Monday, September 12, 2022

TANZANIA YASISITIZA KUBORESHA MIFUMO KUWAINUA WANAWAKE NA VIJANA KIUCHUMI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kusimamia mifumo ya utendaji kazi katika Serikali yake ili kuwawezesha wanawake na vijana washiriki kikamilifu katika biashara.

Ahadi hiyo imetolewa wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara ulioandaliwa na Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) na kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022.

Akiongea katika mkutano huo, Mhe. Rais Samia ameeleza baadhi ya maeneo ambayo Serikali ya Awamu ya Sita imeyafanyia maboresho ili biashara zinazofanywa na Wanawake na Vijana nchini zilete matokeo chanya sambamba na kuinua kipato chao na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Maeneo hayo ni pamoja na: Kuondoa vikwazo vya biashara, kuwawezesha wanawake kupata mikopo ya riba nafuu, maboresho katika mifumo ya tozo katika sekta mbalimbali kama vile kilimo na madini, kuwezeshwa kupata vyeti vya ubora kwa ajili ya kuingia katika ushindani wa soko la kimataifa na kupunguza ushuru unaotozwa na mamlaka mbalimbali za Serikali.

Aidha, Mhe, Rais Samia amesema kuwa Serikali yake inatoa nafasi za upendeleo kwa sekta binafsi kushiriki katika shughuli za maendeleo, na kwa sasa Tanzania imetoa kipaumbele kwa wanawake ambapo asilimia 30 ya manunuzi yote makubwa ya Serikali yanatolewa kwa makampuni ya wanawake.

“Mapema mwezi Mei 2022 nikiwa nchini Ghana kwenye mkutano ulioratibiwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Serikali ya Ghana ambao uliwakutanisha Wakuu wa Nchi na Serikali  nilipewa heshima ya kuwa kinara wa hamasa ya kuinua Wanawake na Vijana kwenye biashara, hivyo naahidi kuendelea kusimamia mapambano hayo”. Alisema Mhe. Rais Samia.

Akieleza zaidi, Mhe. Rais Samia ameeleza kuwa ili kufikia malengo ya kuinua biashara ni vema sasa nchi za Afrika zikawekeza kwenye miundombinu ili ziweze kufikika na kurahisisha shughuli za biashara kwa wananchi wake ambapo sehemu kubwa ya wajasiliamali wake ni wanawake na vijana.

Pia amesisitiza kuwa manufaa ya itifaki ya Wanawake na Vijana katika biashara kwenye Mkataba wa Eneo Huru Barani Afrika hayawezi kupatikana moja kwa moja kama mipango ya kitaifa ya nchi wanachama haitowajumuisha wanawake na vijana katika utekelezaji wake. 

Hivyo, ni vema nchi wanachama zikawekeza pia kwenye tafiti ili kufahamu namna bora ya kuondoa changamoto kwenye uhalisia wa jambo husika ambapo alieleza kwa nyakati tofauti Tanzania imefanya tafiti katika masoko ili yaweze kunufaisha wanawake na kusaidia kuwajengea miundombinu wezeshe kwa shughuli za biashara.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais ameeleza kuwa Tanzania inaandaa mpango wa kusimamia usawa kwa kizazi kijacho ili kuwawezesha wanawake kupata fursa sawa na wanaume na kuhakikisha wanawake na vijana wanawezeshwa kiuchumi na kuwekewa mfumo utakaowawezesha kupata ajira rasmi na zenye ujira utakaowainua kiuchumi kwa maendeleo ya Taifa.

Mhe. Rais Samia pia alitumia fursa ya mkutano huo kunadi fursa za uwekezaji zilizopo nchini katika sekta za kilimo cha mazao ya chakula, matunda na mbogamboga, sekta ya mifugo hususan nyama na bidhaa za ngozi, madini na utalii.

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Mhe Balozi Liberata Mulamula katika mkutano huo aliongoza majadiliano yaliyokuwa na mada isemayo “Kuunga mkono Uongozi wa Wanawake na Vijana katika Biashara” (Supporting Women and Youth’s Leadership in Trade).

Mjadala huo ulihusisha viongozi wakuu wanawake wa nchi za Afrika ambao ni: Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Joyce Banda, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Taylor-Howard, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo, Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Eneo Huru la Biashara Barani Afrika,Mhe. Wamkele Mene na Naibu Mwenyekiti, Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Dkt. Monique Nsanzabaganwa.

Washiriki wengine wa mkutano huo ni pamoja na: Mabalozi, Mawaziri wanaohusika na Biashara na Mawaziri wanaohusika na masuala ya jinsia. wanawake na vijana wanaojishughulisha na masuala ya biashara, watunga será na wadau wa maendeleo.

Sanjari na mkutano huo, wajasiriamali zaidi ya 80 wameshiriki kwenye maonesho ya bidhaa mbalimbali ambapo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ina washiriki wapatao 72.

 ==============================================================

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 

Sehemu ya Mawaziri na Viongozi Waandamizi kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 



Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 

Katibu wa Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika, Bw. Seif Kamtunda akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mindi Kasiga akisherehesha wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma Rajab akisalimiana na sehemu ya Mawaziri walioshiriki Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam. 

Picha ya pamoja

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongoza majadiliano yaliyokuwa na mada isemayo “Kuunga mkono Uongozi wa Wanawake na Vijana katika Biashara” (Supporting Women and Youth’s Leadership in Trade) wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Joyce Banda akichangia hoja kwenye majadiliano yaliyokuwa na mada isemayo “Kuunga mkono Uongozi wa Wanawake na Vijana katika Biashara” (Supporting Women and Youth’s Leadership in Trade) wakati wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) unaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Majadiliano yakiendelea.
Picha ya pamoja, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Malawi, Mhe. Joyce Banda (wa pili kushoto) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Taylor-Howard (wa pili kulia), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo (katikati) na Naibu Mwenyekiti, Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Mhe. Dkt. Monique Nsanzabaganwa (wa kwanza kushoto).

TANZANIA NA DRC ZAKUTANA DAR KUJADILI BIASHARA NA UWEKEZAJI



Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz akiwakaribisha Makatibu Wakuu wa Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Balozi Joseph Sokoine na Mhe. Zacharie Tshimbinda Bilolo  kusoma hotuba za ufunguzi za Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na DRC. 
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akipitia hotuba yake ya ufunguzi ya Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na DRC. 

Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz akifafanua jambo kwa viongozi kuhusu Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na DRC. 

Sehemu ya Ujumbe wa DRC unaoshiriki Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na DRC. 

Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na DRC ngazi ya wataalam unaendelea jijini Dar Es Salaam. 
Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza jambo na Konseli Mkuu wa Tanzania, Lubumbashi, Bw. Selestine Kakere kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na DRC. 

Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mtangamano wa Kikanda na Nchi zinazongumza Kifaransa wa DRC, Mhe. Zacharie Tshimbinda Bilolo wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tanzania na DRC wanaoshiriki Mkutano wa Tatu wa Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na DRC. 


 

Sunday, September 11, 2022

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA WA AfCFTA

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar-es-salaam. 

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika” utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 Jijini Dar es Salaam. 

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye ataufungua rasmi mkutano huo tarehe 12 Septemba 2022 katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano (JNICC), Dar es Salaam.

Mkutano huo utahudhuriwa na  Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali, Marais Wastaafu, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mabalozi, Mawaziri wa Biashara na Mawaziri wa masuala ya jinsia.
 
Mkutano huu pia utawakutanisha, Wanawake na Vijana wanaojishughulisha na masuala ya biashara, watunga sera, wafadhili, wadau wa maendeleo, na wadau wengine muhimu wa biashara barani Afrika ambao watajadili kwa kina agenda Wanawake na Vijana katika biashara barani Afrika.

Viongozi Wakuu walioawasili nchini na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ili kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Howard-Taylor na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo.
============================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Howard-Taylor (kushoto) amewasili nchini kushiriki Mkutano wa Wanawake na Vijana katika biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) utakaofanyika kuanzia  tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Howard-Taylor amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba 2022.

Mhe. Dkt. Jewel Howard-Taylor (kushoto) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba 2022.

==================================
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula pia amempokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Jessica Allupo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba, 2022.

 Mhe. Allupo amewasili nchini kushiriki Mkutano wa Wanawake na Vijana katika biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) utakaofanyika 
kuanzia  tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

===============================
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula alipata  wasaa wa kuagana na Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohola duniani, Mtukufu Syden Mufaddal Saifuddin aliyekuwa nchini kwa ziara. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula  akizungumza na Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora duniani, Mtukufu Syden Mufaddal Saifuddin katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Friday, September 9, 2022

WAZIRI MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Uingereza nchini kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II. Kulia ni Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar 
  


Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme  akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Uingereza nchini kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Balozi Mindi Kasiga (kulia) akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar (kushoto) alipowasili katika ubalozi wa Uingereza kutoa pole kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar (kushoto) alipowasili katika ubalozi wa Uingereza kutoa pole kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II.


Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar akizungumza na Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Liberata Mulamula (wa tatu kulia).

Mazungumzo yakiendelea.

 

TANZANIA, DENMARK KUSHIRIKIANA SEKTA ZA UCHUMI WA BULUU, KILIMO

Katika jitihada za kukuza na kuendeleza diplomasia ya uchumi, Serikali za Tanzania na Denmark zimeahidi kuendelea kushirikiana katika sekta za uchumi wa Buluu pamoja na Kilimo.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) alipokutana na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.  

Waziri Mulamula ameeleza kuwa Ushirikiano wa Tanzania na Denmark ni wa muda mrefu na wa kihistoria hivyo Tanzania itaendeleza  ushirikiano huo kwa maendeleo ya  kichumi na kijamii kwa maslahi ya mataifa yote mawili. 

Pamoja na mambo mengine, Waziri Mulamula amemuelezea Mhe. Mette Spandet juu ya fursa mbalimbali ambazo ziko Tanzania katika kukuza sekta za uchumi wa buluu na kilimo.

“Tanzania inazo fursa nyingi katika sekta ya Uchumi wa Buluu ikiwemo uvuvi, idadi kubwa ya Samaki na wa aina mbalimbali ambapo ni fursa ya kibiashara, tunazikaribisha kampuni za Denmark kuwekeza kupitia sekta hiyo,” amesema Balozi Mulamula.

Viongozi hao pia wamejadili njia za kuboresha sekta ya kilimo nchini Tanzania ili kuwawezesha Watanzania wengi kunufaika na sekta hiyo hasa ikizingatiwa kuwa asilimia kubwa ya watanzania hutegemea kilimo.

Kwa upande wake Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Spandent ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano wake na Denmark na kuahidi kuendelea kuudumisha ushirikiano huo katika sekta za kilimo, biashara na uwekezaji, tehama, utalii, demokrasia na uwezeshaji wa wanawake kiuchumi.

Katika tukio jingine, Waziri Mulamula amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya mataifa hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet wakati wa mazungumzo yao katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Mette Norgaard Spandet katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam 



















VACANCY ANNOUNCEMENT



 

Thursday, September 8, 2022

RAIS SAMIA AIELEKEZANDC KUTOA KIPAOMBELE KWA WANAWAKE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama,Wizara na taasisi mbalimbali kuwateuwa washiriki wenye sifa hususan vijana na kuwapa kipaumbele wanawake kushiriki mafunzo yanayotolewa na Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC).

Mhe. Rais Samia ametoa maelekezo hayo Septemba 8, 2022 wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012.

Mhe. Samia alisema kuna umuhimu wa kuwapa kipaumbele wanawake ili waweze kupata mafunzo hali itakayosaidia kuongeza tija na ufanisi katika maeneo yao ya kazi na Taifa kwa ujumla kwani ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii.

Alisema pamoja na mafanikio yaliyopatikana kwenye kipindi cha miaka kumi anapenda kuona masuala muhimu yanatimia katika muda mfupi ikiwemo kwenda kuwafundisha watu wa ngazi za chini kwenye Serikali za Mikoa na  Wilaya kwani huko ndio kuna kundi kubwa la watu.

"Mafunzo yanayotolewa kwenye ngazi za juu ni lazima yashuke chini ili wafundishwe na kupata uelewa wa masuala ya msingi ya usalama na kuitumikia nchi kizalendo.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax alisema kuwepo kwa chuo hicho nchini kimeliwezesha Jeshi la Tanzania kutoa mafunzo kwa maafisa wakuu wengi zaidi tofauti na awali ambapo Jeshi lililazimika kuwapeleka maafisa wake kupata mafunzo hayo nje ya nchi.

Aliongeza kuwa NDC imewezesha kutoa mafunzo kwa idara nyingine za Serikali na viongozi mbalimbali kwa kuwajengea uelewa wa pamoja juu ya usalama.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni mdau muhimu kwa maendeleo ya Chuo Cha Taifa Cha Ulinzi ambapo hadi sasa Wizara imeendelea kupeleka washiriki kwenye kozi ndefu na fupi ambapo miongoni mwao Wanawake wawili walioshiriki kozi ndefu walitunikiwa tuzo za uongozi kwa nyakati tofauti.

Wanawake hao ni Mkurugenzi wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini, Balozi Mindi Kasiga mwaka 2019 pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Itifaki, Bi. Naomi Zegezege mwaka 2022 wote kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Kadhalika, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika mahojiano binafsi alisema kuwa Chuo Cha NDC kimekuwa msaada mkubwa katika kuwanoa viongozi mbalimbali na baadhi ya watumishi wizarani kujengewa uwezo jambo ambalo limeongeza ufanisi kazini.

"Kila mwaka tumekuwa tukipeleka watumishi wawili katika Mafunzo ya muda mrefu NDC na matunda ya mafunzo hayo yamekuwa chanya kwa Wizara ninayoisimamia, natumaini kuwa tutaendelea kuwapeleka watumishi wengi zaidi baadae hususan Wanawake ili kuwajengea uwezo zaidi wa kujiamini wakati wanapotekeleza majukumu Yao," alisema Balozi Mulamula
Hafla ya Maadhimisho ya miaka 10 ya NDC ilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali waandamizi wa Serikali.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012 
Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Mambio ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Midni Kasiga (wa kwanza kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi waliopata fursa ya kusoma kozi za muda mrefu  katika Chuo cha NDC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) (katikati) pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Mchemba (Mb.) wakizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa (Mb.) waliposhiriki katika hafla ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Vita Kawawa (Mb.) wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Chuo cha Taifa cha Ulinzi mwaka 2012

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Viongozi waandamizi wa Serikali na Wahitimu wa NDC

 

BALOZI MULAMULA AIFARIJI FAMILIA YA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb.) ametoa pole kwa Familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi kufuatia kifo cha mtoto wake Hassan Ali Hassan  kilichotokea tarehe 31 Agosti, 2022 katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akitoa mkono wa pole kwa familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipomtembelea nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam