Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula
akiwa katika Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa
Usuluhishi ujijini New York. |
Wenyeviti wenza wa Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi Uturuki na Finland wakiwasikiliza washiriki wa kikao hicho |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe Balozi Liberata Mulamula ameshiriki Mkutano wa 12 wa Mawaziri Marafiki wa Umoja wa Mataifa wa Usuluhishi unaofanyika sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York.
Akizungumza katika mkutano huo Balozi Mulamula amesema usuluhishi ni njia muhimu katika kutatua changamoto za migogoro duniani na kuusihi Umoja wa Mataifa kuliingiza suala la usuluhishi katika mifumo ya utatuzi wa migogoro ya Umoja wa Mataifa.
Amesema usluhishi ukiingizwa katika mifumo ya utatuzi ya migogoro ya Umoja huo utasaidia shughuli za upatanishi na utatuzio wa migogoro na hivyo kuufanya Umoja huo kufikia lengo la utatuzi wa migogoro na kuifanya dunia kuwa sehemu salama .
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.