelewa na Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Mutukula, alipowasili kwenye kituo hicho kujionea shughuli zinavyoendelea.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge akikagua ubora wa mashine ya kukagulia mizigo iliyofungwa katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja cha Mutukula.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge akiongea na mmoja wa wafanyakazi wa Kituo cha Hudum kw Pamoja Mpakani cha Mutukula.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge akisaini kitabu cha kabla ya kuanza kikao na watumishi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Mutukula.


Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Kamugisha Kazaura akitoa maelezo namna EAC inavyoratibu upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kikanda. 




Ujenzi wa Mtambo wa Kuzalisha Umeme katika Mto Kagera

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge  akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye eneo unapojengwa Mtambo wa Kuzalisha Umeme katika Mto Kagera.


Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Mhe. Dkt. Jilly Maleko akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye eneo unapojengwa Mtambo wa Kuzalisha Umeme katika Mto Kagera.

 Mhandisi wa Kampuni inayojenga Mtambo wa kuzalisha umeme katika Mto Kagera akitoa maelezo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa mtambo huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge akiuliza maswali kwa wahandisi wanaojenga mradi wa kuzalisha umeme katika Mto Kagera.

Sehemu ya Eneo unapojengwa Mtambo wa Kuzalisha Umeme katika Mto Kagera.

OSBP ya Rusumo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge akisalimiana na watumishi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo, mara baada ya kuwasili kituoni hapo kwa ziara ya kikazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge akiongea na Mtalaam wa Afya katika Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo.

Mkuu wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo, Bw. Jackson Mushi akitoa taarifa ya utekelezaji wa kituo hicho kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  IbugeA


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge akiongea na watumishi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo

Watumishi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge.

Mkurugenzi wa Miundombinu kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Kamugisha Kazaura na Msaidizi wa Katibu Mkuu, Bw. Hangi Mgaka wakitabasamu akati wa kikao cha briefing kwenye Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge, Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dkt. Jilly Maleko, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhandisi Steven Mlote pamoja na ujumbe wao akitemb kwa miguu kuelekea katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo.

Malori yakiwa katika foleni ya ukaguzi katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo.

Bango la kutoa elimu kuhusu wafanyabiashara wadogo wanavyoweza kufanya shughuli zao katika nchi a EAC bila usumbufu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert  Ibuge na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Kituo cha Huduma kwa Pamoja Mpakani cha Rusumo.


 





Wednesday, September 30, 2020

AfDB Yamwaga Neema Kigoma




Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge akisalimiana na watumishi wanaofanya kazi katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Kabanga kwenye Mpaka wa Tanzania na Burundi. alipowasili katika kituo hicho kwa ziara ya kikazi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge akiongea na wasafiri wanaokwenda Burundi na Uganda wanaosubiri taratibu za uhamiaji katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Kabanga
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge akiongea na Afisa Uhamiaji katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Kabanga kwenye Mpaka wa Tanzania na Burundi.
Kaimu Meneja wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Kabanga akisoma taarifa kuhusu utendaji wa Kituo hicho.
Ujumbe uliongozana na Balozi Ibuge wakisaini Kitabu cha Wageni katika Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Kabanga kwenye Mpaka wa Tanzania na Burundi.


Malori yakiwa katika foleni ya kusubiri ukaguzi kutoka maafisa wa Burundi ili yaendelee na safari.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge na ujumbe wake wakiwa mpakani mwa Tanzania na Burundi kwenye eneo la Kabanga.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na  watumishi wa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Kabanga kwenye Mpaka wa Tanzania na Burundi.





Tuesday, September 29, 2020

SERIKALI YAONGEZA KASI UTEKELEZAJI WA AHADI ZA MHESHIMIWA RAIS MAGUFULI KWA WANANCHI WA KIGOMA






Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna wa Polisi Thobias Andeng'enye alipowasili katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kujitambulisha kabla hajaanza ziara ya ukaguzi wa miradi ya miundombinu inayoratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma, Bw. Rashidi Kassim alipowasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kwa ajili ya kujitambulisha, kabla hajaanza ziara ya kukagua miradi ya miundombinu inayoratibiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kamishna wa Polisi Thobias Andeng'enye akiwa katika kikao cha kupeana taarifa kuhusu mkoa huo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mhe. Kanali Michael Ngayalina kwenye Mpaka wa Tanzania na Burundi, Eneo la Manyovu ambapo kutajengwa Kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani (OSBP). 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mhe. Kanali Michael Ngayalina pamoja na ujumbe wao wakikagua Eneo litakalojengwa kituo cha Kutoa Huduma kwa Pamoja Mpakani mwa Tanzania na Burundi katika miji ya Manyovu/Mugina.

Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Mhe. Kanali Michael Ngayalina akimuonesha jiwe linalotenganisha Mpaka wa Tanzania na Burundi lililopo kwenye Mji wa Manyovu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge akimsikiliza Mshauri Mwelekezi wa ujenzi wa mradi wa Barabara kutoka Kasulu hadi Kibondo ambao unajengwa na Mkandarasi kutoka China kwa fedha za mkopo nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika.

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Mipango na Miundombinu, Mhandisi Steven Mlote (Kulia) akiwasikiliza wakandarasi kutoka China wanaojenga barabara inayounganisha Tanzania na Burundi kutoka Kasulu hadi Kibondo.

Bi. Edna Chuku akibadilishana mawzo na Mhandisi wa TANROADS wa Mkoa wa Kigoma walipokuwa kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brig. Gen. Wilbert A. Ibuge akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta iliyopo mkoani Kigoma. Sehemu ya Kambi hiyo itapitiwa na barabara inayounganisha Tanzania na Burundi.

 












Wednesday, September 23, 2020

SERIKALI YAELEZA SABABU ZA VYOMBO VYA HABARI VYA KIMATAIFA KUSAJILIWA

Serikali imefafanua hatua yake ya kuvitaka vyombo vya habari vya Kimataifa vinavyotaka kuvitumia vyombo vya habari vya Tanzania kurusha matangazo yake yana lengo la kutambua vyombo hivyo vinashirikiana vyombo gani vya hapa nchini na sio kuvizuia kutangaza na kuendesha vipindi vyake hapa nchini kama inavyoripotiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Dkt. David Concar na kufafanua kuwa mpaka sasa vyombo vyote vya habari vya Kimataifa zimekwishatekeleza matakwa hayo ya kisheria na kupata leseni ya kutangaza na kuendesha vipindi vyao.

"Leo nimekutana na Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini Dkt. David Concar na kumueleza lengo la kusajili vyombo vya Habari vya kimataifa lilikuwa ni kutaka kujua ni chombo gani cha kimataifa kinashirikiana na chombo gana hapa nchini lakini pia ilikuwa ni matakwa ya kisheria,"  Amesema Prof. Kabudi 

Kuhusu suala la mabadiliko ya sheria za asasi za kiraia (NGOs) na vyama vya siasa Prof. kabudi amefafanua kuwa lengo lake lilikuwa ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika fedha zinazoingia kwa asasi hizo pamoja na matumizi yake na kuwa linaendana na sheria na taratibu za kimataifa za kuzuia utakatishaji wa fedha na kuhakikisha makundi yenye nia ovu na misimamo mikali inayokwenda kinyume na tunu za demokrasia hayatumii njia hizo kupenyeza fedha zao.

Balozi mteule wa Uingereza  Dkt. David Concar amesema mazungumzo yao mbali na kulenga masuala ya kidiplomasia na maendeleo pia yalilenga kuangalia namna ya kuondoa malalamiko kutoka kwa baadhi ya NGOs na vyombo vya habari vya kimataifa kuhusu kile kinachodaiwa kuwa ni uminywaji wa haki ya uhuru wa vyombo vya habari.  

Katika tukio jingine pia Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Prof. Palamagamba John Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark hapa nchini Balozi Mette Norgaard ambapo mbali na suala la uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octoba 28 hapa nchini,wamejadili pia masuala yanayohusu mashirikiano katika sekta za elimu, afya, biashara na uwekezaji.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akimkabidhi Balozi mteule wa Uingereza nchini, Dkt. David Concar nakala za sheria ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi  


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi akimuonesha Balozi mteule wa Uingereza hapa nchini, Dkt. David Concar namna magazeti yanavyo ripoti habari za uchaguzi mkuu bila upendeleo  


Balozi wa Denmark nchini Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Kabudi  


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akimuelezea jambo Balozi wa Denmark nchini Mhe. Mette Norgaard Dissing-Spandet akimueleza jambo wakati walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam




Monday, September 21, 2020

TANZANIA IMETAJWA KAMA NCHI YA KIELELEZO CHA AMANI NA DEMOKRASIA KATIKA BARA LA AFRIKA

Norway yaitaja Tanzania kama kielelezo cha amani na demokrasia katika chaguzi Barani Afrika kutokana na mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu unavyofanyika kwa amani,utulivu na usawa kwa wagombea wa vyama vyote huku wananchi wakijitokeza kwa wingi kusikiliza sera za wagombea.

Balozi wa Norway nchini Tanzania Balozi Elisabeth Jacobsen ameyasema hayo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa maandalizi ya uchaguzi mkuu yamefanyika kwa kufuata taratibu za kisheria huku tume ya Taifa ya Uchaguzi ikishughulikia baadhi ya malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya vyama vya siasa na wadau mbalimbali jambo ambalo linaifanya Tanzania kuwa kinara wa demokrasia katika mchakato mzima wa uchaguzi. 

Pamoja na masuala ya kisiasa Balozi huyo amesema katika mazungumzo yao wamegusia pia masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi hususani katika suala la elimu,afya,nishati na uwekezaji pamoja na biashara baina ya nchi hizo mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amemuomba Balozi huyo wa Norway kuendelea kushirikiana na Tanzania na kumshukuru kwa Nchi hiyo kukubali kutoa kiasi cha dola za marekani milioni 7 kwa ajili ya mradi wa TASAF jambo litakalosaidia kupunguza umasikini kwa watanzania hususani katika kipindi hiki ambapo nchi nyingi zimeathiriwa na janga la Corona. 

Mbali na Balozi huyo wa Norway pia Prof. Kabudi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden hapa nchini Balozi Anders Sjöberg ambapo amezungumzia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi,haki za binadamu na uhuru wa vyombo vya habari na kuvipongeza vyombo vya habari hapa nchini kwa kuandika habari za wagombea wa vyama vyote bila ya ubaguzi na ameonesha kufurahishwa kwake na mwitikio wa wananchi katika mikutano ya kampeni na kuomba maamuzi ya wananchi katika sanduku la kura yaheshimiwe.

Kuhusu suala la haki za binadamu prof. Kabudi amesema taswira inayotolewa kuhusu suala hilo haiakisi hali halisi iliyopo nchini na kwamba Tanzania inaheshimu na kulinda misingi ya haki za binadamu kiasi cha suala hilo kuingizwa katika ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ili kikiingia madarakani kitekeleze na kulinda misingi hiyo. 

Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amepokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Uswis hapa Nchini Mhe. Didier Chassot.


Balozi wa Sweden nchini Mhe. Anders Sjöberg akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi wakati alipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Kabudi akimuonesha Balozi Sweden nchini, Mhe. Anders Sjöberg moja ya vipengele vilivyopo kwenye sheria ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Kabudi akimuonesha Balozi Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen moja ya kipengele cha sheria ya uchaguzi na kanuni za uchaguzi wakati alipokuwa akimkabidhi nakala ya nyaraka hizo



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Kabudi akikagua nakala za hati za utambulisho za Balozi mteule wa Uswisi hapa nchini Mhe. Didier Chassot 



Friday, September 18, 2020

TANZANIA YAKABIDHIWA HATI MILIKI YA ARDHI NA SERIKALI YA INDIA

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akiweka saini hati miliki ya ardhi ya jengo la Ubalozi, jijini New Delhi tarehe 17 Septemba 2020.

Naibu Afisa Mkuu wa Ardhi wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Miji ya India, Bw. Satish Kumar Singh akimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda hati miliki ya ardhi ya jengo la Ubalozi, jijini New Delhi tarehe 17 Septemba 2020.

Picha ya jengo la Ubalozi wa Tanzania Jijini New Delhi, India.
=========================================

TANZANIA YAKABIDHIWA HATI MILIKI YA ARDHI MJINI NEW DELHI.

Ubalozi wa Tanzania nchini India umekabidhiwa rasmi na Serikali ya India Hati Miliki ya Ardhi yenye ukubwa wa eneo la mita za mraba 2120.60 ambapo ndipo lilipo jengo la Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania jijini New Delhi.

Akipokea hati hizo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji ya India tarehe 17 Septemba 2020, Balozi wa Tanzania nchini humo, Mhe. Baraka H. Luvanda ameishukuru Serikali ya India kwa hatua hiyo ambayo inathibitisha uhusiano mzuri uliojengeka kati ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake, Naibu Afisa Mkuu wa Ardhi wa Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Miji ya India, Bw. Satish Kumar Singh amesifu uhusiano mzuri wa kihistoria uliopo kati ya India na Tanzania na kueleza kuwa, hiyo ndiyo sababu India imeona fahari kubwa kuipa Tanzania umiliki wa eneo katika sehemu mahsusi ya Jumuiya ya Kidiplomasia (Diplomatic Enclave).

Ni sera na mkakati wa Serikali ya Tanzania ya kuhakikisha kuwa, Balozi zote zilizopo katika maeneo ya kimkakati zinakuwa na majengo na nyumba za watumishi ili kuipunguzia Serikali gharama kubwa za kupanga majengo na nyumba hizo. Katika hafla hiyo Balozi Luvanda aliambatana na maofisa ubalozi, Bibi Natihaika Msuya na Dkt. Kheri Goloka.