Monday, September 19, 2022

DKT. MPANGO AKUTANA NA DKT KABERUKA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akiwa katika mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango akizungumza na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

  

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika picha na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka baada ya kukamilika kwa mazungumzo katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango katika picha ya pamoja na timu iliyoshiriki mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka walipokutana katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.






Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango amekutana kwa mazungumzo na Rais wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na mwanzilishi ya Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Donald Kaberuka katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania Jijini New York tarehe 18 Septemba 2022.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yenye lengo la kuleta maendeleo ya kiuchumi katika bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla ikiwa ni pamoja na jinsi taasisi hiyo inavyoweza kushirikiana na Benki ya Afroexim kuanzisha mfumo wa malipo wa pamoja Barani Afrika hasa ikizingatiwa utekelezaji wa Soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Dkt. Mpango amesema kuanzishwa kwa mfumo huo kunaweza kufungua fursa nyingi na kurahisisha ufanyaji biashara katika Jumuiya mbalimbali kuanzia Afrika, SADC na EAC na kuongeza kuwa ni vyema  Taasisi hiyo na washirika wake kuangalia na kujipanga jinsi ya kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza kutokana na uanzishwaji wa mfumo huo

“Ni imani yangu kuwa kukamilika kwa mfumo huo kunaweza kuondoa vikwazo vingi visivyo vya kiforodha ambavyo nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliana nazo,” amesema Dkt. Mpango.
    
Naye Mwanzilishi wa Taasisi ya Southbridge ya nchini Marekani, Dkt. Kaberuka amemhakikishia Dkt. Mpango utayari wa taasisi hiyo kushirikiana na Benki ya Afroexim kwa lengo la kuondoa vikwazo mbalimbali vya kibiashara ambavyo nchi za Afrika zimekuwa zikikabiliana nazo na hivyo kuzuia ukuaji wa uchumi unaostahili.

Amesema wao kama wanaafrika wanaangalia njia na mbinu mbalimbali za kuwezesha ufanyaji biashara ndani ya bara la Afrika ili kujijengea uwezo wa kufanya biashara na hivyo kunufaika na rasilimali ilizonazo.

Makamu wa Rais, Dkt. Mpango yuko jijini New York nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.