Saturday, August 27, 2022
MKUTANO WA NANE WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA TICAD WAANZA MJINI TUNIS, TUNISIA
Friday, August 26, 2022
TANZANIA NA IRAN ZAAHIDI KUONGEZA MAENEO MAPYA YA USHIRIKIANO
NSSF YACHANGIA M.50 KUTENGENEZA KANZIDATA YA DIASPORA
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesaini makubaliano na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya kuipatia Wizara Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kufadhili utengenezaji wa Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).
Makubaliano hayo yamesainiwa leo kati ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mkurugenzi wa Uthaminishaji, Takwimu na Usimamizi wa Hadhari, Bw. Ibrahim Maftah kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo, Balozi Bwana amesema kukamilika kwa mfumo huo wa kidigitali kutaiwezesha Serikali kuwasajili, kuwatambua na kurahisisha shughuli za kuwaratibu Diaspora na kuwawezesha kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya Taifa.
“Leo hii tumeshuhudia utiaji saini wa makubaliano ambayo yataiwezesha NSSF kutoa Shilingi Milioni 50 ambazo zitaiwezesha Wizara kutengeneza Mfumo wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, kitendo hiki ni mwanzo wa ushirikiano wa muda mrefu ambao Wizara umekuwa nao na NSSF, ni matarajio ya Wizara kuwa NSSF itahuisha program yao ya Diaspora na kubuni programu mpya ili kutoa huduma kwa Diaspora wetu na wao kunufaika zaidi na programu hizo,” alisema Balozi Bwana.
Balozi Bwana aliongeza kuwa Diaspora ni eneo muhimu la uwekezaji kwa maendeleo ya taifa hasa ikizingatiwa kuwa kwa mwaka 2021 Diaspora waliwekeza jumla ya Shilingi Bilioni 3.9 katika mpango wa UTT Amis na kutuma nchini Shilingi Milioni 569.3 kwa ndugu na jamaa zao hapa nchini.
“Serikali inategemea mfumo utakaowatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania Duniani kote kupata huduma nyingi na muhimu wanazohitaji na kushiriki kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo biashara, uchumi na uwekezaji hapa nchini,” aliongeza Balozi Bwana.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Ibrahim Maftah ameipongeza Wizara kwa kuja na wazo la kuanzisha mfumo huo na kuihakikishia Wizara kuwa NSSF itaendelea kushirikiana na Wizara kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa Diaspora Digital Hub unakamilika na kutumika katika maeneo yote yenye tija kwao na kwa taifa kwa ujumla.
“Kitendo cha NSSF kusaini makubaliano hayo kinaonesha utayari na muelekeo wetu katika kutumia fursa mbalimbali zinazopatikana katika eneo la Diaspora,” alisema Bw. Maftah.
Awali mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde amesema kukamilika kwa mfumo huo kutaiwezesha Serikali kufahamu kwa ufasaha idadi ya diaspora wake, ujuzi walionao, elimu zao .
Ameongeza kuwa mfumo huo utakapokamilika diaspora wataweza kupata huduma maalum zitakazoandaliwa kwa ajili ya mahitaji yao kama vile huduma za kibenki, hifadhi ya jamii, bima ya afya kwa wategemezi wao waliopo hapa nyumbani, taarifa za fursa za uwekezaji, biashara na masoko, masuala ya uhamiaji, vitambuklkisho vya taifa na huduma nyinginezo.
KAMISHINA MKUU WA UNHCR ATUA DODOMA
Kamishina Mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa
Mataifa (UNHCR), Bw. Filippo Grandi yupo nchini tokea tarehe 24 Agosti 2022 kwa
ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine, atafanya mazungumzo na viongozi
wakuu wa Serikali na kutembelea Kambi za Wakimbizi mkoani Kigoma.
Thursday, August 25, 2022
TANZANIA YAIHAKIKISHIA IRAN MAZINGIRA SALAMA YA BIASHARA, UWEKEZAJI
Meza kuu ikiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Iran lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam |
WIZARA NA BENKI YA NMB WASAINI HATI YA MAKUBALIANO
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Benki ya NMB Plc wamesaini Hati ya Makubaliano ya kutengeneza Mfumo wa Kanzi Data wa Kidigitali wa kutunza taarifa za Diaspora, (Diaspora Digital Hub).
Makubaliano hayo yamesainiwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora Balozi James Bwana kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa na Serikali wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Akiongea katika hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Balozi Bwana amesema mfumo huo wa kidigitali utaisaidia Serikali kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania waliopo sehemu mbalimbali ulimwenguni kupata huduma mbalimbali na kushiriki kidigitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo, biashara, uchumi na uwekezaji nchini.
“Ushirikiano wa Wizara na Benki ya NMB Plc ni wa muda mrefu na wenye mafanikio mengi katika kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Tanzania. Wizara ina imani kuwa kupitia udhamini huu wa shilingi milioni 100 kutoka Benki ya NMB, fedha hizo zitawezesha kukamilisha matengenezo ya mfumo wa Diaspora Digital Hub na hivyo kuboresha huduma zenye kukidhi mahitaji ya Diaspora wote ulimwenguni,” amesema Balozi Bwana
Balozi Bwana ameongeza kuwa, mfumo huo pamoja na mambo mengine, utafungua uwezekano wa fursa zaidi za ushirikiano kati ya Wizara na Benki hiyo utawezesha utunzaji wa taarifa mbalimbali za Diaspora wa Tanzania popote walipo ulimwenguni na hivyo kurahisisha kazi ya uratibu wa Diaspora.
Balozi Bwana amesema Serikali inategemea kuwa kukamilika kwa mfumo huo kutaweza kuwatambua, kuwasajili na kuwawezesha Diaspora wa Tanzania Duniani kote kupata huduma nyingi na muhimu wanazohitaji na kushiriki kidijitali katika shughuli mbalimbali za maendeleo biashara, uchumi na uwekezaji hapa nchini.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Bw. Alfred Shao amesema benki yao inaamini kuwa kukamilika kwa mfumo huo kutawawezesha Diaspora wa Tanzania kuungana, kutambulika na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzi Data ya uhakika na kuwafikia diaspora wengi kwa wakati mmoja na hivyo kuleta mafanikio makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja anayeishi nje ya nchi.
"Sisi NMB tunaamini kuwa mfumo huu, utawaunganisha, utawatambua na kuiwezesha Serikali kuwa na Kanzidata ya Diaspora wake, ni wazi kuwa mfumo huu utaleta maendeleo makubwa kwa Taifa na Mtanzania mmoja mmoja wanaoishi nje ya nchi," alisema Bw. Shao
Aliahidi kuwa NMB itaendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha mfumo wa kidigitali wa Diaspora Digital Hub unakamilika kwa wakati.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Semeni Nandonde amesema makubaliano yaliyoingiwa kati ya Wizara na Benki ya NMB yanaashiria utayari wao katika kulifadhili na kuliwezesha wazo la Wizara la kuwa na mfumo wa kutunza taarifa za Diaspora na kuwawezesha dispora kunufaika na huduma mbalimbali pindi mfumo huo utakapokamilika.
JPC YA TANZANIA NA YAMALIZIKA
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA IRANI AWASILI TANZANIA KWA ZIARA YA KIKAZI
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mhe. Amir Abdollahian aliwasili nchini jana usiku kwa ziara ya kikazi ya siku tatu na kupokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam
Mara baada ya kuwasili nchini, Mhe. Abdollahian alisema, lengo la ziara yake nchini Tanzania ni kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Iran na Tanzania katika sekta za kisiasa na kiuchumi.
Nae Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula alimueleza nia ya Serikali ya Tanzania ni kuendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya sita imejidhatiti katika kukuza na kuendeleza Diplomasia ya Uchumi hivyo ni matumaini yake kuwa ujio wake hapa nchini utachangia kuendeleza diplomasia ya uchumi kati ya Tanzania na Iran.
Wednesday, August 24, 2022
TANZANIA YAIHAKIKISHIA MSUMBIJI KUENDELEZA USHIRIKIANO
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022. |
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022. |
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022. |
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaofanyika jijini Dar Es Salaam tarehe 22 Agosti 2022. |
Mshereheshaji wa Mkutano wa 15 wa Tume ya Pamoja ya kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22-24 Agosti 2022 akifanya kazi yake |
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati akifungua Mkutano wa 15 wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano ngazi ya Mawaziri kati ya Tanzania na Msumbiji unaoendelea jijini Dar Es Salaam tokea tarehe 22 Agosti 2022.
Amesema Tanzania na Msumbiji ina uhusiano wa kihistoria ambao ni wa kindugu na kwamba Tanzania itaendelea kushirikiana nayo ili kuhakikisha amani inapatikana huko kaskazini mwa nchi hiyo.
"Wakati tukikutana hapa jijini Dar es Salaam nchi zetu na ukanda wa kusini mwa bara la Afrika unakabiliwa na tishio la vitendo vya kigaidi katika jimbo la Gabo del Gado", alisema na kuongeza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Msumbiji ili kuhakikisha amani inapatikana katika eneo hilo.
Amesema kuwepo kwa vitendo vya kigaidi vinavyosababishwa na wanamgambo walioko katika jimbo hilo vinasababisha uharibifu wa mali,vifo na majeruhi kwa watu wasio na hatia na hivyo kuleta tishio la usalama kwa watu wa ukanda wote wa kusini mwa bara la Afrika.
Amesema ni matumaini yake kuwa mkutano huu wa 15 utaimarisha zaidi ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Msumbiji na kusaidia harakati za kujiendeleza kiuchumi kwa faida na manufaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Amesema Msumbiji ni ndugu na Tanzania na kusisitiza kuendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja
Ameishukuru Serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kuwasaidia na kuchangia jeshi la pamoja la SADC katika kukabiliana na vitendo vya kigaidi nchini Msumbiji