Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Care International, Bi. Michelle Nunn huku maafisa walio chini yao wakifuatilia mazungumzo hayo. |
Wednesday, July 13, 2022
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA RAIS WA CARE INTERNATIONAL
Tuesday, July 12, 2022
KIWANDA CHA LABIOFAM KIBAHA KUPANULIWA
Serikali za Tanzania na Cuba zipo katika mchakato wa kupanua kiwanda cha Labiofam kilichopo Kibaha, Pwani cha kuzalisha viuadudu vya mazalia ya mbu ili kiwe na uwezo wa kuzalisha mbolea na dawa nyingine za kuua wadudu waharibifu wa mazao ya kilimo.
Hayo
yamesemwa leo tarehe 12 Julai 2022 jijini Dar Es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt Grace Magembe wakati wa ufunguzi wa kikao kati ya
Serikali za Tanzania na Cuba cha kujadiliana kuhusu upanuzi wa kiwanda hicho
kinachoendeshwa kwa ubia baina ya Serikali hizo mbili.
Dkt.
Magembe ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaojadiliana na ujumbe wa
Cuba, alisema kuwa ana matumaini makubwa katika kikao hicho cha siku mbili,
wajumbe watafikia makubaliano yatakayokuwa na manufaa kwa wananchi wa pande
zote mbili.
“Kama
unavyofahamu asilimia 70 hadi 80 ya Watanzania ni wakulima, hivyo, uwepo wa kiwanda
hiki na uzalishaji wa mbolea na viuadudu ni fursa nzuri kwa wakulima wetu na nchi
kuendeleza sekta ya kilimo pamoja na wananchi kujipatia kipato kwa mazao watakayovuna”,
Dkt. Magembe alisema.
Kwa
upande wake kiongozi wa ujumbe wa Cuba ambaye ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa
Kimataifa kutoka Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo, Bw. Orlando Diaz Rodriguez
alisema kuwa uwepo wa kiwanda hicho ni ishara ya wazi ya uhusiano mzuri uliopo
kati ya Cuba na Tanzania.
Aidha,
naye alielezea matumaini yake kuwa majadiliano hayo ya siku mbili yatakuwa na
faida kubwa kwa maendeleo ya sekta ya kilimo ya Tanzania na azma ya Serikali ya
kupamabana na ugonjwa wa malaria na hatimaye kuuangamiza kabisa.
Wataalamu wa Tanzania wanaoshiriki kikao cha majadiliano kati ya Tanzania na Cuba kuhusu upanuzi wa kiwanda cha LABIOFAM kinachoendeshwa kwa ubia kati ya Cuba na Tanzania |
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt Grace Magembe (katikati), Kiongozi wa ujumbe wa Cuba ambaye ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo, Bw. Orlando Diaz Rodriguez (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Dkt. Nicolous Shombe wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania na Cuba unaofanya majadiliano kuhusu upanuzi wa kiwanda cha LABIOFAM |
Monday, July 11, 2022
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI ISRAEL ULIVYOADHIMISHA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI
Wadau mbalimbali nchini Israel wamepongeza jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza na kuienzi Lugha ya Kiswahili.
Pongezi hizo zimetolewa na wadau hao wakati wa Maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika tarehe katika Makazi ya Balozi wa Tanzania nchini humo tarehe 07Julai 2022 Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Gabriel Kalua amesema kuwa ametumia maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani kukukutana na kujadiliana na wadau mbalimbali kuhusu namna bora ya kukuza na kuendeleza Lugha hiyo adhimu. Aidha, Mhe. Balozi Kalua ambaye alijumuika na viongozi kutoka Serikali ya Israel, wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Tanzania, Watanzania wanaoishi nchini humo na wageni mbalimbali, alitumia maadhimisho hayo kugawa vitabu vya kujifunzia Kiswahili kikiwemo cha “Jifunze Kiswahili, Hazina ya Afrika: Kitabu cha Kwanza”, pamoja na kushiriki chakula cha Kitanzania na wadau hao. Kadhalika, Mhe. Balozi Kalua alitoa hotuba yake kwa lugha ya Kiswahili ambayo ilitafsiriwa kwa Kiebrania. Naye Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, Bibi Amit Gil Bayaz ambaye ni miongoni mwa viongozi kutoka Serikali ya Israel walioshiriki aliipongeza Tanzania kwa maadhimisho hayo. Maadhimisho hayo yalihitishwa kwa Wadau mbalimbali kushiriki chakula na vinywaji vya kitanzania ambapo walieleza kufurahishwa na ukarimu wa watanzanaia na kufurahia vinywaji na chakula cha kitanzania kilichoandaliwa kwa ajili yao. |
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Alex Gabriel Kalua akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika kwenye Makazi ya Balozi nchini humo tarehe 7 Julai 2022 na kuwashirikisha wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel ambaye ni Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki, Bibi Amit Gil Bayaz (wa pili kutoka kushoto), Rais wa Klabu ya Mabalozi waliopo Israel, Mhe. Balozi Yzihack Elden (kushoto) na Mwakilishi wa Balozi wa Heshima, Mhe. Chirich Nuriel Kasbian (wa pili kulia) |
Mhe. Balozi Kalua akimkabidhi kitabu cha kujifunza Kiswahili, Mkurugenzi wa Ukanda wa Afrika Mashariki, Bibi Amit Gil Bayaz. |
Wawakilishi kutoka Jeshi la Israel walioshiriki maadhimisho ya siku ya Kiswahili wakiwa na Mwambata Jeshi wa Ubalozi wa Tanzania nchini, Israel, Brig. Jen. Mziray |
Wadau mbalimbali wakionesha vitabu vya kujifunza Kiswahili walivyokabidhiwa |
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WANAFUNZI-DIASPORA WA MAREKANI.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
amekutana na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani
wanaofundisha na kusoma vyuo mbalimbali vya Marekani ambao wapo nchini kwa
ziara ya kikazi hadi tarehe 17 Julai 2022.
Ziara
hiyo iliyoratibiwa na Mtanzania-Diaspora, Bi Zawadi Sakapala ambaye ni mmiliki
wa kituo cha “Community Centre” kilichopo Kijichi jijini Dar Es Salaam inalenga
pamoja na mambo mngine, kutoa fursa kwa wanafunzi hao kujifunza masuala ya
utamaduni wa Tanzania na kubadilishana ujuzi na uzoefu katika masomo ya
sayansi, ufundi, ufundishaji na Usimamizi wa watoto wadogo (daycare). Katika
kikao hicho, Bi Zawadi alimfahamisha Mhe. Balozi Mulamula kuwa kituo chake
kimekuwa kikishirikiana na vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani kuratibu ziara
za walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani kutembelea nchi za
Afrika kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika sekta ya elimu. Hivyo,
ili kuimarisha sekta ya elimu katika nchi za Afrika, kikao hicho kiliazimia
kuongeza jitihada za kuhamasisha Waafrika wengi zaidi kujiunga na vyuo vya
Marekani, kuunganisha vyuo vya Afrika na Marekani, wanafunzi-Watanzania wanaopata
fursa ya kusoma Marekani, watumike kufundisha lugha ya Kiswahili ikiwa ni moja
ya njia ya kueneza lugha hiyo duniani pamoja na kwahimiza watu wenye asili ya
Afrika kutumia elimu, ujuzi na maarifa waliyopata wakiwa ughaibuni kuinua jamii
za nchi za Afrika. Wakati
huo huo, Balozi Mulamula amekutana na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Programu ya Maendeleo (UNDP) ambao upo nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo
na wadau wa siasa ili kubainisha maeneo ambayo, shirika hilo linaweza kusaidia
katika uendeshaji wa uchaguzi mkuu ujao. Ujumbe
huo unaongozwa na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani
ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola umefanikiwa kufanya vikao na wadau
mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wawakilishi wa vyama
vya siasa na asasi za kiraia, umepokea maoni ya wadau hao ya maoneo yanayohitaji
msaada na umeahidi utayafanyia kazi kikamilifu. Maeneo hayo ni pamoja na uelimishaji
wa wapiga kura, msaada wa kiufundi katika upigaji na uandikishwaji wa wapiga
kura na teknolojia ya mawasiliano wakati zoezi la uchaguzi. Kwa
upande wake, Balozi Mulamula aliueleza ujumbe huo kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kipindi kifupi cha
uongozi wake ameonesha dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya kisiasa
nchini, kwa kuhamasisha majadiliano ya kisiasa, ushirikishwaji wa wadau wote,
umoja na mshikamano wa kitaifa. Hivyo, aliuhakikishia ujumbe huo kuwa uchaguzi
ujao utaendelea kuwa huru, haki na amani kama ilivyo desturi ya Tanzania. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani (hawapo pichani) wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani ambao wapo nchini kwa ziara maalum hadi tarehe 17 Julai 2022. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza mmoja wa mwanafunzi anayesoma katika vyuo vikuu vya Marekani kuhusu mikakati ya kusaidia vijana wa Afrika kupata elimu bora itakayoweza kukabili mazingira ya dunia ya sasa. |
Mhitimu wa Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Howard cha nchini Marekani ambaye pia ni Kiongozi wa Taasisi ya 3GC Inc. akieleza shughuli za taasisi hiyo zinazolenga kuwasaidia vijana wa Afrika |
Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga wakifuatilia mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimvisha scurf ya bendera ya Tanzania, mmiliki wa kituo cha “Community Centre” kilichopo Kijichi jijini Dar Es Salaam, Bi. Zawadi Sakapala |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
Baadhi ya ujumbe uliongozana na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola kwenye mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Afisa huyo. |
Ujumbe wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ukifuatilia mazungumzo yake na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiagana na ujumbe wa UNDP ambao upo nchini kwa ajili ya kuzungumza na wadau wa siasa kuhusu uchaguzi. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa UNDP ambao upo nchini kwa ajili ya kuzungumza na wadau wa siasa kuhusu uchaguzi. |
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UN WOMEN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UN Women, Bi. Hodan Addou kwenye Hoteli ya Seana jinini Dar Es Salaam. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Lt. Jen. Mathew Edward Mkingule yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi Mteule Lt. Jen. Mathew Edward Mkingule baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
Saturday, July 9, 2022
WAZIRI MULAMULA: WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI FURSA ZA MASOKO KATIKA JUMUIYA ZA KIKANDA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na mmoja wa washiriki wa Maonesho ya Bukoba |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (aliyevalia kilemba) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Charles Mbuge akiwa katika picha ya pamoja Waandaaji wa Maonesho ya Kagera na Washiriki wa maonesho hayo. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Moses Machali alipowasili kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Bukoba mjini |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimkabidhi cheti cha kufanyavizuri mmoja wa washiriki wa Maonesho Bukoba kutoka nchini Burundi |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza hadhira iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha na mmoja wa washiriki wa Bukoba Expo mzalishaji wa bidhaa za mafuta ya asili ya ngozi |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokelewa katika viwanja vya CCM mjini Bukoba alipowasili kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba “Bukoba Expo”. |
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye madhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwasili kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba “Bukoba Expo” yaliyofanyika katika viwanja vya CCM Bukoba mjini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na mmoja wa washiriki wa Maonesho ya Bukoba |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiangalia bidhaa za mmoja wa washiriki wa Bukoba Expo |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Mati Super Brands Ltd Bw. Living Munishi kwenye maadhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifurahia jambo baada zoezi la upandaji mti kwenye madhimisho ya kilele cha Maonesho ya Bukoba |
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA NSSF ZAJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI NJE YA NCHI
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii - NSSF, Bw. Masha Mshomba tarehe 8 Julai 2022 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao wamejadili juu ya umuhimu wa kukuza na kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara na mfuko huo wa NSSF.
Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamezungumzia kuhusu uwekezaji kwenye viwanja vya Serikali nje ya nchi ili kuona namna ambavyo Wizara na NSSF wanaweza kushirikiana katika miradi ya ujenzi wa ofisi na vitega uchumi.
Aidha, Balozi Sokoine akaeleza kuwa Serikali ina miliki viwanja zaidi ya 40 kwenye maeneo ya uwakilishi nje ya nchi, hivyo akatoa rai kwa taasisi hiyo kushirikiana na Wizara katika kuviendeleza kwa kujenga majengo ya Ofisi za Balozi pamoja na vitega uchumi ili kuipunguzia Serikali gharama ya kupanga lakini zaidi kupata faida kutokana na vitega uchumi hivyo.
Naye Bw. Mshomba aliafiki wazo hilo la uwekezaji na kueleza kuwa NSSF imeshakuwa na mipango ya miradi ya uwekezaji nje ya nchi hivyo, wazo hilo limekuja wakati mwafaka na kwamba NSSF inaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kufungua mipaka hususan katika sekta ya biashara na uwekezaji.
Aidha, Kikao hicho kiliridhia kuundwa kwa timu ya Wataalamu kutoka katika pande zote mbili ili kuruhusu kufanyika kwa tathmini ya kina juu ya uwekezaji huo na faida zake ili kuweza kuwa na miradi ya pamoja na Wizara wenye tija kwa Taifa.
======================================
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Joseph Sokoine (kulia) amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii - NSSF, Bw. Masha Mshomba tarehe 8 Julai 2022 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
|
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Sera na Mipango, Bw. Justin Kisoka akifafanua juu ya uwekezaji wa miradi ya pamoja na namna Wizara na NSSF zinavyoweza kushirikiana katika kutathmini uwekezaji kwenye maeneo ya miradi. |
Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara hiyo wakifuatilia mazungumzo. |
Picha ya pamoja |