Umoja
wa Afrika (AU) umezitaka nchi wanachama wa umoja huo kutilia mkazo azimio la kuondoa
na kutokomeza silaha haramu ili kuliondoka na migogoro inayolifanya bara hilo
kushindwa kusonga mbele kiuchumi.
Akifungua
Mkutano wa 14 wa dharura wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia ya mtandao
(virtual Conference) Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya
Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa amesema ni vigumu Bara la Afrika kupiga
hatua za kimaendeleo kiuchumi endapo suala la usalama halitapewa kipaumbele na
kuruhusu migogoro kuendelea.
Rais,
Ramaphosa ameongeza kuwa wakati umefika kwa nchi za afrika hususani zilizopo
katika migogoro na vita kuhakikisha kuwa zinatatua vyanzo vya machafuko hayo na
kuboresha hali ya kiuchumi kwa wananchi, utawala wa sheria, na kuzingatia misingi
ya haki na utawala bora.
Akimwakilisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Meh. John Pombe Joseph Magufuli katika
mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof.
Palamagamba Kabudi amesema mkutano huo ulikuwa unajadili mpango na mkakati wa
miaka 10 iliyopita wa kuondoa na kutokomeza silaha haramu na kujenga amani
katika bara la Afrika.
"Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania imeunga mkono azimio la nchi za AU kuongeza miaka
mingine 10 ya kutokomeza silaha haramu na kusisitiza tena ushiriki wake
kikamilifu katika kuhakikisha kuwa Afrika inatatua migogoro yake yote yenyewe
bila kuingiliwa na nchi za nje, lakini pia kuzitaka nchi za Afrika kuzuia
mitafaruku na migogoro yote ambayo kwa miaka mingi imeigharimu sana bara la
Afrika," Amesema Prof. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa, toka hatua ya kuondoa na kutokomeza silaha haramu
ilipoanza mwaka 2017 hadi 2019, silaha zaidi ya 1,233 zimerejeshwa na Serikali
itaendelea na jitihada ya kuhakikisha kuwa inazitambua silaha zote.
Aidha,
Prof. Kabudi ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zote ili
kuwa na amani endelevu na utulivu endelevu katika eneo lote la Maziwa Makuu,
pia Serikali ya Tanzania itaendelea kutoa mchango wake katika nchi mbalimbali
zenye mapigano ikiwemo DRC halikadhalika katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na
sehemu nyingine ambapo vikosi vyake vya kijeshi vitatumwa kulinda amani.
Nae
Rais wa Ghana, Mhe. Nana Akufo-Addo amesema kuwa Ghana inaungana na Umoja wa
Afrika (AU) na itaendelea kuhakikisha inaondoa na kutokomeza silaha haramu kwa
lengo la kuimarisha masuala ya Amani, umoja na ushirikiano wa nchi za AU.
"Ghana
tangu mwaka 2014 tulishaanza mkakati wa kuzuia na kutokomeza matumizi holela silaha
haramu kwa kuzihakiki na kuandikisha wamiliki wote wanaomiliki silaha,….….pia
mwaka jana 2019 kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) tumeweza
kuendelea kudhibiti silaha matumizi ya silaha holela," Amesema Rais Akufo-Addo
Nae
Rais wa Somalia, Mhe. Mohamed Farmajo amesema kuwa suala la Amani na usalama ni
suala muhimu sana kwenye jamii hivyo Somalia inaungana na Umoja wa Afrika
katika kuhakikisha kuwa wanaondoa na kutokomeza silaha haramu na kujenga amani
katika bara la Afrika.
Rais
Mohammed ameongeza kuwa amani na usalama vitakumbukwa kuwa ni msingi wa
maendeleo kwenye katika jamii. Aidha, Rais huyo ameuomba umoja wa Afrika
kushirikiana kwa karibu na Somalia katika kuhakikisha kuwa wanatokomeza vikundi
vya kigaidi (Alshabab) kwa maendeleo ya ukanda wa Afrika.
Pamoja
na mambo mengine, Umoja wa Afrika umekubaliana kuongeza muda wa kuondoa na
kutokomeza silaha haramu na kujenga amani katika bara la Afrika kwa kipindi cha
miaka 10 ijayo kuanzia mwaka 2021 hadi 2030.
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akichangia
moja ya agenda katika mkutano wa 14 wa dharua Umoja wa Afrika uliofanyika kwa
njia ya mtandao (virtual Conference) jijini Dar es Salaam |
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi akiwa
pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji
Mnyepe pamoja na washiriki wengine wakifuatilia mkutano wa 14 wa dharua Umoja
wa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao (virtual Conference)