Friday, June 11, 2021

RAIS WA JAMHURI YA BOTSWANA MHE. DKT. MASISI ATEMBELEA KIWANDA CHA KUSAGA NAFAKA CHA AZAM


Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa mmoja wa Watendaji wa kiwanda cha Azam alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam, ili kujionea uwekezaji unaofanywa na Wawekezaji binafsi wa Kitanzania. Katika ziara hiyo Mheshimiwa Dkt. Masisi aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb).
Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi  akiwa ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakilakiwa na baadhi ya Watendaji wa Kiwanda cha kusaga nafaka cha Azam waliopowasili kiwandani hapo kwa lengo la kujionea uwekezaji unaofanywa na Wawekezaji binafsi wa Kitanzania.

Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi  na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakiwasili katika kiwanda cha Azam kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi akizungumza na baadhi ya Watendaji (hawapo pichani) wa Kiwanda cha Azam
Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mheshimiwa Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi  ameondoka nchini leo Juni 11, 2021 baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili.


Thursday, June 10, 2021

MAKATIBU WAKUU KUTOKA NCHI ZA EAC WANAOSHUGHULIKIA MIPANGO NA MASUALA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA ARUSHA

Mkutano wa Makatibu Wakuu wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika jijini Arusha tarehe 10 Juni 2021.


Mkutano huo ambao ulitanguliwa na Mkutano kwa Ngazi ya Wataalam uliofanyika tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 jijini hapa, pamoja na mambo mengine umekamilisha agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika tarehe 11 Juni 2021.


Miongoni mwa agenda zitakazowasilishwa kwa Mawaziri ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la kujiunga na EAC; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa ya utatu wa Jumuiya za EAC-COMESA-SADC katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika na Taarifa ya Uchangiaji wa Bajeti ya EAC kutoka Nchi Wanachama.


Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Makatibu Wakuu umeongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome. Viongozi wengine walioshiriki Mkutano huo ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali na   Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. 

Mwenyekiti wa Mkutano wa Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Kenya, Mhe. Dkt. Kevit Desai (kushoto) akiongoza Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha tarehe 10 Juni 2021 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021. Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili na kupitisha agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa Mawaziri.

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome (kulia) akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Dodoma tarehe 10 Juni 2021 kwa ajili ya kukamilisha maandalizi ya Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021. Kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa Makatibu Wakuu. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Zanzibar, Bw. Mussa Haji Ali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Prof. Abel Makubi na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi

Sehemu ya ujumbe wa Kenya ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

Sehemu ya ujumbe wa Uganda ukishiriki Mkutano wa MakatibuWakuu

Sehemu ya ujumbe wa Rwanda ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

Sehemu ya ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Sudan Kusini

Prof. Mchome akiwa amesaini Ripoti ya Makatibu Wakuu itakayowasilishwa kwa Mawaziri

Mjumbe kutoka Sudan Kusini naye akisaini Ripoti hiyo

Mjumbe wa Uganda akisaini ripoti hiyo

Mjumbe wa Kenya akisaini ripoti hiyo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, Mhe. Clementine Mukeka akizungumza kwa niaba ya Makatibu Wakuu wenzake walioshiriki Mkutano wa Ngazi ya Makatibu Wakuu uliofanyika jijini Arusha kwa ajili ya kuandaa  Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango utakaofanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukifuatilia matukio mbalimbali wakati wa Mkutano wa Makatibu Wakuu

Sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania

Ujumbe wa Tanzania ukishiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu

 

RAIS WA JAMHURI YA BOTSWANA DKT. MOKGWEETSI ERIC KEABETSWE MASISI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU MBILI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimlaki Rais wa Jamhuri ya Botswana Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi,wakati akiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere - Dar es Salaam. Dkt. Masisi yuko Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Rais wa Botswana Dkt.Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi wakipita katikati ya gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya mapokezi ya Mhe. Masisi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Rais wa Botswana Dkt.Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi wakipita katikati ya gwaride lilioandaliwa kwa jailli ya mapokezi ya Mhe. Masisi

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwatambulisha baadhi ya wajumbe wa Tanzania walioambatana nae katika mapokezi ya Rais wa Botswana Dkt.Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nerere - Dar es Salaam.

Wednesday, June 9, 2021

BALOZI MULAMULA AMLAKI WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHINI BOTSWANA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimlaki Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Botswana Mhe. Lemogang Kwape mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere - Dar es Salaam.

Mhe. Lemogang Kwape amewasili Nchini kufuatia ziara ya kikazi ya siku mbili ya Rais wa Jamhuri ya Botswana Mheshimiwa Dkt. Mokgweetsi Eric Keabetswe Masisi anayetarajiwa kuwasili Nchini siku ya Alhamis  Juni 10, 2021
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Botswana  Mhe. Lemogang Kwape baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere - Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Botswana  Mhe. Lemogang Kwape baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere - Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Botswana  Mhe. Lemogang Kwape akiwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere - Dar es Salaam

Monday, June 7, 2021

BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WANAOSHUGHULIKIA MIPANGO KATIKA EAC KUKUTANA ARUSHA

Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (SCMEACP) unafanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 7 hadi 11 Juni 2021.


Mkutano huo ambao umeanza kwa Ngazi ya Wataalam leo tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 10 Juni 2021 na kuhitimishwa na Mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 11 Juni 2021.


Akifungua Mkutano wa Ngazi ya Wataalam, Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughilikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Mhe. Christophe Bazivamo amezipongeza Nchi Wanachama kwa kufufua viwanda vidogo na kutumia bidhaa za ndani hususan katika kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa Corona ambalo limeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli za uzalishaji na ufanyaji biashara katika nchi nyingi duniani zikiwemo zile za EAC.


Ameongeza kusema kuwa, ugonjwa wa Corona umetoa funzo kubwa kwa Nchi Wanachama wa EAC kwamba zinaweza kufanya biashara miongoni mwao na kujitosheleza kwa mahitaji mbalimbali ya msingi kwa maendeleo ya wananchi wa nchi hizo ikiwa ni utekelezaji wa Itifaki mojawapo muhimu ya Jumuiya ya Soko la Pamoja.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Ngazi ya Wataalam, Bi. Alice Yalla kutoka Jamhuri ya Kenya amesisitiza wajumbe kujadili kwa umakini agenda mbalimbali zilizopo mbele yao na kutoa mapendekezo yenye tija, ikizingatiwa kuwa Sekta ya Mipango ni moja ya Sekta muhimu katika Jumuiya ambayo pamoja na mambo mengine pia hushughulika na tathmini ya mipango na masuala yote yanayotekelezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki.


Mkutano wa Wataalam pia utapitia agenda mbalimbali muhimu ambazo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 9 na 10 Juni 2021 kwa majadiliano na hatimaye agenda hizo zitawasilishwa kwenye Mkutano ngazi ya  Mawaziri unaotarajiwa kufanyika jijini hapa tarehe 11 Juni 2021.


Miongoni mwa agenda hizo ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa kwenye vikao vilivyopita; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki; Kupitia maelekezo ya Baraza la Mawaziri kuhusu  Rasimu ya Maboresho ya Utaratibu wa Mafao katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu ombi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la kujiunga na EAC; Taarifa kuhusu hatua iliyofikiwa ya utatu wa Jumuiya za EAC-COMESA-SADC katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika; Taarifa ya Uchangiaji wa Bajeti ya EAC kutoka Nchi Wanachama; na Taarifa ya majadiliano kuhusu Eneo Huru la Biashara Barani Afrika.


Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ngazi ya Wataalam unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi. Kadhalika Mkutano huo umehudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama ambazo ni Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda na Sudan Kusini.

Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya wataalam uliofanyika jijini Arusha tarehe 7 Juni 2021 kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika Arusha tarehe 11 Juni 2021. Mkutano kwa ngazi ya wataalam unafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 9 Juni 2021 na utafuatiwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu tarehe 10 Juni 2021. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji  na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benard Haule.
Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta ya Uzalishaji na Jamii, Mhe. Christophe Bazivamo akifungua rasmi Mkutano wa Ngazi ya Wataalam uliofanyika jijini Arusha kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika  tarehe 11 Juni 2021

Mkurugenzi katika Wizara ya Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda ya Kenya na Mwenyekiti wa Mkutano wa Ngazi ya Wataalam,  Bi. Alice Yalla akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo uliofanyika jijini Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Juni 2021.

Ujumbe wa Kenya ukiwa kwenye mkutano wa ngazi ya wataalam

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania ukishiriki Mkutano wa ngazi ya wataalam
Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi Agnela Nyoni akifuatilia ufunguzi wa mkutano wa wataalam uliofanyika Arusha kwa ajili ya kuandaa Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Juni 2021.
Ujumbe wa Uganda ukiwa kwenye mkutano wa ngazi ya wataalam
Balozi Mteule na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Bibi Caroline Chipeta akifuatilia mkutano wa ngazi ya wataalam uliofanyika Arusha ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa 31 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Masahriki na Mipango katika Jumuiya ya Afrika Mashariki unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 Juni 2021.
Ujumbe kutoka Taasisi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki nao ukishiriki mkutano wa ngazi ya wataalam
Mkutano ukiendelea
Mjumbe kutoka Rwanda akiwa kwenye mkutano wa wataalam
Mjumbe wa Burundi naye akifuatilia mkutano
Sehemu ya ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ukishiriki mkutano wa wataalam
Mkutano ukiendelea
Mjumbe kutoka Tanzania akishiriki mkutano wa ngazi ya wataalam
Mkutano ukiendelea


BALOZI MULAMULA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini kwake jijini Dodoma. Dkt alifika Ofisini kwa Mhe. Waziri kujitambulisha na kujadiliana namna ya kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini alipomtembelea kwake jijini Dodoma.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini kwake jijini Dodoma.

Mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dodoma yakiendelea.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo ofisini kwake jijini Dodoma.

Waziri Mulamula amesema mazungumzo yake na Dkt. Taufila ambaye pia alikuwa anajitambulisha yamelenga kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania ili kuimarisha mahusiano hayo na hivyo kunufaika na miradi ya maendeleo.

Akiongelea uhusiano baina ya Tanzania na Benki ya Dunia Mhe. Balozi Mulamula amesema Tanzania imejipanga kuhakikisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo yanaimarika na kuendeleza uwezo wa Watanzania wanaosimamia miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki ya Dunia ikiwa ni pamoja na kuendeleza sekta binafsi na kuifanya kuwa imara.

“leo hapa tumejadiliana juu ya mahusiano yetu, kuangalia namna ya kuyaboresha ili kunufaika na miradi  ya maendeleo inayofadhiliwa na Benki hiyo, kuwajengea uwezo watu wetu wanaosimamia utekelezaji wa miradi hiyo na uimarishaji wa Sekta binafsi ili kuwa imara na hivyo kufikia maendeleo ya kweli,” alisema Balozi Mulamula

Akiongelea kuhusu mipango ya Serikali ya kuimarisha Sekta Binafsi Mhe Waziri Mulamula amemuhakikishia Dkt. Taufilo nia na mtizamo wa Serikali wa kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara na kuwekeza nchini ikiwa ni pamoja na kushirikiana na sekta binafsi hasa ikizingatiwa kuwa Benki ya Dunia inachukulia sekta binafsi kama chachu ya maendeleo na hivyo kuwa na miradi ya kusaidia ukuzaji wa Sekta binafsi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji huyowa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika kundi la kwanza Dkt. Taufila Nyamadzabo amesema miongoi mwa mambo waliyojadili leo ni pamoja na umuhimu wa kuhusisha sekta binafsi na kuiendeleza.

Amesema miongoni mwa vipaumbele vya Benki ya Dunia kwa sasa ni kuimarisha Sekta binafsi na kuifanya kuwa imara hasa katika maeneo ya biashara na uwekezaji pamoja na kuimarisha miundombinu ya usafirishaji, na ukuzaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ili kuiwezesha duniani kuendelea kufanya shughuli zake hasa katika kipindi hiki cha changamoto ya ugonjwa wa Covid 19.

Amesema wamekubaliana kuendelea kushirikiana na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Benki hiyo na hivyo kuiwezesha Tanzania kunufaika na miradi ya maendeleo inayosimamiwa na benki hiyo.