Thursday, September 15, 2022

MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR AFUNGA MKUTANO WA WANAWAKE NA VIJANA KATIKA BIASHARA WA AfCFTA


Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Masoud Othman akihutubia wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliomalizika tarehe 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Katika hotuba yake Mhe. Masoud Othman alisisitiza kuwa kauli mbiu ya mkutano huo isemayo "Wanawake na Vijana ni injini ya biashara katika Mkataba wa Eneo Huru Barani Afrika" ni kauli inayoishi na imekuja wakati sahihi ambapo biashara zinazofanywa na wanawake na vijana zimekuwa zikikua kwa kasi.

Pia amepongeza muamko mkubwa ulioneshwa na washiriki ambao wametoka maeneo mbalimbali barani Afrika kuja kushiriki mkutano huo na kufafanua kuwa mkutano huo ulikuwa na washiriki wasiopungua 5,000 pamoja na wafanyabiashara wapatao 100 walioshiriki maonesho ya biadhaa ambayo yalifanyika katika eneo la mkutano.

"Ni matumaini yangu kuwa kupitia kusanyiko hili kutatokea maafikiano na kuanzishwa kwa mawasiliano baina yenu na hivyo kuwawezesha kupeana uzoefu" alisema Mhe. Masoud Othman

Aidha, akaeleza mkutano huu umekuwa na manufaa mengi kwakuwa wanawake na vijana wanaojihusisha na masuala ya biashara wamepata nafasi ya kueleza hali halisi ya kuendesha biashara, biashara wanazozifanya, changamoto wanazokutana nazo na kushauri suluhisho la kila changamoto kwa uhalisia wake.

Vilevile akaeleza maarifa na michango yote iliyotolewa ina manufaa katika kuleta maboresho kwenye maeneo ya biashara na kuwezesha kutumia fursa zilizopo kikamilifu kwa maslahi ya Taifa na Afrika kupitia utajiri wa rasilimali zilizopo. 

Hivyo, akasistiza kuwa maoni na mapendekezo yaliyotolewa yatazingatiwa katika itifaki ya wanawake na vijana katika biashara ili kuwezesha fursa zilizopo kutumika kwa ustawi wa watu wake na kanda ya Afrika kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifuatilia hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Fatma Rajab akifuatilia hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Barani Afrika, Mhe. Wamkele Mene (AfCFTA) akipongeza muitikio mkubwa wa washiriki na kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utayari wake wa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliomalizika tarehe 14 Septemba 2022  Jijini Dar es Salaam.

Afisa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Namibia, Bi. Upendo Mwasha (katikati) akifuatili hotuba ya kufunga Mkutano wa Wanawake na Vijana katika Biashara katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika uliofanyika tarehe 12 hadi 14 Septemba 2022 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo.

Sehemu nyingine ya washiriki wakifuatilia hotuba ya kufunga mkutano huo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.