Thursday, September 22, 2022

DKT. MPANGO AKUTANA NA MKURUGENZI WA USAID

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na ujumbe wa Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power Jijiji New York Nchini Marekani

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango katika picha na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijiji New York Nchini Marekani


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na ujumbe wake katika picha ya pamoja na ujumbe wa Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijiji New York Nchini Marekani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power wakionesha zawadi ya picha ambayo Bi. Samantha alipatiwa na Dkt. Mpango baada ya kumaliza mazungumzo yao Jijiji New York Nchini Marekani

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power, Mazungumzo yamefanyika Jijiji New York Nchini Marekani .
 
Katika kikao hicho Makamu wa Rais ametaja hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya afya hususani afya ya mama na mtoto ambapo ameelezea kuanzisha programu mbalimbali za kuokoa maisha ya mama na mtoto kwa kushirikiana na wadau ikiwemo programu ya M- Mama. 

Amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa afya katika kuboresha huduma za afya na kuongeza juhudi katika ujenzi wa miundombinu ya afya ikiwemo vituo vya afya pamoja na hospitali.
 
Makamu wa Rais ameishukuru Serikali ya Marekani kwa kushirikiana na Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Uviko 19 ambapo nchi hiyo imetoa msaada wa dozi milioni  5 za chanjo ya ugonjwa huo.
 
Amesema serikali imeweka mkazo katika kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kuweka sera rafiki na kuunganisha taasisi zinazohusika na uwekezaji ili kuondoa urasimu kwa wenye nia ya kuwekeza Tanzania. Pia Makamu wa Rais ametaja juhudi zinazofanywa katika kuboresha miundombinu ya usafirishaji pamoja na nishati ili kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji.
 
Katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, Makamu wa Rais ameikaribisha USAID kushirikiana na Tanzania katika kupata teknolojia rafiki ya mazingira itakayowezesha wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi na kijamii bila kuathiri mazingira.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Shirika la Maendeleo  ya Kimataifa la Marekani (USAID) Bi. Samantha Power amesema Shirika hilo litaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuunga mkono juhudi mbalimbali za mageuzi hususani katika sekta ya afya na kilimo.
 
Bi Samantha ameongeza kwamba shirika hilo linaiunga mkono Tanzania katika kuifanya kuwa tegemeo la upatikanaji wa chakula kwa kuwezesha kupatikana kwa mbolea ya gharama nafuu itakayosaidia kuinua sekta ya kilimo.

Mhe. Dkt. Mpango yuko nchini Marekani kuhudhuria Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Dkt. Mpango atahutubia Mkutano huo  Alhamis tarehe 22 Septemba 2022.

 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.