Sunday, September 11, 2022

TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA WA AfCFTA

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar-es-salaam. 

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa “Wanawake na Vijana katika Biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika” utakaofanyika kuanzia tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 Jijini Dar es Salaam. 

Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, ambaye ataufungua rasmi mkutano huo tarehe 12 Septemba 2022 katika Kituo Cha Kimataifa Cha Mikutano (JNICC), Dar es Salaam.

Mkutano huo utahudhuriwa na  Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali, Marais Wastaafu, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mabalozi, Mawaziri wa Biashara na Mawaziri wa masuala ya jinsia.
 
Mkutano huu pia utawakutanisha, Wanawake na Vijana wanaojishughulisha na masuala ya biashara, watunga sera, wafadhili, wadau wa maendeleo, na wadau wengine muhimu wa biashara barani Afrika ambao watajadili kwa kina agenda Wanawake na Vijana katika biashara barani Afrika.

Viongozi Wakuu walioawasili nchini na kupokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ili kuhudhuria mkutano huo ni pamoja na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Howard-Taylor na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo.
============================

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia, Mhe. Dkt. Jewel Howard-Taylor (kushoto) amewasili nchini kushiriki Mkutano wa Wanawake na Vijana katika biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) utakaofanyika kuanzia  tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Howard-Taylor amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba 2022.

Mhe. Dkt. Jewel Howard-Taylor (kushoto) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba 2022.

==================================
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula pia amempokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Jessica Allupo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimpokea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba 2022.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akizungumza na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Jessica Allupo (kushoto) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba, 2022.

 Mhe. Allupo amewasili nchini kushiriki Mkutano wa Wanawake na Vijana katika biashara kwenye Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) utakaofanyika 
kuanzia  tarehe 12 hadi 14 Septemba, 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

===============================
Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula alipata  wasaa wa kuagana na Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohola duniani, Mtukufu Syden Mufaddal Saifuddin aliyekuwa nchini kwa ziara. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula  akizungumza na Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora duniani, Mtukufu Syden Mufaddal Saifuddin katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.