Friday, May 7, 2021

MAWAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI WA EAC WAKUBALIANA KUBORESHA TUME YA KISWAHILI

Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Mashauriano ya Kibajeti umefanyika jijini Arusha leo tarehe 7 Mei 2021 huku Mawaziri hao wakikubaliana na hoja ya kuiboresha Tume ya Kiswahili ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi badala ya kuivunja.

 

Awali hoja ya kuivunja Tume ya Kiswahili ambayo ni moja ya Taasisi za Jumuiya iliwasilishwa kupitia ripoti ya mshauri mwelekezi na kuungwa mkono na takriban Nchi zote Wanachama isipokuwa Tanzania  kama moja ya mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji ndani ya Jumuiya. Hata hivyo,nchi hizo ziliafiki kwa kauli moja hoja zilizolizotolewa na Tanzania kuhusu umuhimu wa Tume hiyo.

 

Akizungumza kwenye mkutano huo, Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba alieleza umuhimu wa Tume hiyo na kwamba ni kielelezo pekee muhimu cha Jumuiya na kuwataka kuunga mkono hoja ya kuiboresha na kuiimarisha ili iendelee kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

 

“Hoja ya kuvunja Tume ya Kiswahili kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji wa Jumuiya inalenga kudidimiza malengo na misingi iliyopo ya kuiunganisha jumuiya. Hivyo nasisitiza kuwa bado upo umuhimu mkubwa wa kuienzi Tume hiyo ambayo ni kielelezo muhimu cha Jumuiya  badala ya kufikiria kuivunja” alisema Mhe. Nchemba.

 

Awali, akifungua mkutano huo, Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Fedha wa Kenya, Mhe. Ukur Yatani Kanacho,  alisema ana matarajio makubwa mkutano huo utafanyika kwa mafanikio na kutoa pole kwa niaba ya Mawaziri walioshiriki Mkutano huo kwa Ujumbe wa Tanzania na Serikali kwa ujumla kwa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli. Pia alitoa pole kwa Nchi Wanachama kufuatia janga la ugonjwa wa Corona na kuwataka wajumbe kuendelea kushirikiana kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

 

Mkutano huo pamoja na mambo mengine umepokea na kujadili agenda mbambali zilizowasilishwa ikiwemo taarifa za Kamati zinazoshughulikia masuala ya Fedha ikiwemo ile ya Makamishna Wakuu wa Mamlaka za Mapato za Nchi Wanachama pamoja  na taarifa ya Utafiti wa kuboresha Mifumo na Miundo ya Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na rasilimali zilizopo.

 

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano huo umewahusisha pia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga, Waziri, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali,   Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina HK. Shaaban na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.

 

Mkutano huo ambao umeitishwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, ulitanguliwa na kikao cha Ngazi ya Wataalam kutoka Sekta za Fedha na Uchumi uliofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Mei 2021 na kufuatiwa na kikao cha Makatibu Wakuu kilichofanyika tarehe 6 Mei 2021.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 7 Mei 2021. Mkutano huo ulitanguliwa na vikao vya Wataalam  na Makatibu Wakuu vilivyofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 6 Mei 2021. Kulia ni Waziri, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Jamal Kassim Ali na kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga akichangia jambo wakati wa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kushoto ni Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina HK. Shaaban
Ujumbe wa Burundi ukiongozwa na Mhe. Balozi Ezechiel Nibigira (katikati) wakishiriki Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wajumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Mhe. Waziri Nchemba kwa pamoja na Mawaziri kutoka Zanzibar wakifuatilia Mkutano. Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uwekezaji, Uchumi na Ajira Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga

Mhe. Balozi Nibigira kutoka Burundi akichangia jambo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji wa Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na Kamishna Msaidizi, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. James Msina

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elias Bagumhe akiwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ujumbe wa Tanzania

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania

Mkutano ukiendelea

Wajumbe wakifuatilia mkutano

Mkutano ukiendelea

WAZIRI MULAMULA AKUTANA NA MABOLOZI WANNE, KUPOKEA NAKALA YA HATI YA UTAMBULISHO

 Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kuzungumza na mabalozi wanne wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na kupokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji hapa nchini.

Mabalozi waliokutana na Waziri katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Rwanda, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba, Balozi wa Indonesia Mhe. Ratlan Pardede, Balozi wa Sweden Mhe. Anders Sjöberg na Balozi wa Norway Mhe. Elisabeth Jacobsen.

Pamoja na mambo mengine, Mhe. Waziri Mulamula na mabalozi hao wamejadili juu ya kuimarisha na kuongeza ushirikiano baina ya mataifa wanayoyawakilisha hapa nchini na Tanzania.    

 “Leo nimekutana na mabalozi kadhaa wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, akiwemo Balozi wa Rwanda, Sweden, Norway na pia nimepokea nakala ya hati ya utambulisho ya balozi mteule wa Msumbiji na kuwahakikishia ushirikiano wetu kama wizara, kama nchi katika kuboresha na kukuza mahusiano yetu,” amesema Balozi Mulamula

Nae Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba amesema kuwa ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda ni mzuri hivyo wataendelea kuudumisha uhusiano huo kwa maslahi ya pande zote mbili.

“Nchi zetu mbili zimekuwa zikishirikiana vizuri hivyo tumekubaliana kuendelea kudumisha ushirikiano huu kwani Watanzania na Wanyarwanda ndugu na marafiki,” amesema Balozi Karamba

Kwa upande wake Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Ratlan Pardede amesema Indonesia na Tanzania zitaendelea kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo uchumi, utalii na kijamii na kuhakikisha kuwa ushirikiano huo unazidi kuimarika.

“Tumejaribu kuwahamasisha wawekezaji kutoka Indonesia kuja kuwekeza hapa Tanzania na hadi sasa kampuni kumi (10) zimewekeza katika sekta za biashara na uwekezaji, madini, uvuvi, ujenzi na viwanda,” amesema Balozi Pardede     

Nae Balozi wa Sweden Mhe. Anders Sjöberg amesema kuwa Sweden itaendelea kuimarisha mahusiano na ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari pamoja na haki za binadamu.

“Tumejadiliana kuhusu kuimarisha mahusiano, biashara na uwekezaji, utunzaji wa mazingira pamoja na masuala ya kijamii kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu,” amesema Balozi Sjöberg.

Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen amesema Norway na Tanzania zimekuwa na uhusiano mzuri ambapo kwa sasa Norway inaangalia fursa za uwekezaji na biashara hapa nchini ili kuimarisha mahusiano na kukuza uchumi.

“Norway itaendelea kutumia fursa za uwekezaji na biashara zilizopo Tanzania ili kuimarisha mahusiano yetu na kukuza uchumi wa pande zote mbili,” amesema Balozi Jacobsen

Katika tukio jingine, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amepokea nakala ya hati ya utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Ricardo Ambrosio Sampaio Mtumbuida.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Rwanda hapa nchini, Mhe. Meja Jenerali Charles Karamba katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kulia ni baadhi ya Wakurugenzi na Afisa kutoka Wizarani 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo na Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Ratlan Pardede katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) na Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Ratlan Pardede yakiendelea 


Balozi wa Sweden nchini, Mhe. Anders Sjöberg akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula wakati balozi huyo alipomtembelea Mhe. Waziri ofisini kwake Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza na Balozi wa Norway nchini Mhe. Elisabeth Jacobsen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Bw. Hassan Mwaweta pamoja na Afisa Dawati Bibi. Tunsume Mwangolombe

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akipokea nakala ya hati ya utambulisho ya Balozi Mteule wa Msumbiji hapa nchini Mhe. Ricardo Ambrosio Sampaio Mtumbuida katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

 



Thursday, May 6, 2021

KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA SEKTA YA FEDHA NA UCHUMI WA EAC CHAFANYIKA ARUSHA

Kikao cha Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kimefanyika Arusha tarehe 6 Mei 2021.


Kikao hicho kimefanyika kwa lengo la kukamilisha agenda mbalimbali za msingi zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Mashauriano ya Kibajeti unaotarajiwa kufanyika  tarehe 7 Mei 2021.


Miongoni mwa Agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi ni  pamoja na Taarifa ya Utafiti wa Kuboresha Mfumo na Muundo wa Uendeshaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kulingana na Rasilimali zilizopo pamoja na kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Maazimio mbalimbali yaliyofikiwa wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza hilo la Kisekta.

 

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaongozwa na Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, Zanzibar na kuhudhuriwa pia na Bi. Amina KH. Shaaban, Naibu Katibu Mkuu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango.


 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,  Fedha na Mipango, Zanzibar, Mhe. Dkt. Juma Malik Akil akizungumza kama kiongozi wa ujumbe wa Tanzania wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wanaoshughulikia Sekta ya Fedha na Uchumi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika jijini Arusha tarehe 6 Mei 2021 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi unaotarajiwa kufanyika jijini humo tarehe 7 Mei 2021. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina KH. Shaaban.

Ujumbe wa Burundi ukiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu wanaoandaa Mkutano wa 12 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na uchumi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ujumbe wa Uganda nao ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukishiriki kikao cha Makatibu Wakuu

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania ukiwa kwenye kikao cha Makatibu Wakuu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na Kamishna Msaidizi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. James Msina

Kamishna wa Uchambuzi wa Sera kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. William Mhoja (kulia) akiwa na Kamishna wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bw. Said Athumni wakati wa kikao cha Makatibu Wakuu wa Sekta ya Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

Ujumbe wa Tanzania kwenye kikao cha Makatibu Wakuu

Kikao kikiendelea

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania

Ujumbe wa Tanzania

Wajumbe wakifuatilia kikao

Kikao kikiendelea

BALOZI SIMBACHAWENE AIPONGEZA TIMU ILIYOFANIKISHA ZIARA YA MHE. RAIS KENYA

 

Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene akizungumza na watendaji na wataalamu kutoka Tanzania waliokuwa nchini Kenya kwa ajili ya kuhakikisha ziara ya Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan nchini Kenya inafanyika kwa mafanikio


Watendaji na wataalamu kutoka Tanzania ambao walikuwa nchini Kenya kwa ajili ya kufanikisha ziara ya Mhe. Rais alipoitembelea Kenya tarehe 4-5 Mei 2021 wakiwa katika ukumbi wa mikutano katika Ubalozi wa Tanzania  jijini Nairobi.


Baadhi ya watendaji na wataalamu kutoka Tanzania wakizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Simbachawene katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi.  


Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Simbachawene akiwa na Mkurugenzi wa TanTrade Bw. Edwin Rutagaruka na Mkurugenzi wa idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikian wa Afrika MasharikiBw. Frank Mwega katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Simbachawene (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)  Bw. Maduhu Kazi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili kushoto) walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa Mhe. Balozi jijini Nairobi.



Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)  Bw. Maduhu Kazi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) Bw. (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Frank Mwega na maafisa Ubalozi walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa Mhe. Balozi jijini Nairobi.


Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt John Steven Simbachawene (katikati) akiwa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)  Bw. Maduhu Kazi (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Mauzo ya Nje (EPZA) Bw. (wa kwanza kulia), Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bw. Edwin Rutageruka (wa pili kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Shirka la Viwango Tanzania (TBS) Dkt. Yusuf Mngenya (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Frank Mwega na maafisa Ubalozi walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwa Mhe. Balozi jijini Nairobi.


Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene katika picha ya pamoja na watendaji kutoka Tanzania  waliofanikisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Kenya tarehe 4-5 Mei 2021.




Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Dkt. John Simbachawene ameipongeza timu ya watendaji na wataalamu kutoka Tanzania  kwa kufanikisha ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyoifanya nchini Kenya tarehe 4-5 Mei 2021.

Dkt. Simbachawene ametoa pongezi hizo katika Ubalozi wa Tanzania jijini Nairobi alipokutana na timu ya watendaji na wataalamu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Viwanda na Biashara.

“Nawashukuru na kuwapongeza kwa kazi kubwa na nzuri mliyoifanya hadi kukamilika kwa ziara ya Mhe. Rais, ni wazi kuwa kufanya kazi kwa pamoja ni kitu kizuri wote tumeona hapa, asanteni sana na hongereni kwa kazi,” alisema Dkt. Simbachawene.

Amewataka watendaji hao kuhakikisha wanazingatia na kutekeleza yale yote yaliyoongelewa na kutolewa maelekezo na viongozi wakuu wa nchi hizi ili kuhakikisha vikwazo vya biashara visivyo vya kodi vinaondolewa na hvyo kukuza na kuimarisha uwekezaji na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta. Ziara hiyo ilifanyika tarehe 4-5 Mei 2021 na kushuhudia makubaliano kati ya Tanzania na Kenya kuhusu kushirikiana kwenye masuala ya utamaduni na ujenzi wa bomba la gesi asilia kutoka Dar es Salaam hadi Mombasa yakisainiwa kwa ajili ya utekelezaji

Katika ziara hiyo Viongozi wa nchi hizo walikubaliana kuondoa vikwazo vya biashara vilivyopo baina ya nchi hizo vinavyozuia uwekezaji na biashara katika nchi hizo na hivyo kushindwa kukuza uchumi wa nchi hizo .


RAIS SAMIA NA UJUMBE WAKE WAREJEA NYUMBANI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe, Uhuru Kenyatta wakati akielekea kupanda Ndege kurejea nchini mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili  nchini Kenya tarehe 05 Mei, 2021.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe, Uhuru Kenyatta wakati akielekea kupanda Ndege kurejea nchini mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili  nchini Kenya tarehe 05 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akimshukuru Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta alipomsindikiza mara

baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili nchini Kenya tarehe 05 Mei, 2021. PICHA NA IKULU

Wednesday, May 5, 2021

RAIS SAMIA AHUTUBIA MABUNGE YA KENYA

Wabunge wa Mabunge Mawili ya Kenya (Bunge la Taifa pamoja na Bunge la Senate la Kenya) wakiwa tayari kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan aliyekwenda kuwahutubia wabunge hao Jijini Nairobi tarehe 05, Mei, 2021 wakati ya ziara yake rasmi nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Mabunge ya Kenya Jijini Nairobi tarehe 05, Mei, 2021 wakati ya ziara yake rasmi ya siku mbili nchini Kenya.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Mabunge ya Kenya Jijini Nairobi tarehe 05, Mei, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Mabunge ya Kenya Jijini Nairobi tarehe 05, Mei, 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amehutubia Mabunge Mawili ya Kenya (Bunge la Taifa pamoja na Bunge la Senate la Kenya) Jijini Nairobi tarehe 05, Mei, 2021.

Akiwahutubia wabunge hao wa Mabunge hayo ya Kenya Mhe. Rais Samia amewataka kuendeleza udugu wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Kenya.

Amesema Tanzania na Kenya ni ndugu wa siku nyingi udugu ambaoo utaendelea kuwepo siku zote na ndio maana hata wanyama aina ya nyumbu huishi kwa kuhama kati ya Kenya na Tanzania kama mzunguko wa maisha yao

Mhe. Rais Samia alikuwa nchini Kenya kwa ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru. Kenyatta.

Mhe. Rais na ujumbe wake wamerejea nchini joini ya tarehe 05/05/2021 baada ya kukamilika kwa ziara hiyo.