Friday, September 16, 2022

BALOZI MINDI ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA WANAWAKE WA AFRIKA KATIKA UONGOZI

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga ameelezea uzoefu wa Tanzania kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia na uongozi wakati akiwasilisha mada katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) unaoendelea jijini Durban, Afrika Kusini. 

Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika kuanzia tarehe 15-17 Septemba 2022, chini ya wenyeji wa kiongozi wa Jimbo la KwaZulu-Natal Bi. Nomusa Dube-Ncube, hufanyika kila mwaka kwa kuwaleta pamoja viongozi wanawake kutoka Bara la Afrika ili kujadili masuala yanayohusu usawa wa kijinsia na uongozi. 

Miongoni mwa waliohuduhuria mkutano huo ni pamoja na viongozi mashuhuri katika siasa, Sekali na makampuni binafsi kutoka nchini. Liberia, Nigeria, Tanzania, Cameroon, Rwanda, na wenyeji Afrika Kusini. 

Kongamano lijalo linatarajiwa kufanyika Agosti 2023 jijini Arusha, Tanzania.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mindi Kasiga akielezea uzoefu wa Tanzania kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia na uongozi katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) unaoendelea jijini Durban, Afrika Kusini. 
Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Afrika katika Uongozi (African Women in Leadership International Conference) ukiendelea jijini Durban, Afrika Kusini.
Kutoka kushoto ni Prof. Fortunata Makene Mkuu wa Sera na Utafiti kutoka Taasisi ya Uongozi Tanzania; Mkunde Senyagwa Mkurugenzi wa Mikutano na Masoko katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha; Festo Mramba kutoka AICC, Balozi Mindi Kasiga kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, mwanzilishi wa AWLO Dkt Elisha Attai , Bibi Happiness Godfrey kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini na Bi. Maria Mafie kutoka Bodi ya Utalii Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.