|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
akisalimiana na Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa
Mataifa jijini New York ikiwa ni moja ya mikutano ya pembeni inayoendelea sambamba na Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa nvhini Marekani. |
|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
akiangalia kitabu cha taarifa alichopatiwa na na Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa
Mataifa jijini New York. |
|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
akimuelezea kuhusu zawadi ya picha aliyompa Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa
Mataifa jijini New York. |
|
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
na ujumbe wake katika picha ya pamoja na Waziri wa Nchi, Maendeleo, Kifaransa na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa
Mataifa jijini New York. |
|
Waziri Mulamula
alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini
New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao.
|
|
Waziri Mulamula
akiwa na Balozi wa Tanznia nchini Marekani Mhe. Dke Elsie Kanza (wa kwanza kulia) walipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini
New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi zao. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Mhe. Chrysoula Zacharopoulou katika Ofisi za Ubalozi wa Ufaransa Umoja wa Mataifa jijini New York.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo na namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Ufaransa na namna ya kuendeleza sekta za uchukuzi, muindombinu, kilimo, biashara na uwekezaji nchini.
Viongozi hao pia wamejadiliana namna ya kuongeza ujazo wa biashara kati ya Tanzania na Ufaransa na kuihusisha sekta binafsi katika harakati za kuinua uchumi wa Tanzania.
Katika tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Mhe. Vincent Biruta jijini New York na kujadiliana juu ya masuala yenye maslahi baina ya nchi hizo.
Viongozi hao wajadili namna wanavyoweza kushirikiana kupitia sekta ya biashara, uwekezaji na uchukuzi na hivyo kuchangia harakati za ukuzaji wa uchumi wan chi hizo.
Viongozi hao wako jijini New York kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) unaoendelea nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.